Leo ningependa kushare nanyi juu ya haya maisha ya Baharia

buzitata

JF-Expert Member
Apr 11, 2017
1,997
7,068
habar zen wandugu

Leo ningependa kushare nanyi juu ya haya maisha

Baharia ninayemzungumzia hapa ni Yule anayefanya kazi kwenye meli

Kufanya kazi kwenye meli Kuna changamototo nyingi Kwanza zinaanzi namna ya kupata kazi pia kazi yenyew huwa inachangamoto kidogo

Nakumbuka first time nilipata mchongo wa kwenda mbele ila Kama unavojua Tena wabongo Mambo yetu huwa ni ya kuunga unga tu..bas nikaingia Chaka nikatengeneza bonge la CV ili nipate kazi kirahisi na wakati sijawah panda meli hata siku moja😁😁😁. Jamaa walivoona cv yangu imenona wakanichukua fasta bila ubish, ila moyon nilikua najua nimefoji CV (hiyo kitu kwa mabaharia ni kawaida coz hatuna mfumo mzuri wa mtu kupata kazi hata kama amesoma)

Siku ya siku nikaona simu inaingia naangalia nakuta namba si ya bongo, basi nikajibanza sehem ile napokea tu nakutana na lugha iliyopanda ndege lahaulaaaa nilijikanyaga ile siku na kingereza Cha kuunga unga na tukaelewana coz jamaa aliniuliza tu upo tayar kusafiri kesho mi nikasema tu (yah I'm ok sir) yaan Kila kitu ilikua yah yah yah mpaka mwisho

Kweli bwana jamaa baada ya kukata simu haikupta Kama lisaa iv nikachek kwenye email nikakutana na attachment nne moja wapo ilikua ni ticket ya ndege (hapo ujue mwananzengo nilikua sijawah kuiona ndege ikiwa karbu yang nilikua naziona kwa mbali tu). Nikajipinda hiyo siku kuelekea pale kwa nyerere nikakwee pipa for the first time.

Kwa nyerere nilipata usumbufu kidogo ila kwa kudra za mwenyez mungu wakaniruhusu nikwee pipa

Tulitumia Kama masaa 7 au 8 iv had kufika kule.. nikapokelewa na jamaa zen akanibwaga hotel zen yeye akasepa zake akanambia tu ushalipiwa Kila kitu na utakaa hapo kwa wiki Moja...tatizo lilikuja kwenye vyakula Kila coz ile hotel wanakula kea bufee so unaenda tu unapojiskia zen unapakua bila kumuuliza mtu, Sasa mm mshamba wa keko machungwa nimezoea nikifunua poti nakutana na ugali samak kule Kila ninachofunua nilikua sikijui mwisho wa siku nikajikuta nashindwa soseji na nyanya tu😁😁😁

Wiki ilivoisha nikapelekwa melini huko ndo kimbembe kiaanza had nikahs kibarua kitaota nyasi

Jamaa walinipokea na wananiuliza una experience ya muda gan? Mi nikalopoka tu 3yrs na wakati ukweli sijui hata kitu.. chief engineer akapitia CV yangu coz mi nilikua upande wa engineering, bas jamaa akasema Mr buzitata unaonekana upo vizuri na hii meli itakua ndogo Sana kwako hivyo tunakuamin nenda kabadilishe nguo zen ingia engine room ukaanze kazi

Kijana wa watu nikaenda kubadilishana nguo nkapga ovaloli Lang zen nkawa nashuka na ngaz naelekea chumba Cha mitambo kilipo

Lahaula wandugu nilichokiona ilibid nirudi juu fasta nikijiuliza hi kazi nitaiweza kwel😂😂 coz nilikutana na maengine makubwa Yan hata sikuwah kufikiria KWAMBA melin Kuna vtu vikubwa Kama ivo, hapo kaa ukijua jamaa wananiamin coz wakichek CV yangu ilivonona walijua wamepata bonge la jembe kumbe wamepata mpini😁. Nikaingia mzigoni hapo sijui pump zipo wap Wala compressor zilipo ila nilikua nazipita tu coz kutokana na ukubwa wake Wala sikuwaza KWAMBA HV ni vitu gan

