Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,332
- 18,510
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, inaendelea leo Jumatano, Septemba 23, 2026, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. Mahakama kinatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi, mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru.
Hatua ya leo ni uwasilishaji wa maelezo ya mwisho (final submissions) kutoka pande zote mbili, baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wake kwa mashahidi 17 na upande wa utetezi kufunga ushahidi baada ya kuwasilisha mashahidi watano, akiwemo Lissu mwenyewe.
Katika hatua hiyo, upande wa Jamhuri utawasilisha hoja zake kuhusu ushahidi uliotolewa na kuieleza Mahakama kwa nini unaunga mkono mashtaka, huku Lissu, anayejitetea mwenyewe, akiwasilisha hoja za utetezi kuhusu ushahidi na masuala ya kisheria yanayohusu kesi hiyo. Mahakama ilielekeza mawasilisho hayo yafanyike kwa njia ya mdomo.
Baada ya maelezo ya mwisho kukamilika, hatua inayofuata itakuwa kusubiri Mahakama kupanga tarehe ya kutoa uamuzi. Hata hivyo, muda wa kukamilika kwa mawasilisho ya leo haujajulikana, hivyo pia haijabainika ni lini tarehe ya uamuzi itapangwa.
Nini unatarajia kusikia kutoka Mahakamani?
Updates kutoka Mahakamani
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika tayari amefika Mahakama kuu kwenye Kesi ya Tundu Lissu inayoendelea siku ya leo.
Mabalozi wa nchi mbalimbali tayari wameingia kwenye chumba cha Mahakama kufuatilia kesi ya Tundu Lissu.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Godbless Lema amefika Mahakamani muda huu kufuatilia kesi ya Tundu Lissu
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu amefikishwa Mahakamani
Wajumbe wa kamati kuu wakiwasili mahakamani
Tayari Mahakama imeanza, muda si murefu nawaletea live updates ambapo leo Lissu atahitimisha safari yake ya utetezi kwa kufanya majumuisho ya mwisho (Final Submission).
Wiki iliyopita tuliishia sehemu ya 433 kwahiyo, leo tunaendelea na sehemu ya 434
Leo hapa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMATaifa, Tundu Lissu inakuja kwa ajili ya mawasilisho ya mwisho yani Final Submission.
Kisheria huwa Mashahidi wa Pande zote wakishasikilizwa na kutoa ushahidi wao Mahakama inasikiliza pande zote kwa maana ya kutoa nafasi ya kufanya mawasilisho ya mwisho kwa namna walivyoiona kesi kupitia ushahidi ulioletwa na vifungu vya sheria vinasema nini?
Anasimama Karani anasoma namba ya shauri.
Anasimama Wakili wa Serikali Ajuaye Zengeli anatambulisha wenzake na kusema wako tayari.
Anasimama Mwenyekiti Mhe. Lissu nae anasema yuko tayari.
Leo ukimbi wa Mahakama umejaa sana watu wengine wamekosa nafasi wamebaki njee, Mwenyekiti Lissu wakati anaingia ameingia kwa vibe sana na ukumbi wote umesimama na kumpa heshima ya kumpigia makofi mengi sana huku wakiimba “Mwambaaa!… Mwambaaa!… Mwambaaa!… “
Tutegemee kupata shule ya sheria kuhusu kosa la Uhaini na kesi hii maana kawaida Final Submission na kwa mujibu wa Sheria.
Jaji Ndunguru anauliza anayeanza ni nani?
Lissu anasema kifungu cha 313 kinasema ambae anapaswa kuanza ni Mshitakiwa.
Jaji Ndunguru anasema haya endelea.
Lissu anaanza Final Submission.
Mnano Tarehe 08/09/2025 niliiambia Mahakama hii kwamba kesi hii itaamua kama kwa sheria za Nchi hii inawezekana kwa kiongozi wa Kisiasa au kwa mtu mwingine yeyote anaweza kuhukumiwa kifo kwa makosa ya kisiasa.
Leo mwaka mmoja baadae nimesimama mbele yenu kuwaambieni kwamba kwa Sheria za Tanzania, na kwa ushahidi uliotolewa Mahakamani jambo hilo haliwezekani. Naomba kurudia. [anarudia tena maneno hayo].
Haiwezekani kuhukumu Kiongozi wa kisiasa adhabu ya kifo au mtu mwingine yeyote for that matter kwa ushahidi ambao tumeusikiliza kwenye Mahakama hii.
Niko hapa kuwaonyesha kwamba hilo jambo haliwezekani.
Waheshimiwa Majaji nilikamatwa katika mji wa Mbinga Mkoa wa Ruvuma jioni ya siku ya Tarehe 09/04/2025 na nilikamatwa nikizungumza kwenye Mkutano halali wa hadhara wa CHADEMA, Chama ambacho nimekiongoza tangu tarehe 22/01/2025.
Baada ya kukamatwa huko nilisafirishwa usiku huo huo hadi hapa Dar es salaam.
Na mchana wa Tarehe 10/04/2025 nilisomewa mashitaka kwenye kesi mbili zilizofunguliwa dhidi yangu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Waheshimiwa Majaji katika kesi ya kwanza nilisomewa shitaka la Uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code.
Katika kesi ya pili nilisomewa shitaka la kutoa taarifa za uongo kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya makosa ya Mtandao.
Kesi ambayo imenileta mbele yenu leo hii inatokana na kesi ya kwanza ambayo nilisomewa mashitaka yake Kisutu yaani Uhaini.
Baada ya takribani miezi minne na nusu ya mashauri kabidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mkurugenzi wa Mashitaka DPP aliwasilisha taarifa kuhusiana na hilo shitaka la Uhaini. Hiyo ni taarifa ya tarehe 14/08/2025.
Taarifa hiyo (information) kwa maneno mengine unaweza kusema Hati ya Mashitaka inanituhumu kwa mambo yafuatayo:
Kwamba nikiwa na utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya Jamhuri hiyo nilitengeneza nia ya kuhamasisha umma kuwezesha kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nilidhihirisha nia hiyo kwa kitendo changu cha kutamka au kusema na kuchapisha maneno yafuatayo..
"……Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, wamasema hivi msimamo huu unaashiria uasi. Ni kweli, ni kweli kwasababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi na hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko kwahiyo tunaenda kukinukisha sana sana. Huu uchaguzi tutauvuruga, tutauvuruga kwasababu tunaenda kuuvuruga sana sana….”
Sehemu ya 435
Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Waheshimiwa Majaji haya maneno ninayoyasema yana kile kinachoitwa ellipsis nne yaani kabla ya maneno kuna ellipsis na kuna ellpsis kwenye neno la mwisho na katikati ya hayo maneno kuna ellipsis mbili.
Hizo ellipsis maana yake ni kwamba kuna maneno yameondolewa.
Sasa Waheshimiwa Majaji Mashitaka yanasema nilifanya kosa hilo katika Wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es salaam.
Wakati wa Preliminary Hearing mnamo Tarehe 22/09/2025 upande wa Mashitaka ulitoa maelezo ya ziada uliprovide additional information in support of the charge.
Waheshimiwa Majaji kwenye maelezo ya ziada yaliyotolewa upande wa mashitaka ulidai kwamba mimi ndo niliyeitisha Mkutano wa watia nia wa Chama Changu mnamo Tarehe 03/04/2025 ambapo nilisema hayo maneno.
