kambagasa
JF-Expert Member
- Aug 18, 2014
- 2,261
- 1,785
Ndugu zangu jana nilipata taarifa ya msiba wa kijana mwezangu tuliyekua pamoja ujanani na ikafikia hatua kujitambulisha kama watoto kwa pande zote za wazazi. Mimi nina vishughuli vyangu mbali na huko kijijini kwa vile huyu kijana mwezangu alikuwa na familia yake maiti ilifika jana tokea hospital na kuletwa kwake kwa mazishi.
Mke na baadhi ya kina mama walilala sebuleni maiti ikiwa chumbani. Baadae maiti ikasafishwa (kuoshwa asubuhi chini ya usimamizi wa ndugu na baadhi ya wanakijiji). Sasa kituko ni pale inaenda kufungwa sanda na kuona imenyolewa na kunyofolewa nywele na kipande cha nyama kisigoni!! Wanaume walioiosha ni ndugu na wanakijiji (watu aged) wamepigwa na butwaa kukutana hali hiyo asubuhi hii wakati waliiosha ikiwa haina mkato wowote na mimi nikaitwa kwenda kushuhudia masaibu yaliyompata rafiki yangu (marehemu).
Ukweli nimezika na kutokomea bila kuaga wasije kunifuata kwa nyuma. Ilibidi tushauriane kukaa kimya (inasemekana kuna mama mmoja ndiye kahusika maana ni mchawi hadi mbwa wanamtambua na alilala hapo