Mungu si athuman mule melini kulikua na jamaa anatokea Egypt na kama unavojua Egypt ipo Africa so jamaa akanichukulia Kama wakunyumba ndo akaanza kunipa michoro na kunielekeza Mambo mbalimbali.. baada ya mwezi mmoja nikawa fiti Kila Kona naijua na maisha yakawa mepesi tu

Tatzo lilianza baada ya kamaliza miez sita, kule melin Kuna kitu wanaita home sick(fever) yaan unakua unataman kurud nyumbani tu kwenye hiyo Hali ndo watu wanaweza kutukanana bila sababu... Nashukuru mungu ile fever kwangu ilidumu kwa muda mfupi tu zen ikatoweka na maisha yakaendelea

Nimejitahidi kufupisha Mambo mengi Sana hapo ila Kama una swali uliza

Hi kazi ukishaizoea utaipenda balaa ila tu jitahidi Kama hujaoa basi hakikisha unavoondoka bongo usiache Dem ili asikufanye ukapatwa na home fever mapema.
 
hahhhahahaha, watu wamesoma CV tu wamekupa kazi haya tueleze huo mtemba wa kwanza ulikuwa KW ngapi propelling force, Generators KVA ngapi na Engine type and model..

Ulipataje kazi ya meli ukiwa 3yrs experience bila kuulizwa signed sea book. Maana wakati mwingine melini CV haifanyi kazi ila seaman book ndio inaonyesha experience.. Hiyo hiring process hata pale Greece kwa wasoteaji au dubai haipo dah ulikuwa na bahati kama ni kweli tena Engine room and I hope hukuwa oiler..
 
Mkuu unamaanisha hata chuo hukuwahi kusoma kuhusu meli?
Yaani ulitokea kitaa na cv zako za kuunga hadi kwenye mitambo ya meli ukaelekezwa mwezi mmoja tu ukawa expert
 
hahhhahahaha, watu wamesoma CV tu wamekupa kazi haya tueleze huo mtemba wa kwanza ulikuwa KW ngapi propelling force, Generators KVA ngapi na Engine type and model..

Ulipataje kazi ya meli ukiwa 3yrs experience bila kuulizwa signed sea book. Maana wakati mwingine melini CV haifanyi kazi ila seaman book ndio inaonyesha experience.. Hiyo hiring process hata pale Greece kwa wasoteaji au dubai haipo dah ulikuwa na bahati kama ni kweli tena Engine room and I hope hukuwa oiler..
Mkuu baharia ukiambiwa cv inamaanisha mpaka seeman book lazma iendane na CV. Nadhan utakua umenielewa. Na niliingia Kama oiler
 
Mkuu unamaanisha hata chuo hukuwahi kusoma kuhusu meli?
Yaani ulitokea kitaa na cv zako za kuunga hadi kwenye mitambo ya meli ukaelekezwa mwezi mmoja tu ukawa expert
Chuo nilisoma long course na vyeti vyote nilivonavyo ni og ila makeke niliyafanya kwenye experience tu
 
Aah hapo sawa..
Tanzania tunasema cheti kwanza experience tutakutana nayo kazini.
Wabongo wengi kazi tunajifunzia huko huko site
Na ndomana sikuchukua muda mrefu kuweza kujua coz kichwani nilikua nimebeba theory tu..na hata huyo jamaa alokua ananipa maelezo alishangaa how nimechukua muda mfupi coz ashawah kunambia Kuna jamaa alikaa nae miez 6 ila bado akawa hayupo fiti
 
Kwenye meli huko ukitaka kupiga pumbu inakuaje mkuu
Watu huwa wanajilipua wenyew tu kupitia mikono yao. Ila Kuna baadh ya meli hasa zile wanazolipa hela mkononi mkifika port unaweza ukatoka zen unanunua Malaya unajipigia zako kiroho safi
 
Mkuu malizia hii stori kwanza halafu ndio masuali yafate.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Naskia mnakuwaga na roho mbaya sana nyie mnaoshinda kwenye engine huko,tatizo nini?
 
Back
Top Bottom