Nimewaza Ujinga: Kwanini magari yasigome kuwaka mpaka dereva atakapochomeka leseni yake na funguo kwa pamoja?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini kusiwe na mfumo ambao utawezesha, licha ya kwamba engine imewashwa kwa funguo, lakini bado gari itagoma kuwaka mpaka utakapochomeka pia leseni yako ya udereva?

Yaaani kunakuwa na direct contact baina ya servers za TRA, Police Traffic pamoja na ignition system ya gari.

(1) Faida yake ya kwanza ni kwamba, hakuna mtu atakayeweza kuendesha gari kama hana leseni (Leseni inakuwa na smartchip kama ya ATM Card)

(2) Faida ya pili ni kwamba, ata ikitokea kuwa gari imeibwa ni rahisi kujua ni leseni ya dereva yupi inatumika kuendesha gari hiyo. Pia Mamlaka husika wanaweza kulizima hilo gari mara moja.

WATAALAM WA ICT, COMPUTER NETWORKING PAMOJA NA MECHANICAL/AUTOMOBILE ENGINEERING msipite bila kusema chochote please.

I STAND TO BE CORRECTED.....!!!!!

Nimelisajili hili wazo langu la kijinga kijinga...!!!!!

NB: TTCL nitawapa wazo kubwa sana la biashara ambalo halipo katika mitandao mingine ya simu za mikononi/kiganjani.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Sio Ujinga ni Mawazo Mazuri

Cheap kama ATM connected
na system unahitaji Network nzuri

Huku kwetu Africa kuna Vijiji utaenda gari ukizima lisiwake

Pili ikitokea dharura kijana asiye na Leseni ila ni Dereva yupo mwenyewe nyumbani hataweza kumsaidia mgonjwa kufika hospital haraka

Kuhusu Magari kuibiwa siku hizi security systems za magari zanazidi kua za kisasa sana miaka 10 ijayo kuiba gari utahitaji akili nyingi sana usikamatwe
 
inawezekana sanaaa, zipo baadhi ya hotel/nyumba ili kuingia lazima uweke/upachike kadi ndipo mlango ufunguke....ukishaingia unapachika kadi sehemu husika, ndipo taaa zinawakaa


ni nawazaga kwa nini wakati mwingine kupiga chafya na kutoa hewa ya ukaa hutokea kwa pamoja, je waeza zuia kimojawapo?
 
Thanks...
Teknolojia ya mawasiliano Bongo bado ipo chini mno. System kama hii inahitaji umakini na ujuzi ambao Bongo bado ni ndoto za mchana. Pamoa na hayo lakini nadhani utakuwa una-complicate mambo bila kupata faida ya maana.

Kama shida yako ni kuzuia wasio na leseni wasiendeshe gari basi watu wataazima leseni. Kama shida yako ni kuzuia wizi basi kuna teknolojia cheap na realible kuliko hii ya kuchomeka leseni.

Kwa kifupi ni wazo lisilo na impact yoyote bali litasabisha usumbufu usio na maana. Na zaidi watu bado watabuni njia za kufanya gari liwake hata kama hujaweka leseni.
 
miaka 10 ijayo kuiba gari utahitaji akili nyingi sana usikamatwe
Hii pia inaweza kuwa sehemu ya hiyo advancement ya miaka 10 ijayo kwa maana kuna uwezekano network coverage ikawa ipo kubwa sana mpaka huko vijijini.
 
Back
Top Bottom