Waheshimiwa Majaji maneno hayo yapo Ukurasa wa 131 wa record ya Mahakama.
Pia Upande wa Mashitaka ulidai mimi ndio niliyeitisha Waandishi wa Habari waliohudhuria kwenye Mkutano huo.
Na waandishi wa habari niliodaiwa kuwaita walidaiwa kutokea kwenye Vyombo vya habari vifuatavyo, Jambo TV, Clouds Media, The Chanzo, Mwanzo n.k haya pia yapo Ukurasa wa 131 wa records za Mahakama.
Pia inadaiwa kwamba hiyo kauli niliyoitoa kwenye mkutano huo ilihamasisha baadhi ya wananchi wa huo umma ambao walianza kuhamasishana katika maeneo mbalimbali yaliyotajwa kama vile Arusha, Kilimanjaro, Ruvuma, Dar es salaam na Mbeya.
Na walianza kuhamasishana ili kuzuia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kwa kutumia nguvu "Through violence."
Na baadhi yao inadaiwa walikamatwa na askari Polisi wakati wakitekeleza maelekezo yangu.
Maneno hayo yapo Ukurasa wa 132 wa Records za Mahakama, kwamba mimi nilisema maneno halafu huo umma ukahamasika na kuanza kuchukua hatua.
Na maelezo mengine ya ziada waliyoyaleta Jamhuri ( Hizi ni hoja za Awali yaani PH) kwamba maneno hayo niliyotoa yalikuwa amounted to Criminal offence yaani yalikuwa ni Uhalifu.
Na wakasema hayo matendo yaliripotiwa kwa Afisa Mkuu wa Upelelezi wa kanda maalumu ya Polisi Dar es salaam.
Kwenye hayo maelezo ya ziada kuna kitu nimekisahau na inadaiwa kuwa hayo maneno niliyosema kwenye mkutano vilevile niliyachapisha mwenyewe kwenye Chombo cha Habari kinachoitwa Jambo TV na yalirushwa moja kwa moja kwa umma.
Taarifa iliyowasilishwa Mahakamani pamoja na maelezo ya ziada ya mashitaka niliyoyasema ndio kiini cha kesi hii. They are the centre of this case.
Kwa vile yapo katikati ya huu mgogoro hoja zangu za leo na pengine kesho zinahusu hayo.
Hiyo taarifa, maelezo ya ziada yaliyoletwa na mashahidi wao pia.
Waheshimiwa Majaji kuhusiana na tuhuma hizi zilizopo kwenye information na maelezo ya ziada nina mambo yafuatayo ya awali ya kuyasema kuhusu hizi tuhuma.
Jaji Ndunguru anasema rudia...
Mhe. Lissu anasema
With regards to information and additional particulars given at the preliminary hearing, I have the following initial comments to make.
Nina kauli zifuatazo za kuzitoa za awali kabisa.
1. Sijawahi kuficha wala kukana maneno ninayodaiwa kusema. Mkiangalia ukurasa wa 97 wa record ya Mahakama Kabidhi Kisutu Tarehe 18/08/2025 niliiambia Mahakama Kabidhi Maneno yafuatayo: "It is true i stated those words in an open meeting, the issue is whether those words amount to commission of said offence of treason"
Suala sio nilisema au sikusema? Suala ni kwamba hayo maneno yanatengeneza kosa la Uhaini?
Waheshimiwa Majaji kuna kitu kingine muhimu nilisema "I did not said those words just once I repeated in Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe, Lindi and Mtwara."
According to the committal records na nikaendelea kusema the words calling to prevent 2025 election hayajawahi kuwa siri.
Na nikasema kwa kumalizia do these words constitute treason or any other criminal offence?
Yanatengeneza kosa la uhaini au kosa lingine lolote la jinai? Nilimalizia kwa kusema hivyo.
Sehemu ya 436

Waheshimiwa Majaji Mashahidi wangu wote pamoja na mimi mwenyewe vilevile wamesema kwa kiapo kwamba maneno haya yametolewa kwa nyakati mbalimbali ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mimi mwenyewe.
Haijawahi kuwa siri kabisa.
2. Kauli yangu ya pili ya awali ni kwamba utetezi wangu, my defence has never been that I am ashamed of what i said. Utetezi wangu haujawahi kuwa ninaona aibu kuyasema maneno niliyoyasema.
Huo haujawahi kuwa utetezi wangu, utetezi wangu na umekuwa siku zote kwamba nilichokisema sio uhaini.
Nilichokisema sio uhaini na sio kosa lolote la jinai kwa mujibu wa sheria za Tanzani na huo ndio umekuwa utetezi wangu since day one.
3. Kauli yangu ya 3 ya awali kabisa ni kwamba baada ya kusikiliza mashahidi 17 wa upande wa mashitaka kingereza after 17 prosecution witnesses and 16 defence exhibit and not a single prosecution exhibit the case for the prosecution is weaker today than it was than the day the information was filed.
Ni kwamba baada ya kusikiliza mashahidi wao 17 na vielelezo 16 vya utetezi na baada ya kutokuona kielelezo hata kimoja cha mashitaka leo ni dhaifu kuliko siku siku waliyoileta Mahakama Kuu.
Waheshimiwa Majaji kauli yangu ya 4 ya awali.
4. Iko hivi kama ambavyo nimeiambiwa Mahakama hii kuwa hii ni kesi ya 3 ya Uhaini katika historia ya nchi yetu katika miaka 65 ya hii nchi tunayoipenda. Angalau mimi naipenda na nimeitolea damu, hii ni kesi ya 3 ya Uhaini katika historia ya nchi yetu.
Ni kesi ya tatu kufunguliwa chini ya kifungu cha 39(2) cha Kanuni ya Adhabu. Waheshimiwa Majaji kesi mbili za kwanza za Uhaini. GREY LIKUNGU MATAKA NA WENZAKE 1970 na KHATIBU GHANDI na wenzake 1983
Zilifunguliwa chini ya kifungu 39(2) a, b, c ya Kanuni ya adhabu na zote zilihusu mipango ya kuipundua Serikali na kumuua Rais.
Tofauti na hizo kesi mbili za mwanzo hii ya kwangu imefunguliwa kifungu cha 39(2) d na uhaini wa hapa ni wa kuitishia serikali.
Hakuna kumuua Rais wala kuipindua serikali, hii ni kesi ya kwanza.
Kwasababu hii ni kesi ya kwanza ya Uhaini isiyohusu kumuua Rais whichever way you decide you are going to set a precedent.
Vyovyote vile mtakavyoamua mtaweka msingi wa kisheria kuhusu Uhaini wa kuitishia Serikali.
Wahehsimiwa Majaji mtaweka a precedent ambayo itaongoza Mahakama zetu kwa miaka mingi sana ijayo kama ambavyo Grey Likungu Mataka tuna miaka 50 leo tunatumia msingi uliowekwa na Grey Likungu mwaka 1970. You are setting the law for the future.
Kwahiyo Majaji hamtahukumu mtu mmoja kwahiyo mtaweka utaratibu wa kisheria utakaofuatwa miaka mingi ijayo. Waheshimiwa Majaji wangu sihitaji kuwakumbusha uzito wa huo mzigo mliobebeshwa. Hamuamui guilt ya mtu mmoja bali mzigo wa kisheria kwa masuala haya for many years to come.
