Utapeli wa mitandao, usumbufu wa "Tuma kwenye namba hii"

Kakijana

JF-Expert Member
Aug 8, 2021
727
3,343
Wakuu poleni na majukumu.

Hoja ninaipeleka kama "mkopo", maana leo ni "freeday" ya karibu kabisa na ATM za sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kuna kale kaujumbe kanaingia paaap! na unakumbuka jana "rafiki mpya" kwaajili ya sikukuu kakutajia namba moja kati ya mbili ulizo na uhakika nazo kuwa ana namba ya ziada, na mliongea kwa kifupi tu furaha za urafiki wenu kwa sikukuu hizi, maswala ya viwanja na nauli, na ili asikwepeshe dhumuni lako la kufurahia sikukuu unaikumbuka "fimbo" ya karibu ni "muamala", na hapohapo vile vimeseji vya tuma kwa namba hiii xxxxxx jina ni (Sikukuu Tamu) nawewe hujapewa namba ya pili na "rafiki" yako na una uhakika anayo.

Unazama menu ya muamala, unatuma na ya kutolea, na jina linakuja kweli Sukukuu Tamu amepokea "nauli"
Unampigia "rafiki" au kwakua mliongea kwa kuaminiana unasubiria simu ya "tuma location" holaaa hata sms, holaaa mda unaenda, ndipo unakumbuka ni kitu kizito kutoka kwa matapeli wa mitandaoni.

Tuwe na akili ya akiba, na kama kuna namba special ya TCRA au mitandao ya simu mtu anaweza kui-report namba ya " Sikukuu Tamu" on-the-sport tuwahabarishe wengine ili kwenye hizi hekaheka za kumtumia mama,bibi,shangazi hela ya sikukuu kijijini tusikutwe na "Sikukuu Tamu" njiani.

Shukran

Screenshot_20221216-085302.jpg
 
Hawa jamaa kama wameshindikana vile! Maana mpaka kesho, bado wanawapigia watu na kujifanya wanatokea kwenye makampuni ya simu, kuna hela imetumwa kimakosa, nk.
 
Back
Top Bottom