Leo ningependa kushare nanyi juu ya haya maisha ya Baharia

Hiyo kazi naipenda sana Ndio mmasai wa Kwanza kupenda kazi ya ubaharia
 
hahhhahahaha, watu wamesoma CV tu wamekupa kazi haya tueleze huo mtemba wa kwanza ulikuwa KW ngapi propelling force, Generators KVA ngapi na Engine type and model..

Ulipataje kazi ya meli ukiwa 3yrs experience bila kuulizwa signed sea book. Maana wakati mwingine melini CV haifanyi kazi ila seaman book ndio inaonyesha experience.. Hiyo hiring process hata pale Greece kwa wasoteaji au dubai haipo dah ulikuwa na bahati kama ni kweli tena Engine room and I hope hukuwa oiler..
Daaahhhh we ni baharia aiseeee ila naomba unithibitishie kua wewe sio le nyenyenyeeeee.
 
Wafanyakazi wote wa kwenye meli wana elimu husika na hiyo kazi?
Vipi kwa wale wasio na vyeti hkuna kazi zao huko chini?
 
Wafanyakazi wote wa kwenye meli wana elimu husika na hiyo kazi?
Vipi kwa wale wasio na vyeti hkuna kazi zao huko chini?
Yah inatakiwa wawe na elimu husika...
Kwa MFANO kule saudia Kuna wajomba wanaitwa ARAMCO, hao jamaa wakikubaini lazima utimuliwe na always hakuna campun itakayokuajili bila kuwa na vyeti
 
habar zen wandugu

Leo ningependa kushare nanyi juu ya haya maisha

Baharia ninayemzungumzia hapa ni Yule anayefanya kazi kwenye meli

Kufanya kazi kwenye meli Kuna changamototo nyingi Kwanza zinaanzi namna ya kupata kazi pia kazi yenyew huwa inachangamoto kidogo

Nakumbuka first time nilipata mchongo wa kwenda mbele ila Kama unavojua Tena wabongo Mambo yetu huwa ni ya kuunga unga tu..bas nikaingia Chaka nikatengeneza bonge la CV ili nipate kazi kirahisi na wakati sijawah panda meli hata siku moja😁😁😁. Jamaa walivoona cv yangu imenona wakanichukua fasta bila ubish, ila moyon nilikua najua nimefoji CV (hiyo kitu kwa mabaharia ni kawaida coz hatuna mfumo mzuri wa mtu kupata kazi hata kama amesoma)

Siku ya siku nikaona simu inaingia naangalia nakuta namba si ya bongo, basi nikajibanza sehem ile napokea tu nakutana na lugha iliyopanda ndege lahaulaaaa nilijikanyaga ile siku na kingereza Cha kuunga unga na tukaelewana coz jamaa aliniuliza tu upo tayar kusafiri kesho mi nikasema tu (yah I'm ok sir) yaan Kila kitu ilikua yah yah yah mpaka mwisho

Kweli bwana jamaa baada ya kukata simu haikupta Kama lisaa iv nikachek kwenye email nikakutana na attachment nne moja wapo ilikua ni ticket ya ndege (hapo ujue mwananzengo nilikua sijawah kuiona ndege ikiwa karbu yang nilikua naziona kwa mbali tu). Nikajipinda hiyo siku kuelekea pale kwa nyerere nikakwee pipa for the first time.

Kwa nyerere nilipata usumbufu kidogo ila kwa kudra za mwenyez mungu wakaniruhusu nikwee pipa

Tulitumia Kama masaa 7 au 8 iv had kufika kule.. nikapokelewa na jamaa zen akanibwaga hotel zen yeye akasepa zake akanambia tu ushalipiwa Kila kitu na utakaa hapo kwa wiki Moja...tatizo lilikuja kwenye vyakula Kila coz ile hotel wanakula kea bufee so unaenda tu unapojiskia zen unapakua bila kumuuliza mtu, Sasa mm mshamba wa keko machungwa nimezoea nikifunua poti nakutana na ugali samak kule Kila ninachofunua nilikua sikijui mwisho wa siku nikajikuta nashindwa soseji na nyanya tu😁😁😁