Tumaini langu kwenu ni kwamba mtabeba mzigo huo mzito wa kihistoria bila upendeleo kwa ujasiri na kwa heshima ambayo imebebwa na viapo vyenu vya kazi ya Ujaji.
My hope is you will bare this hostoric burden with courage by your oath in office.
Hizo ni kauli zangu za awali sasa mniruhusu nizungumzie sheria. Hii sheria ya Uhaini ikoje na inataka nini?
Mhe. Lissu anapiga taratibu huku anakunywa maji. Mahakama imetulia hata ukiingiza mkono mfukoni watu wanakusikia. Majaji wamekuna hadi vichwa baada ya Lissu kumaliza hizo hoja zake za utangulizi. Muda huu sasa anaanza kuzungumza sheria.
Waheshimiwa kifungu kinasema mtu yeyote mwenye utii kwa Jamhuri na akatengeneza nia ya kuwezesha au kusababisha kuwezeshwa au anayetengeneza nia ya kuchochea, kushawishi au kushauri mtu yeyote au kikundi cha watu to effect kimoja wapo kati ya matendo yafuatayo yaani-;
Sehemu ya 437

Kuitishia Serikali ya JMT, Bunge au Mahakama ya JMT na anadhihirisha nia hiyo kwa kuchapisha maandishi au machapisho au kwa kitendo chochote dhahiri au kwa kitendo chochote kile atakuwa ametenda kosa la Uhaini na akipatikana na hatia anaweza kuhukumiwa adhabu ya kifo.
Sasa ni mambo gani muhimu yanayotakiwa kwenye kifungu nilichosoma cha 39(2)d yakithibitishwa mna mamlaka ya kutoa adhabu ya kifo?
What are the essential elements of the offence of treason under that provision of the law.
Jambo la Kwanza ni utiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani allegiance to the URT.
Jambo la pili ni kwamba kosa lilifanyika ndani ya nchi au kokote kule.
Jambo la Tatu ni kutengenezwa kwa nia ya kutenda kosa la Uhaini haiwezi kuwa nia ya kufanya kitu kingine. The formation of the intention to commit treasonous act.
Na kama ni ya kuchochea lazima huo uchochezi uwe ni wa kufanya kosa la uhaini na sio kuchochea watu kufanya wizi.
Jambo la nne, kama ni kosa la kuchochea basi awe ni mtu mmoja au kikundi cha watu. The target of instigation must be any person or a group of person na sio umma. Ni kikundi cha watu.
Sharti la tano ni kwamba hiyo nia ya kutenda kosa au kushawishi watu ni lazima idhirishwe kwa kuchapisha maandishi au machapisho of any writing or printing or by overt act or deed whatsoever.
Waheshimiwa Majaji sharti la 6 halipo katika kifungu cha 39(2) d bali lipo katika kifungu cha 10(2) kwamba hilo sharti lazima matokeo ya yaliyotakiwa kutokea kwenye hiyo nia ni lazima kuwe na malengo yaliyotakiwa kutokea kutonana na hiyo nia.
Kama sheria imetamka wazi wazi kuwa kosa fulani lazima lioneshe nia basi matokeo ya hiyo nia lazima yaonekane maana yake kama nia ni kuchochea kutengeneza kosa la uhaini lazima matokeo ya hiyo nia yaonekane na kifungu cha 39 kimesema habari ya nia.
Kama nia ilikuwa ni ya kufanya kosa na kosa hakuna maana yake hakuna kosa na nia inakuwa imekufa ndio maana yake.
Hili ambalo nimelisema sasa hivi halikuzungumzwa kabisa kwenye kesi ya Grey Likungu na Khatibu Gandi. Mahakama zote mbili were not drawn on the implication of the current provision of the law ndo maana nilisema mnaenda kuweka precedent ya sheria.
Na vilevile mtaona kwamba the attention of the court in those case were not drawn on the issue of instigation.
Mahakama hii ina hiyo fursa ya kujadili hili na kulitolea mwongozo kwa vyovyote vile Waheshimiwa Majaji you are decision will be developing the law na baada ya kivumbi kutulia tutapata sheria mpya.
Uzito wa innocence sio ya mtu mmoja tu bali ni Precedent.
Waheshimiwa Majaji baada ya kuwa nimeweka hizo parameters za hicho kifungu cha Sheria naomba nipendekeze kwenye masuala ambayo mnatakiwa kuyatolea uamuzi.
The following issues to be determined by this Court.
The information, the additional information and the evidence.
1. The first issue is whether the accused person convened the meeting as alleged? Inadaiwa kuwa mimi ndio niliyeitisha Mkutano wa Tarehe 03/04/2025 kama inavyodaiwa?
2. Whether the accused person invited members of the media to the said meeting? Je ni mshitakiwa ambae aliyeitisha Mkutano huo na kualika waandishi wa habari kama inavyodaiwa?
3. Is whether the accused person formed any intention to instigate any person or group of persons to obstruct the 2025 General Election for the purpose of intimidating the Executive?
Je nilichochea mtu au kikundi cha watu kuzuia uchaguzi huo kwa lengo la kuitishia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Sehemu ya 438

Na hapa anaendelea kuwaeleza Waheshimiwa Majaji masuala ambayo wanatakiwa kuyatolea uamuzi.
4. Is whether the word alleged spoken by the accused constitute any offence known to law? Je hayo maneno yaliyozungumzwa na mshitakiwa yanatengeneza kosa linalojulikana na sheria za Tanzania? Kama jibu ni ndio hilo kosa linalotengenezwa na hayo maneno ni kosa la Uhaini?
5. Is whether the words allegedly spoken by the accused constitute a deed under the law? Je maneno ni matendo? Imedaiwa kuwa yaliyozungumzwa ni matendo under the law of treason.
6. Is whether the accused published the alleged utterances in the Jambo TV YouTube account as alleged. Je mimi nilichapisha huko Jambo TV kama ilivyodaiwa.???
7. Is whether the Executive of the United Republic is intimidated by the word of the accused person?
8. Whether in the light of the answers of the foregoing issues the prosecution has proved the case on the standard required by the law? Kwa kuangalia majibu ya maswali yote kuanzia swali la 1 hadi la 7 Je upande wa mashitaka umethibitisha mashitaka yake kwa kiwango kinachohitajika na Sheria? Hiyo ndio issue.
9. What judgement should the court give in the light of the answers to the foregoing issues from no. 1 to 8?
Na hayo ndo maswali yangu na nitaanza kujadili swali moja baada ya jingine na kulitolea majibu moja baada ya jingine.
Waheshimiwa Majaji katika Tafakari yenu kuhusu ushahidi uliopo kwenye rekodi na sheria husika. Ninawaalika muongozwe na kanuni kuu zifuatazo za sheria.
In your consideration of the evidence and laws to be guided on the following principles:
Kanuni kuu za sheria ni hizi zifuatazo.
1. Ni kwamba statute with penal sanctions must be construed strictly in favour of the accused person. Sheria zinazotoa adhabu zinatakiwa kutafsiriwa kwa umakini mkubwa sio kama sheria za madai na hiyo strictly favour inatakiwa kuwa upande wa mshitakiwa. Kanuni hii mtaipata katika kesi zifuatazo.
a) Kesi ya zamani sana Rex vs Mwanangomeni (mfalme) 1933Vol. 9 EACA 134 to 135 ukurasa.
b) Kesi ya Baada ya Uhuru Amin S/o Mrisho vs Republic 1971 HCD 41 at page 42 Nassoro Mzava acting CJ as he then was.
c) Issa Hassan Uki vs Republic CA No. 129 CAT at Mtwara 2018 at page 23.
