Leo tujifunze maana ya halisi ya Alama ya Mnyama kabla hatujachukua jukumu la kupata chanjo[emoji120]

Kwahiyp Miungu 36 jumla yake ni miungu 666?
Mkuu, pamoja na jitihada zote za kuweka kanuni ya kimahesabu katika kutafuta jumla ya hiyo namba bado wewe huelewi!? Keeli nimeamini bado kuna watu wamepitia elimu za kimangumashi za hapa na pale. Hesabu za "Arithmetic & Geometric Progression" si ni za Form I & II?
 
Huwezi kujumlisha idadi ua miungu kwa hesaby za arithmetric kwani hapo ulichofanya ni cummulative summation na sio Jumla halisi. Hivi mkuu tukipiga kura watu 36 jumla zinakuwa kura 666? Mnaokoteza concept ili uongo wenu utimie. Nyie ndio Manabii wa uongo mtakao potesa yamkini hata wateule.
 
Mambo mengine mnajitesa bila Sababu...wewe una Miaka michache tu ya kuishi Dunian afu unahangaika na Dunia ya kufikurika!
Tenda wema,ishi na watu Vizuri.....Hiyo ndio Dini...hayo Mafumbo utayajua hukohuko!
Kuacha dhambi hawataki lakini wanahangaika na mambo yakufikirika. Eti yaani mpaka mtu aelewe hilo neno mpaka ahanagike huku na kule kutafuta maana. 😅😅😅
 
Huyo mnyama namfananisha na sirro
Wewe ndio umeongea. Mnyama halisi ni kama akina Thisss wanaoteka watu. Manabii wa uongo wanasakizia watu kesi na kadhalika. Wanyama mnawakumbatia mnahangaika na wanyama wa Daniel na Yohana
 
Alama ya mnyama ipo na ndio inakutambulisha kuwa wewe au fulani ni mfuasi wa shetani, na ndio maana ni rahisi kutambuana wao kwa wao maana utaiona hiyo alama kwenye paji la uso.

Sema nyakati hizi kwa vile sio nyakati za siku za mwisho wa dunia wengi wanaipokea kwa hila, unajua shetani yeye ni mzee wa hila, kwa vile nyakati hizi atumuoni shetani live ndio maana anatumia hila hivyo unajikuta umeipokea hiyo alama bila kujijua kuwa umepoikea ila Mungu akikuona katika ulimwengu wa kiroho anakuona unayo hiyo alama.

Mfano pale Eden kitendo Adam and Eve kufanyiwa hila na nyoka na wao kukubali kula lile tunda tayari katika ulimwengu wa kiroho walishaipokea alama ya mnyama na ndio maana walifukuzwa pale Eden.

Mfano mwingine watu wanspata alama ya mnyama kwa kuuza nafsi zao kwa shetani ili wawe matajiri au maarufu, wengine ni kwenye uchawi na ndio maana ni rahisi kwa mchawi kumtambua mchawi mwenzake.

Nyakati za mwisho wa dunia mnyama ataonekana live hatajificha tena kama hivi sasa, hivyo inatakuwa rahisi kwa wale watakaobaki kumtambua kwa urahisi tofauti na sasa, sasa kwa vile watakuwa wanamtambua watajaribu kukutaa kupokea hiyo alama ya mnyama maana wanamjua sasa, na yeye yaani mnyama atawalazimisha kwa kuwambia "chagua ufe au upokee chapa ya mnyama upone"

Sasa chanjo ya covid19 ni chapa ya mnyama? Ebu angalia mfanano huu

Kwenye covid19 "ukipata "chanjo ya covid19 hutakufa kwa corona ila usipo pata chanjo utakufa na corona"

Kwenye alama ya mnyama "chagua ufe au upokee chapa ya mnyama upone"

Kwa msio jua ni kwamba siraha ya mwisho ya shetani ni vitisho, sasa unaona kwenye corona kuna vitisho na kwenye alama ya mnyama kuna vitisho.

Sasa kote kwenye chanjo ya covid19 na kwenye alama ya mnyama wanasema upokee chanja/alama upone au usipokee chanjo/alama ufe. Waswahili wana msemo wao mwenye macho haambiwi tazama.
Rudi kasome Dini
 
Huwezi kujumlisha idadi ua miungu kwa hesaby za arithmetric kwani hapo ulichofanya ni cummulative summation na sio Jumla halisi. Hivi mkuu tukipiga kura watu 36 jumla zinakuwa kura 666? Mnaokoteza concept ili uongo wenu utimie. Nyie ndio Manabii wa uongo mtakao potesa yamkini hata wateule.
Mhh! Mkuu naomba kila mtu ashike kile anachokiamini, naheshimu mawazo na akili zako, na pia ruksa kwako kupuuzia kile ambacho mimi ninachokiamini.
 
Kuunganisha dini zote ulimwenguni na kuwa na siku moja ya mapumziko kwa ajili ya ibada ni sawa na historia ya "symbolic combination" ya miungu yote 36 ya Wakaldayo wa Babeli ya kale. Nguvu za Mungu wao mkuu jua ilikuwa ni sawa na nguvu ya miungu yote 36 ikiwekwa kwa pamoja, yaani;
1+2+3+4+......+34+35+36 = 666

Hizi hesabu na formula zake huwa zipo kitabu gani kwenye Biblia?
Msaada tafadhali, nahitaji kukua kiimani ila kama utanisaidia kupitia maandiko na siyo dhahania.

Sent from my Nokia 3.1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, ukiambiwa hesabu ya jina la mnyama ni hesabu ya kibinadamu. Je! Unafikiri hesabu hizi ni zipi zaidi ya hizi zinazotumika katika mazingira yanayomzunguka mwanadamu!?
 
Back
Top Bottom