Wiki ilivoisha nikapelekwa melini huko ndo kimbembe kiaanza had nikahs kibarua kitaota nyasi

Jamaa walinipokea na wananiuliza una experience ya muda gan? Mi nikalopoka tu 3yrs na wakati ukweli sijui hata kitu.. chief engineer akapitia CV yangu coz mi nilikua upande wa engineering, bas jamaa akasema Mr buzitata unaonekana upo vizuri na hii meli itakua ndogo Sana kwako hivyo tunakuamin nenda kabadilishe nguo zen ingia engine room ukaanze kazi

Kijana wa watu nikaenda kubadilishana nguo nkapga ovaloli Lang zen nkawa nashuka na ngaz naelekea chumba Cha mitambo kilipo

Lahaula wandugu nilichokiona ilibid nirudi juu fasta nikijiuliza hi kazi nitaiweza kwel😂😂 coz nilikutana na maengine makubwa Yan hata sikuwah kufikiria KWAMBA melin Kuna vtu vikubwa Kama ivo, hapo kaa ukijua jamaa wananiamin coz wakichek CV yangu ilivonona walijua wamepata bonge la jembe kumbe wamepata mpini😁. Nikaingia mzigoni hapo sijui pump zipo wap Wala compressor zilipo ila nilikua nazipita tu coz kutokana na ukubwa wake Wala sikuwaza KWAMBA HV ni vitu gan

Mungu si athuman mule melini kulikua na jamaa anatokea Egypt na kama unavojua Egypt ipo Africa so jamaa akanichukulia Kama wakunyumba ndo akaanza kunipa michoro na kunielekeza Mambo mbalimbali.. baada ya mwezi mmoja nikawa fiti Kila Kona naijua na maisha yakawa mepesi tu

Tatzo lilianza baada ya kamaliza miez sita, kule melin Kuna kitu wanaita home sick(fever) yaan unakua unataman kurud nyumbani tu kwenye hiyo Hali ndo watu wanaweza kutukanana bila sababu... Nashukuru mungu ile fever kwangu ilidumu kwa muda mfupi tu zen ikatoweka na maisha yakaendelea

Nimejitahidi kufupisha Mambo mengi Sana hapo ila Kama una swali uliza

Hi kazi ukishaizoea utaipenda balaa ila tu jitahidi Kama hujaoa basi hakikisha unavoondoka bongo usiache Dem ili asikufanye ukapatwa na home fever mapema.
nimeishia njian kusoma baada ya kuona uandishi wako tu wa hizo Zen zen zako nikagundua we bado mtoto kwa hio hizo enzi unazozungumzia we hukuwepo
 
nimeishia njian kusoma baada ya kuona uandishi wako tu wa hizo Zen zen zako nikagundua we bado mtoto kwa hio hizo enzi unazozungumzia we hukuwepo
Mkuu kuelewa hilo ni jukumu lako
Kila mtu Kuna maneno common ambayo ameyazoea kuyatumia so kuhusu zen huo ndo uandishi wangu ulivyo kwenye thread zote
 
Ulisoma chuo gani ambacho hamkua mnaenda field,ninavyo jua vyuo vya ubaharia field ndio inachukua muda mrefu kuliko kitu chochote.
 