Hizo ni kesi zina support kanuni kuu kuwa sheria za jinai zitafsiriwe kwa uzito mkubwa upande wa mshitakiwa.
2. Kanuni kuu ya pili inasema offences are acts punishable by law, they are actions or omissions defined as crimes by the law. Yanayoitwa makosa kisheria umefanya kitendo kilichokatazwa na sheria na kama hakijakatazwa kisheria sio kosa na huwezi kushitakiwa nayo.
Msingi wa kanuni hii uko kwenye ibara ya 13(6)c ya Katiba ya JMT Mtu hawezi kuadhibiwa kwa kitendo ambacho sio kosa wakati anakifanya. Kifungu cha 5 cha Penal Code na kipo kwenye amri ya kwanza para 25 ya PGO kuwa makosa ni yale yaliyotajwa na sheria tu.
Kanuni kuu hii ipo kwenye uamuzi wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika kesi ya-;
Bahame Sitta na mwenzake vs Jamhuri CA 166/2019 CAT at Shinyanga 11/11/2022 page 13 to 14 Mr. Justice Kente.
Wakati mwingine inaitwa the principle of legality.
3. Kanuni kuu ya tatu ninayoipendekeza kwenu ni kanuni pendwa ya wanasheria kwamba he who alleges must prove.
Anayetoa tuhuma lazima athibitishe. Kanuni hii ipo kwenye kifungu cha 117(1) cha Evidence Act na maamuzi lukuki ya Mahakama zetu. Anayeshitakiwa hana wajibu wa kuthibitisha chochote.
4. Kanuni namba 4 ni kwamba in criminal cases the burden of proof lies to the prosecution side and that burden never shift at all. Huo mzigo hauhami at all.
Uamuzi wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika kesi ya Oscar Rwela vs Jamhuri CA no. 49/2013 CAT at Mbeya at page 13 Madam Justice Mjasiri.
Sehemu ya 439

5. Kanuni kuu ya nne ninayopendekeza kwenu ni kwamba the standard of proof required conviction is one of beyond any reasonable doubt. Vilevile hii ni kanuni maarufu kifungu cha 3(2) (a) cha Evidence Act.
6. Kanuni kuu ya 6 ninayoipendekeza kwenu inasema evidence must be assessed cumulatively and as a whole, rather than by examining each piece of evidence in isolatiin. Ushahidi unatakiwa kuangaliwa as whole. Kanuni hii utaikuta kwenye kesi ya Nguza Vikings alias Babu Seya na wenzake.
7. Kanuni Kuu ya 7 ninayoipendekeza kwenu inasema a conviction in a criminal case must be based on the strength of the prosecution case and not on the weakness of the defence case. Hatia inapatikana kwa nguvu ya ushahidi wa Jamhuri. Kesi ya Nguza Vikings ukurasa wa 25. Pia mtaikuta katika kesi ya Mohamed Mtupeni vs Republic na Vitalis Joseph vs Republic CA 384/2021.
8. Kanuni Kuu ya 8 ninayoipendekeza kwenu inasema When prosecution give contradictory evidence on a crucial point its effect is to render prosecutions evidence whole unreliable.
Yaani pale upande wa mashitaka unapotoa ushahidi unaojikanganya kwenye suala muhimu matokeo yake ni kuufanya ushahidi wa mashitaka kuwa hauaminiki.
Mtaikuta kwenye kesi ya Makonyo John alias Kibuna and 2 others vs Republic CA 305 CAT at Mwanza 2022 page 26. Justice Gareba. Kesi ya Hamis Said Adam vs Republic CA no. 529/2016 CAT at Arusha 2018 page 11 Mr. Justice Lila.
9. Kanuni kuu ya 9 ninayowaalika nayo muitumie
Kanuni hiyo ya 9 ambayo nawaalika muitumie inasema hivi:
Particulars of a charge or information must disclose the essential element or ingridients of the offence and where the definition of the offence charged specifies factual circumstances if the offence committed: they must be be included in the particulars of the offence.
Maelezo ya shitaka lazima yaoneshe viini muhimu vya shitaka na pale ambapo shitaka linahitaji mazingira ya kiushahidi basi lazima ziwe sehemu ya maelezo ya hilo kosa.
Mfano kama shitaka linasema nia ya chapisho lazima hilo chapisho lioneshwe kwenye mashitaka.
Hii ipo kwenye kesi ya Isdory Patrice vs R CA no. 224 of 2007 CA at Arusha October 2007 page 13.
10. Kanuni ya 10 zinahusu uhaini ni zifuatazo:
A) Inahusu Uchapishaji yaani Publication under sect. 39(2) means the act of sending out or sharing a writing or printing with the third part.
Huo uchapishaji wa mambo ya kihaini ni kitendo cha kutuma au kubadilishana maandishi kilichoandikwa au kuchapishwa na watu wengine. Haina maana zaidi ya writing or printing.
Picha na video hiyo sio publication kwa mujibu wa kifungu cha 39 na hii ipo kwenye kesi ya Grey Likungu Mataka at page 509 and 510.
Full citation ya hiyo kesi ya Grey Likungu Mataka ni 1971 vol 1 EA 495 na hii kanuni ipo katika page 509 na 510.
B) Kanuni ya pili specific to treason inasema hivi a conviction on a charge of treason require a prove of an overt act or deed Hatia kwenye kesi ya uhaini inahitaji uthibitisho wa kitendo cha wazi na sio maneno.
They must be a prove of an overt act or deed. Iko kwenye Khatib Gandi and others vs R 1996 TLR 12 Page 13 CJ Francis Nyalali. Ni lazima kuwe na uthibitisho wa matendo ya wazi.
(C) Kanuni ya tatu ya uhaini inahusu maneno inasema mere worda do not amount to overt act or deeds to a treason charge unless those words explain the treasonable conduct Maneno matupu hayavunji mfupa isipokuwa maneno hayo yanaelezea matendo ya uhaini. Hii ipo kwenye Khatib Gandi kwenye page 55.
(D) Kanuni ya nne inasema kuhusu maneno pia, the position that as a general rule words do not constitute overt act or deed apllies only to individual person hiyo kanuni kuwa maneno matupu sio uhaini inahusu walioshitakiwa kwa uhaini mtu mmoja. At page 67.
Sehemu ya 440

Sasa hizo ndio kanuni kuu za Sheria ambazo nawaalikeni ziwaongoze wakati mtakapokuwa mnatafakari ushahidi na sheria kwenye kesi hii.
Kwa ruhusa yenu sasa naomba sasa nijielekeze kwenye yale masuala niliyoyapendekeze kwenu zile issues 9 niliposema awali.
1. Issue ya 1 Je Mshitakiwa ndie aliyeitisha huo Mkutano wa Tar. 03/04/2025 alipozungumza hayo maneno ya kihaini?
Suala la nani aliyeitisha huo mkutano? Kwenye ukurasa wa 131 wa rekodi imedaiwa na upande wa mashitaka kwamba mnamo tar. 03/04/2025 kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti niliitisha mkutano na kuzungumza na watia nia katika makao makuu ya Chama Mikocheni.
