Leo nimewakomesha matapeli wa mitandao ya simu

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,109
9,407
Wakuu leo nimewachezea akili matapeli wa mitandao ya simu hadi wamejiona mafala, ilikua mida ya saa9 alasiri wakafoadi sms imethibitishwa tsh 198,000 hivyo salio langu likawa 399,000.

Punde wakapiga simu nakujitambulisha ni tigo makao makuu, wakanambia kiasi kilichokuwepo kabla ya kufoad sms yao, pia wakanambia mara ya mwisho kufanya muamala.

Muda huo mimi nawachora tu coz nawajua vizuri, wakanambia nimtumie huyo mteja alokosea nikakubali bt sikutuma, wakapiga tena wakisema wanasubiri muamala la sivyo watafunga line yangu.

Nikawatukana wakanambia unajifanya jeuri tunailock namba yako kuanzia sasa haitatumika kisha wakakata japo hakijatokea chochote kwenye line yangu mpaka sasa.

Sasa nachojiuliza hawa washenzi taariba binafsi za acount zetu wanazipata wapi au niwafanya kazi wa mitandao ya simu ndio wanafanya hii issue ya utapeli?
 
Taarifa zako wanapewa na watumishi wa tigo, tena walivyo wajanja wanatoa no za sehemu moja (wilaya), au mkoa mmoja watapiga elaa tena wanahamia location nyingine
Kwa Namna Wanavyokupa Taarifa Zako Ni Rahisi Sana Kuwaamini Kama Hujui Aina Hii Ya Utapeli
 
Weka namba yao hapa ili uwaokoe na wengine.
mkuu hawa mabwana wanatumia namba tofauti tofauti hivo kilichomuhimu ni kua makini unapoona sms ya pesa, wao hucheza na saikolojia yako watakupa baadh ya taarifa zako ili usiwatilie shaka then wanafanya yao.
 
Mimi huwa baadae tunagonga story, wanasimulia wanavyopiga pesa, Kuna mmoja tu alinitukana baada ya kumgundua.
 
Back
Top Bottom