Ulisoma chuo gani ambacho hamkua mnaenda field,ninavyo jua vyuo vya ubaharia field ndio inachukua muda mrefu kuliko kitu chochote.
Nmesoma dmi na nikilitaja jina langu hapa kwa wale walosoma 2014 watakua wananijua coz nishawah kuwa kiongoz matata Sana hapo hata walimu nikienda wanalikumbuka jina langu had leo

Kuhusu suala la field mkuu hyo experience ya field ukisema uitumie kuombea Kaz utasumbuka Sana coz meli nying za bongo Zina horse power ndogo.... All in all mi field zangu zote had namaliza chuo nilifanyia bandari na nilishauriwa nisitumie mihuri ya bandari so ikabidi nijilipue upande wa pili coz unafanya field miez 3 ukijumlisha mpaka unamaliza chuo unapata miez 6....kwa akili ya kawaida tu Nani atakuajili kwa miez sita yako? Jibu kaa nalo mwenyewe
 
Meli ni kama kiwanda,nina hakika kuingia melini ni lazima uwe umepitia darasani,hiyo kampuni iliyokuajir nayo ni magumashi bana,kampuni za uhakika haziajiri baharia mwenye CV feki,kwa ajili usalama unapokua kazini,kwaiyo CV zote nilazima zipitie kwenye cestem ya ukaguzi,ili kupata mtu sahih anaejua majukumu yke ya kazi na sheria zote za meli.
 
Mkuu baharia ukiambiwa cv inamaanisha mpaka seeman book lazma iendane na CV. Nadhan utakua umenielewa. Na niliingia Kama oiler

Mkuu seaman book ni certified document ambayo iko signed and stamped kama passport, CV ni piece of paper tu ambayo unajiandikia na inaweza ukawa umedanganya tu mpaka followup ifanyike kuthibitisha ulichoandika.. In onboard job hasa za Cargo, tankers, Roro, Chemicals long safari's ,process yake ya recruiting sidhani kama inaweza kuwa rahisi hivyo..otherwise itakuwa ni hizo shunters na kuna mahala umetaja Saudi-Aramko labda ni hizo supply boat za kwenye rigs na meli za uchimbaji.. Hiring process haiwezi kuwa rahisi hivyo tena you are not proffessional unaenda kuwa oiler bado napata shida kuamini..
 
Hata mm nna mashaka na ww
All in all siwez kumwaga mchele hapa ila elewa tu mtu anaweza akawa na seaman book Zaid ya mmoja na hz seaman book zetu wapo watu wanaweza kuzichezea so Kama nikitaka kuondoka naweza nikawanayo Moja ya chaka nikaitia mihuri zen ile og isiwe na muhuri hata mmoja

Nna mashaka na UBAHARIA wako mkuu
 
Meli ni kama kiwanda,nina hakika kuingia melini ni lazima uwe umepitia darasani,hiyo kampuni iliyokuajir nayo ni magumashi bana,kampuni za uhakika haziajiri baharia mwenye CV feki,kwa ajili usalama unapokua kazini,kwaiyo CV zote nilazima zipitie kwenye cestem ya ukaguzi,ili kupata mtu sahih anaejua majukumu yke ya kazi na sheria zote za meli.
Sawa baharia mzoefu
 
Mkuu seaman book ni certified document ambayo iko signed and stamped kama passport, CV ni piece of paper tu ambayo unajiandikia na inaweza ukawa umedanganya tu mpaka followup ifanyike kuthibitisha ulichoandika.. In onboard job hasa za Cargo, tankers, Roro, Chemicals long safari's ,process yake ya recruiting sidhani kama inaweza kuwa rahisi hivyo..otherwise itakuwa ni hizo shunters na kuna mahala umetaja Saudi-Aramko labda ni hizo supply boat za kwenye rigs na meli za uchimbaji.. Hiring process haiwezi kuwa rahisi hivyo tena you are not proffessional unaenda kuwa oiler bado napata shida kuamini..
Nimetolea tu MFANO wa ARAMCO coz hao jamaa huwa wanasumbua Sana wabongo but in my seaman life sijawah fanya nao kaz
 
yaani umetuma tu CV, ukapigiwa simu tena lugha hukuielewa ukawa unaitikia tu yah yah yah, kwenda kwenye email mkataba na tiketi ya ndege hapo hapo tena ukaenda kuwa oiler dah hiyo kampuni kiboko imesajili kweli na IMO..
 
Back
Top Bottom