Anamsomea huo ukurasa wa 131 Jaji ameuliza arudie.
Lissu anasema kwanini hili suala ni muhimu kwenye kesi hii kuhusu nani aliitisha huo Mkutano.
Wahehsimiwa Majaji kwenye kifungu cha 49 cha Kanuni ya Adhabu kinasema " in the case of any of the offences set out .....
Anasoma kifungu hicho kuwa kile kitendo cha kuwezesha kosa kufanyika kinahesabika kuwa ni tendo la wazi linalothibitisha hiyo nia.
Kwahiyo ukiitisha mkutano wenye lengo la kwenda kufanya kosa la jinai ni tendo ambalo linapaswa kuwa pleaded and proved. Kama niliitisha Mkutano that is an overt act kwamba niliitisha mkutano wa kwenda kutenda kosa la Uhaini.
Umeitisha Mkutano umeenda kuzungumza mambo ya Uhaini
Khatibu Gandi in a charge of treason you need to prove overt act kwahiyo kwamba niliitisha mkutano sio jambo la bahati mbaya walitaka ku prove overt act sio jambo la bahati mbaya.
Kwahiyo wanaposema nimeandaa mkutano they are not being innocent at all sio jambo lililorushwa kwa bahati mbaya.
Pia kama Mkutano ulikuwa ni wa kihaini walioshiriki kuuandaa pamoja na mimi wanakuwa ni core conspirator wanakuwa washiriki kwenye hilo kosa la Uhaini.
Na vilevile conspiracy is an overt act kwa mujibu wa Khatib Gandi na nilishirikiana na watu hiyo kula njama is another overt act na kumbukeni bila overt act hakuna uhaini.
Sababu nyingine ni kwamba kama mkutano ulisikilizwa kwa nia ya Uhaini na waliowezesha kurusha hayo matangazo wamefanya kosa la misprision of treason yaani wamewezesha kosa la uhaini.
All those persons who attended the meeting and heard the treasonous word being spoken all those who published or disseminated the words will be liable to be charged with the offence of misprison of treason in terms of sect. 41 of the Penal Code. Na adhabu yake ni kifungo cha Maisha.
Hoja yangu hapa kwamba suala la niliitisha mkutano au la nj suala muhimu kweli kweli.
Sasa Waheshimiwa Majaji ushahidi unasema kuhusu kuitisha Mkutano?
Katika Mashahidi wote 17 wa Mashitaka hakuna shahidi hata mmoja aliyetoa ushahidi wa namna Mkutano huo ulivyoitishwa. Absolutely none.
Wameleta tuhuma ambayo ikithibitishwa inatjibitisha tendo la wazi na wakaleta mashahidi 17 hakuna shahidi wao hata mmoja aliyeleta ushahidi wa nani aliyeitisha huo mkutano.
Upande wa Mashitaka walisema wangeleta na vielelezo kuthibitisha mashitaka yao. Vielelezo 11 viko ukurasa 135 wa record ya Mahakama, hakuna ushahidi wa maneno wala ushahidi wa nyaraka.
Ushahidi pekee uliopo kwenye rekodi za Mahakama ni ushahidi wa Utetezi na unasema hivi.
Ukurasa wa 660 wa rekodi DW 2 John John Mnyika unasema hivi "Mkutano ule uliitishwa na kuandaliwa na Sekretarieti ya Chadema Makao Makuu." aliwaambieni kuwa mkutano ule ulikuwa ni wazo lake mwenyewe.
DW 2 alisema yeye ndie aliyewaelekeza surbodinate wake DW3 na DW4 kuandaa huo mkutano. Na DW2 ameiambia Mahakama kwamba mimi na DW 5 John Heche Makamu Mwenyekiti Bara wa Chadema, tulikuwa waalikwa tu.
Sehemu ya 441

Waheshimiwa Majaji ushahidi huo wa DW2 umeungwa mkono na DW3 na DW4 yaani Amani Golugwa na Brenda Rupia ambao ni Naibu Katibu Mkuu Bara na Mkurugenzi wa Habari hawa ndio maafisa wa Chama walioandaa huo Mkutano.
Hii tuhuma kuwa ni mimi ndio niliandaa mkutano ni tuhuma ya uongo na ninachoweza kusema kwa upole ni kwamba haijathibitishwa kabisa. Na nikisema hivyo nasema kwa upole.
The answer to the first issue must necessarily be answered in negative. Jibu la swali la kwamba mtuhumiwa ndio aliandaa mkutano huo jibu lake ni HAPANA. Sio mimi niliyeandaa huo mkutano.
2. Naomba niende kwenye issue ya pili sasa.
Ni je ni mtuhumiwa ndie aliyealika waandishi wa habari kwenye huo mkutano wa Tar. 03/04/2025? Ndio swali linalopaswa kujibiwa.
Waheshimiwa Majaji suala hili pia ni muhimu sana kujibiwa.
Kama lengo la mkutano lilikuwa la kihaini kualika waandishi wa habari ili waje wacover huo mkutano basi hicho ni kitendo cha wazi yaani overt act.
Hivyo na waandishi wa habari waliokuja kwa mwaliko wangu wanakuwa accessory after the fact. Washirika wa kosa na misprision of treason itakuwa inawahusu. Hawawezi kupona kwenye kosa hilo.
Hii tuhuma sio ya bahati mbaya na haijaletwa bure ina lengo la kuthibitisha an overt act kwamba wakithibitisha overt act wanathibitisha kosa la uhaini. It is not innocent at all.
Waheshimiwa majaji tuhuma ya kwamba mimi ndio niliyealika huo mkutano ipo kwenye ukurasa wa 131 wa record za Mahakama Hii (Court Proceedings) mkiangalia walichokileta waendesha mashitaka kwenye preliminary hearing hawakusema clearly kwamba mimi ndie niliyealika waandishi wa habari. Kwenye hayo maelezo ya ziada.
The only say members of the media they were invited. Hawakusema walialikwa na nani?
Waheshimiwa Majaji i take it that not mentioning person of the media it was not dental to innocent haikuwa bahati mbaya na haikuwa innocent. Ilikuwa na nia mbaya na haikuwa innocent.
Wakati wa ushahidi walileta mashahidi wa kusema mimi ndio niliitisha waandishi wa habari. Mimi ndio nilialika hao waandishi wa habari.
PW 1 George Bagyemu alisema hivi wakati anaongozwa kwenye ushahidi wake ukurasa wa 147 wa rekodi. Alisema on this particular point said "Ni mtuhumiwa aliwaalika waandishi wa habari ili hotuba yake iweze kusikilizwa na watanzania na wasio kwenye jambo tv channel" kingereza mlichosema " accused person imvited journalist so that his speak to be heard by Tanzanians and non Tanzanias..
Waheshimiwa Majaji ushahidi wa PW 1 kwenye hoja hii uliungwa mkono na PW 2 Insp. John Kaaya kuhusu hoja hii angalia ukurasa wa 210 na 221 za rekodi ya Mahakama hii.
Waheshimiwa Majaji mtakumbuka nilimuhoji sana PW 1 and on this particular point alisema it is true that is you who imvited the journalist and i dont know the means used to invite them.
Jaji leo hatuna break?
Mhe. Lissu namalizia tu hapa.
Alijibu kuwa sijui ulitumia njia gani kuwaalika lakini ninachojua ni wewe uliyealika waandishi wa habari ukurasa wa 161 na ukurasa wa 210 na 221 PW2 nae aliunga mkono mambo haya.
