Uhusiano wa biashara yako na nchi

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Utangulizi
Neno Nchi Kibiblia ni ardhi yenye mipaka Halali ya kiumiliki. Kuna tofauti Kati ya nchi na taifa , Taifa ni watu ambao wanania moja au lengo moja

Taifa la Israeli lilikuwa ndani ya nchi ya misri , kwahiyo taifa linaweza kuwa ndani ya Taifa jingine

Nchi inamilikiwa
Ardhi au nchi inamilikiwa kihualali na Mungu au Miungu , na anayemiliki Ardhi ndiye Mwenye mamlaka juu ya maamuzi yoyote katika eneo juu ya nini kifanyike au kutofanyika?

2 Wafalme 17:26 Kwa hiyo wakamwambia mfalme wa Ashuru, wakasema, Wale wa mataifa, uliowahamisha, na kuwaweka katika miji ya Samaria, hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi; kwa hiyo
amepeleka simba kati yao, na tazama, wanawaua, kwa sababu hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi.

Wakristo wengi wanapoingia kwenye biashara au kutokana na kutokujua au kutokukosa maaarifa hawajui kwamba Mungu anaweza kumiliki nchi na kuhamua Nani hauze au Nani hasiuze

Ile kwamba Una Mungu na unafanya biashara si kweli kwamba Mungu wako anamiliki na kutawala eneo unalofanyia biashara

Mungu anayemiliki nchi ndiye anayehamua Nani hauze na Nani asihuze? Watu wengi wanafunga na kuacha biashara na kupata hasara lakini hapo hapo wanapofunga biashara kuna watu wanafanya biashara hiyo hiyo Kwa mafanikio makubwa Sana , Kwa hiyo ile kwamba Una Mungu ina maana kwamba biashara yako utafanikiwa Tu

Ufunuo wa Yohana 13:16-17
[16]Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;

[17]tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
.
Ulishawai kujiuliza kwanini baadhi ya wakristo wanakwenda kanisani na kwenda kwa mganga?

2 Wafalme 17:41Basi mataifa hawa wakamcha BWANA, tena wakaziabudu sanamu zao za kuchongwa; na wana wao vile vile, na wana wa wana wao; kama walivyofanya baba zao, wao nao hufanya vivyo hivyo hata leo.
 
Hata Leo wako baadhi ya wakristo wanakwenda kanisani lakini wanakwenda kwa mganga? Wanadhania kwamba Mungu waliyenaye Hana uwezo wa kuwasaidia kupata wateja

Kwanini wakristo wanakwenda kwa waganga? Wakati Mungu wao ni Mkubwa kuliko Mungu wa waganga ?

Katika ulimwengu wa Roho kuna Sheria zimewekwa ambazo kazi yake ni kutuongoza katika Maisha ya ulimwengu wa mwili.

Maombi au neno la Mungu ambalo inaweza lilitumika kuponya magonjwa ? Haliwezi kutumika kuleta wateja au kukuletea faida ? Kwa hiyo Kwa sababu watu wengi hawajawai kumwona Mungu anawasaidia watu kwenye biashara wanazania kwamba Mungu hawezi kuwasaidia kwenye biashara ?

Mathayo 4:8-9 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.

Mungu tunayemuabudu Katika Kristo Yesu anaouwezo wa kukusaidia katika biashara unayoifanya , unachotakiwa ni kumwita Mungu katika hiyo biashara?

Kama unaouwezo WA kuchunguza chunguza na kuuliza uliza kwa watu juu ya mganga ambaye anaweza kuwasaidia watu Katika biashara? Unakosaje ujasiri was kuuliza uliza kwa watu juu ya Mungu Huyu katika Kristo Yesu aweze kukusaidia katika biashara yako?

Nataka kukwambia ewe mfanyabiashara mwenzangu Mungu anaweza kukupigania pia kwenye biashara yako na ukaona ushindi kama kuna watu wanategemea irizi katika biashara zao , wewe weka tumanini katika jina la Yesu

Matendo ya Mitume 10:1,6 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani, atakuambia yakupasayo kutenda.

Chukua hatua aliyofanya Kornelio Huyu Baba yeye alikuwa anatamani kumjua Huyu Mungu WA Israeli na nguvu zake, ili aweze kumsaidia katika Maisha yake ya kila siku akawa anatoa sadaka akimwomba Mungu kumjua

Unaweza kutumia sadaka kwa Mungu ili akupe maelekeza ya namna ya kukusaidia katika biashara yako, toa sadaka ukimwomba Mungu kuwa Mungu WA biashara yako na Mungu atakuonekania
 
Back
Top Bottom