Ushahidi wa PW1 na PW 2 ulipingwa na PW 16 na PW 17. The testimony of PW 1 and 2 was flately contradicted by the testimony of PW 16 and 17. Ulipingwa moja kwa moja na hao mashahidi wengine.
PW 16 Amin Mahamba ndie alikuwa mpelelezi mkuu wa kesi hii. Alisema yafuatayo kuhusu nani aliyealika waandishi wa Habari na ukurasa 467 wa rekodi. Anasema hivi
"P and P1 they said they instruxted by the director to go and record and live strim the accused speech meeting. John Marwa was informed and invited by director of information and publicity of Chadema Brenda Rupia"
Sehemu ya 442

Hao Waandishi wa Jambo TV aliyekuja kutoa ushahidi na yule ambae hakuja walipata taarifa kutoka kwa John Marwa aliyeambiwa na Brenda na niliwauliza kuwa mimi ndie Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA wakajibu Tundu Lissu sio Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chadema.
Waheshimiwa Majaji kwa upande wake PW 17 alisema nini for his part a protected witness who testified named P as PW 17 could not have been clearler about who invited the jouranlist to the meeting
PW 17 said that, ukurasa wa 439 "the information about the meeting was communicated to our director to our director John Marwa by the Chadema Communication Officer it is not true that the accused was the communication officer of CHADEMA.
Alisema pia the communication officer of Chadema is Brenda Rupia na akamalizia kwa kusema it is not correct for someone to say the meeting was organized by Tundu Lissu and that he was responsible for sending out the invitations.
Mtu akisema Mkutano uliandaliwa na Lissu na kwamba ni yeye ndie aliyetuma mialiko kwa waandishi wa habari. Hayo ni maneno ya PW 17. Ukurasa wa 496. Kwahiyo kwenye suala hili tuna hadithi mbili kwenye ulimi wa mashitaka.
Kuna ulimi mmoja unasema mshitakiwa ndio alialika waandishi wa habari na kuna sehemu nyingine inasema sio yeye. Hizi ndimi mbili za mdomo mmoja wa mashitaka ni kama ndimi za nyoka. Nyoka ana ndimi mbili.
Ni ulimi upi Mahakama hii iende nao? Wao upande wa mashitaka walipaswa kuwa na ushahidi wa aina moja.
Ni upande gani kati ya PW 1 na PW 2 au ule wa PW 16 na PW 17 tuuamini? Hasa kwenye suala crucial ambalo wao wamelileta kwamba mimi ndio nilialika waaandishi wa habari.
Kesi ya Said Hamis Adam Supra. Mahakama ya Rufani Tanzania ilisema kwenye ukurasa wa 11 Jaji Lila alisema "it is now settled that descrepancies and contradictions in the evidences of the witnesses are the bases for a finding of lack of credibility.
Ndimi mbili za aina hii hakuna ubishi tena ni uthibitisho kwamba huo ushahidi hauaminiki.
Waheshimiwa Majaji hii mikanganyiko ya upande wa mashitaka katika suala hili sio mdogo. Sio minor unahusu issue itself nani aliyealika waandishi wa habari?
Huo mkanganyiko wa suala lililotolewa ushahidi the contradictory is not minor or inconsequencial . The my are the major and they gk to the root of the issue on whether the accused invited the media personnel to the meeting. Sio jambo dogo kabisa.
Mahakama ya Rufani ilisema yafuatayo ilisema kwenye kesi ya Makonyo alias Kibona. Kwamba hii contradiction ni ndogo au kubwa ilisema hivi:
Mahakama ya Rufani ilisema ukurasa wa 26
"The law on inconsistent and contradictions is that where a part rises an issue that they were inconsistencies or contradictions in the evidence implicating him the duty of the trial court is to address the contradiction and determine whether they are minor or major contradictions. If the Court makes a finding that the contradictions are minor and inconsequential, it may go ahead to rely on the evidence as tendered. However if it find the inconsistent goes to the root of the case to the extent of shaking its very substractum the trial court shall not take that evidence and credible or reliable."
Mahakama inatakiwa ipime hiyo mikanganyiko na kuamua kuwa ni ya mambo madogo au ni mikanganyiko inayoenda kwenye mizizi ya kesi. Ukiwa ni mkanganyiko wa mambo ya msingi Mahakama haiwezi kuchukulia huo ushahidi ni wa kupuuzwa.
Jaji Ndunguru naomba uishie hapo.
Lissu naomba lisaa limoja na nusu niongee na Mawakili wangu pia nahitaji pia kupumnzisha miguu.
Jaji vipi Jamhuri?
Ajuaye: Hatuna shida.
Jaji basi twende tukapumnzike kwa huo muda tafadhali.
Inapigwa Court tukutane saa tisa kamili hapa kuendelea kula shule kutoka kwa Mh. Tundu Lissu.
Mahakama itaendelea Saa Tisa Kamili alasiri
MAHAKAMA IMEREJEA | Viongozi na Wanachama wa CHADEMA wakirejea Mahakamani baada ya mapumziko
Sehemu ya 443
Lissu anaulizia alipoishia.
Jaji Ndunguru anamkumbusha.
Sasa kwenye hiyo quotation naomba muweke kwenye blacket kuwa the same position was taken in the case of Mahomed Matura supra and in Marano Slaa Hofu.
Waheshimiwa Majaji kumalizia hiyo issue ya contradictory testimony of the prosecution witness. Kwasababu hizo contradictions na inconsistences zinahusu jambo kubwa linalohusu ushahidi wa prosecution.
Jambo kubwa la whether the accused person invited the journalist. The effect of this render the prosecution evidence unreliable. Ni ushahidi usiokuwa na thamani yoyote kabisa.
Waheshimiwa Majaji what about the defence testimonies on this issue?
Ushahidi wa utetezi umefuta shaka yoyote juu ya mshitakiwa kuwaalika waandishi wa habari kwenye mkutano wa tarehe 03/04/2025. Kama kulikuwa na doubt anywhere kwamba mshitakiwa alihusika.
Hiyo shaka haipo tena kutokana ba ushahidi wa utetezi. Ushahidi wa mashahidi wote wa Utetezi without exception unasema kwamba waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo walialikwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema Brenda Rupia.
Upo ukurasa wa 592 DW1, 661 mpaka 662 hui ni wa DW 2, na DW 3 upo ukurasa wa 693, DW 4 uko ukurasa wa 800 wa mwenendo wa shauri hili. Wote mashahidi hawa walisema aliyealika waandishi wa Habari ni DW 4 Brenda Rupia.
Crucially, that testimony was left intact no cross examination , haukuhojiwa hata mara moja. Hakuwa cross examined at all.
What is the effect of not examining on a particular point? Jibu lake lipo katika kesi ya Director of Public Prosecutions vs Justice Lumima Katiti na wenzake 3 CA No. 15/2018 CAT at Dar es salaam page 16.
It is a well known principle of law failure to examine on a material point of law is taken to be admission of the fact in question.
Kuna kesi zingine mbili on that principle. Nyerere Nyague vs R CA no. 67/2010 na Chora Samson alias Kiberiti vs Republic CA 516/2019.
Waheshimiwa Majaji kwa sababu hizi. Jibu la swala la pili je mshitakiwa aliwaalika waandishi wa habari kwenye mkutano huo wa Tarehe 03? Jibu lake ni negative. HAPANA.
The accused did not invite any of the media personnel who attended the meeting.
Kwa ruhusa yenu waheshimiwa Majaji nitaenda kwenye suala la tatu.
Nb. Kumbukeni yako maswali 9.
Je mshitakiwa alitengeneza nia ya kuchochea mtu yeyote au kikundi cha watu kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Waheshimiwa Majaji kwa kesi hii hili ni suala la kufa au kupona kwa kesi hii. Is a question of life or death with regard to a case at hand.
It is one of the central issue of the entire case. Taarifa iliyoko Mahakamani inayonishitaki inatuhumu kwamba nilitengeneza nia ya kuhamasisha umma. Anarudia tena KUHAMASISHA UMMA.
Kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waheshimiwa Majaji kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code ambacho kimetumika kunishitaki kinasema.
Mtu yeyote anayechochea mtu au kikundi cha watu.
Kinachochochewa ni mtu au kikundi cha watu.
Shitaka dhidi yangu linasema nimechochea umma. Waheshimiwa Majaji kifungu cha 39(2)(d) hakuna umma kuna mtu au kikundi cha watu.
Sasa Waheshimiwa Majaji hiki kinachoitwa umma ni kitu gani?
Kanuni ya adhabu imetoa tafsiri ya kimachoitwa neno umma. Public means kwa kifungu cha 5 Public refer to not only all persons but also to persons using particular place or to such indeterminate person to be affected by persons.
Umma ni watu wote na ni pamoja na watu wanaokaa mahali popote au wanaotumia eneo lolote ikiwemo Bar, Guest au vilabuni na ni pamoja na watu wote ambao huwezi kuwajua. Huo ndio umma ninaodaiwa kuuchochea uzuie uchaguzi.
Sehemu ya 444
Lissu anaendelea anasema
Waheshimiwa Majaji sheria inasema unachochea mtu au kikundi cha watu.
Mtu inajulikana sasa what is a group of persons? Natumia oxford advanced learners dictionary group means a number of leople who are together in certain place and connected in certain way.
It is not all. Watu wote hawawezi kuwa group of people. A group may be defined as a subset of all.
Nimeshitakiwa kwa kitu ambacho hakipo kisheria, sheria iko very specific.
Hili kosa lilivyokuwa drafted haiwezi kujibika. Hakuna mtu anayeweza kujitetea kwa watu wa namna hii. Wageni na wasio wageni walioko nyumbani kwao na wanaotembea. It is incapable of being defended.
Hii kesi haipo kwenye kifungu cha 39(2) cha Penal Code.
Waheshimiwa Majaji kwasababu ya upana wa hilo neno Public hilo neno Umma. Upande wa Mashitaka walikuwa na wajibu kisheria ku specify huo umma ni upi kwenye hati yao ya Mashitaka.
Ili kumuwezesha mshitakiwa kuandaa utetezi wake the orosecutio had a duty to specify what exactly that public alleged is? They did not so specify. In fact they had a duty to charge me to instigate a persons or a group of persons.
Wameleta mashitaka ambayo hayapo kwenye sheria.
Sasa turudi kwenye the first principle. Nilisema kitu kinachoitwa kosa la jinai ni kile kilichokatazwa na sheria. Sect. 5 an offence is an act attempt or an omission punishable by law.
Ni kitendo, jaribio au omission ambayo imetolewa adhabu na sheria. Kifungu cha 39(2) kimetengeneza kosa la Uhaini kwahiyo mtu anyechochea mtu au kikundi kuitishia Serikali.
Sheria haijatengeneza kosa la kuchochea watu wote yaani umma. Haipo hiyo.
Hakuna sheria inayosema ukichochea watu wote inasema mtu au kikundi kwahiyo nimekaa jela mwaka na nusu kwa kitu ambacho hakipo kwenye sheria za nchi hii.
Waheshimiwa Majaji ibara ya 13(6)(c) ya Katiba yetu inasema "ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa kitendo chochote ambacho alipokitenda kilikuwa sio kosa chini ya Sheria"
Nimeshitakiwa kwa kuchochea umma lakini hakuna sheria inayosema kuchochea umma bali inasema kuchochea mtu au kikundi cha watu. Nimekaa mwaka mzima kwa kitendo ambacho wala sio kosa.
Waheshimiwa Majaji nilisema PGO O. I para. 25 inasema crimes are actions defined as such by the laws.
Makosa ni matendo ambayo sheria imeyatamka kwamba matendo haya ni makosa. Kama sheria haijatamka kwamba tendo hili ni kosa. Haiwezi kuwa ni kosa kabisa.
Waheshimiwa Majaji kesi ya Bahame Sitta inaeleza kuhusu jambo hili.
Mahakama ya Rufani ilisema ilizungumzia principle of legality na ikasema kwamba
Walitumia Latin Marxim kwamba Nullum Crimen Sine Lege kwamba a person should not serve criminal punishment unless that act punishable by the law.
No one should be punishable by an act which is not punishable by the law at the time committed.
Kwenye kesi ya Bahame Sitta. The Appellants walishitakiwa kwa kuingia kwenye hifadhi ya taifa kinyume cha Sheria illegal entry into a National Park. There was no such offence. You cannot charge people on non existed offence.
Ninakabiliwa na kosa la jinai waheshimiwa Majaji ambalo ibara ya 28(4) ya Katiba kuwa Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria ni ule uliofafanuliwa na kifungu cha 29 cha kanuni ya Adhabu na 39(2) nilioshitakiwa nao mimi umesema ni uhaini gani napaswa kushitakiwa nao hili la kusema nimechochea umma sio kosa lililopo kwenye Sheria.
Waheshimiwa Majaji wakati nazungumzia principles nilisema kwamba penal statute must be construed stricly in favour of the accused.
Nilitaja kesi ya Rex vs Mwanangomeni. Sheria inasema wanawake hawatakiwi kulipa kodi ya kichwa. Na Mwanangomeni alishitakiwa kwa kutolipa kodi ya kichwa.
Mahakama kuu ya kikoloni ikasema penal statute must be construed strictly. Haiwezi kuwa kosa. Hiyo ilikuwa miaka 93 iliyopita. Wakati wa Ukoloni.
Sehemu ya 445 nitakuletea hapa.....
PART 445
Mhe. Lissu anasema kwenye kesi niliyoisema ya Uhuru ya Amin Son of Mrisho 1971 alipatikana na kosa la kawaida la wizi. Akahukumiwa kwa kosa lililopo kwenye Minimum Sentence Act. Mahakama Kuu ikasema HAPANA. A penal statute must be strictly construed unless expressly provided by the law and charged for it.
Usipomuhukumu mtu kwa kosa hilo huwezi kumshitaki kwa kosa hilo. Strictly construction of the penal statute inalinda uhuru wetu raia. Hawa wanaotutawala tukiwaachia, magereza yatajaa. Watasema umechochea umma wakati sheria inasema hakuna kitu kama kuchochea umma.
Waheshimiwa Majaji naomba nipendekeze uamuzi wa Mahakama hii kwenye kesi ya Freeman Aikael Mbowe and 7 others vs Jamhuri. CA/2020 Ni muhimu kwa Precedent na muhimu kwa ushahidi wa kesi hii.
Proof ni hii kesi ya Freeman Mbowe and 7 others for the purposes za kisheria. Sio umuhimu wake wa kuonesha namna wapinzani tulivyoonewa.
Kuanzia ukurasa wa 52 hadi 59 Jaji Mugeta. Facts were that the appellant were charged of making statements which caused hatred to lawful authority of the government.
Na maneno waliyosema pia lawful authority ni kitu gani?
Mahakama hii ilisema Lawful authority kwenye shitaka la aina hiyo the prosecution must specify what is the lawful authority targeted?
Lazima upande wa mashitaka wafafanue hicho kinachoitwa lawful authority ni kitu gani?
Kwenye kesi hii hii ya Freeman Mbowe ilicite the decision of the Court of Appeal in Isdory Patrice Supra. Na ikasema kwenye Isdory Patrice Mahakama ya Rufani the prosecution must always provide particulars to enable the accused person to prepare his defence.
Na Mahakama ya Rufani ilisema hati ya mashitaka isipotoa hizo particulars basi ni shitaka batili. Na kwa Freeman Mbowe shitaka waliloshitakiwa nao lilikuwa batili ndio Mahakama hii ilisema hivyo. Hawakuambiwa Lawful authority ni kitu gani?
Sasa waheshimiwa Majaji kuna sababu mbili zinazofanya the information iliyopo Mahakamani kwenye kesi hii kuwa na makosa yale yale ambayo Mahakama hii iliyaona kwenye kesi ya Freeman Mbowe na Isdory Patrice.
Sababu hizo mbili za kusema shitaka hili ni batili ni hizi zifuatazo:
1. Sababu ya kwanza ni ile ambayo nimeielezea kwa kirefu kuwa Sec.39(2)(b) haijasema kuinstigate members of the public bali imesema a person or members of the public. In terms of Bahame Sitta and Isdory Patrice.
2. Sababu ya pili ya kwanini shitaka ni batili vilevile nimezungumzia kuwa hilo neno public ni pana sana na hati ya mashitaka haijadisclose hiyo public ni ipi? Walioko vilabuni, sokoni au eneo lingine lolote. Walitakiwa kuniambia.
Kama hawajafanya hivyo basi kosa ni batili na shitaka ni batili hili.
Linakiuka hiyo principle ya legality la uhalali wa kosa kisheria.
Kwahiyo Waheshimiwa Majaji katika suala hili la tatu, on this third issue on the first limb ya to instigate any person or group of person is NEGATIVE. Sijachochea mtu wala kikundi cha watu.
Hakuna kitu kama kuchochea umma.
What about the second limb of this issue?
Sehemu hii inasema hivi lengo la hiyo instigation. Shitaka linasema nilichochea umma kwa nia ya kuzuia uchaguzi mkuu.
The objective ya huo uchochezi wa umma ilikuwa ni kuzuia uchaguzi Mkuu. Sasa Sheria inasemaje?
Kuhusu hiyo intention to instigate sheria inasema any person who form intention to instigate person or group of person.......
Hapo inasema lengo ni INTIMIDATION TO EXECUTIVE.
The intention to instigate person or group is to effect the intimidation of executive.
Mimi nimeambiwa nimeinstigate umma kuzuia uchaguzi.
Sheria inasema nimeinstigate umma kuitishia Serikali.
Narudia tena for effect.
Waheshimiwa Majaji nimesema shitaka ni muhimu kulisoma the accused person forms an intention kuwezesha kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025.
Sheria inasema unachochea mtu au kikundi cha watu kuitishia Serikali na sio kuzuia uchaguzi Mkuu.
Part 446 itaendelea kwenye post inayofuata.
PART 446
Halafu baadae ndio wanasema kutishia Serikali. Hili lengo lao la kuzuia uchaguzi halipo, lengo kama hilo kwenye sheria za nchi yetu.
Clearly on this ground too nimeshitakiwa kwenye kitu ambacho hakipo Kisheria.
Waheshimiwa Majaji, tatizo la tatu la hiyo charge sheet ni hii inayoitwa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maana naambiwa nimewachochea watu waitishie.
Swali hili ni muhimu lijibiwe kwasababu nilizosema zimeelezwa kwenye Isdory Patrice. Reason to disclose particulars so that the defence could prepare their own defence.
Hili sio jambo rahisi kama walivyodhani hawa Upande wa Mashitaka.
Hiyo Serikali imeelezwa kwenye Katiba ya Nchi yetu. Hilo neno Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sura ya Pili ya Katiba inaelezea hiyo Serikali ya JMT.
Hiyo Serikali ni pamoja na watu wafuatao: Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na viongozi wengine hadi watendaji wa vijiji na kata huko chini kabisa ni Serikali.
Ukisoma ibara ya 59 DPP pia ni Serikali na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Baraza la Mapinduzi Zanzibar ni Serikali na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nayo ni Serikali.
Sura ya 6 yote ya Katiba nayo ni Serikali.
Waheshimiwa Majaji, sura ya nane inahusu Local Governments nayo ni Serikali.
Waheshimiwa Majaji, sura ya 9 majeshi ya ulinzi, Polisi, Magereza, JWTZ hiyo nayo ni Serikali.
Ili kuonesha kwamba sizungumzii off my head, naomba angalieni ibara ya 151 ya Katiba. Hii ni pamoja na Serikali ya Muungano, ile ya Zanzibar na mtu yeyote anayetekeleza majukumu yake.
Kwahiyo upande wa mashitaka walitakiwa kuniambia from the President to Village Executive Officer. Hao watendaji wa vijiji should have disclose in the information hiyo Serikali iliyotishiwa ni ipi?
Rais, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais, Mapolisi au ni nani? Nilimtishia nani haswaa? Mwenyekiti wa Kijiji gani hicho niliyemtishia?
Sasa Waheshimiwa Majaji, katika mazingira hayo hii hati ya mashitaka, hii information ambayo inazungumzia public wakati sheria inasema to instigate person or group of person, hati ambayo haisemi who is this animal Executive?
Isdory Patrice imesema you must provide particulars. How can it be in light of the case of Freeman Mbowe na Isdory Patrice?
Nafahamu Freeman Mbowe ni maamuzi ya Mahakama hii, haiwalazimishi, lakini alisema ili kulinda haki za watu ni lazima watoe particulars ili kosa lieleweke kwa mtuhumiwa.
Nimejulishwa kwamba saa 11 imefika. Kesho nataka nizungumzie ushahidi ulioletwa kuhusu jambo hili.
Kwahiyo nitaendelea kesho.
Ajuaye anasema kuwa tuendelee kesho, lakini mshitakiwa azingatie huo muda wa siku mbili uliobaki.
Mh. Tundu Lissu anasimama kuwa hili sio suala la kwangu pia ni majaji pia. Hii ni kesi ya adhabu ya kifo. I must defend myself with all what I have.
NB: Wao wamepoteza muda mwaka mzima kwenye hii, leo inawauma Lissu kufanya final submission hadi kesho na siku yote ikakamilika?
Majaji wanateta na watu wanasonya humu wamekerwa na kauli ya Ajuaye.
Majaji wanateta pale juu.
Jaji: Tunasisitiza huko mwanzoni kuwa wakati sisi tunaendelea na shauri hili tunaobserve utulivu kwamba tusipige makofi sana wakati watu wengine wanapotumia Mahakama hii na shauri linaahirishwa hadi kesho saa tatu asubuhi.