Leo nimetafakari sana kifo cha Rais Benjamin Mkapa

Status
Not open for further replies.

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
9,949
2,000
Ni miezi takriban minne sasa tangu Rais Mstaafu BWM atutoke. Bila ubishi, Rais Mkapa alikuwa na ushawishi mkubwa ndani ya siasa za CCM, na ni ukweli usio na shaka kuwa outcome ya siasa za CCM za uchaguzi wa mwaka 2015 ambazo yeye alishiriki kikamilifu ndizo leo hii tunaishi kwa consequences zake. Pamoja na hayo nimetafakari sana juu ya kifo chake na kujaribu kufikiria leo angekuwa hai angekuwa na fikra gani au angeshawishi vipi mwenendo wa serikali hii pamoja na chama chake. Nimetafakari sana pia urais wa huyo mheshishimiwa.

1. Ni mwaka 1995,Mkapa achaguliwa kuwa rais, ala kiapo na kisha kusema wapinzani ni mkono mmojawapo katika mikono yake miwili ya kufanya kazi
Mwaka 1995 baada ya kuapishwa pale uwanja wa uhuru, Mkapa atoa hotuba na kulihutubia Taifa, asema Wapinzani ni watu muhimu kwa maendeleo ya Taifa, Asema mawazo mbadala katika nchi ni kitu chanya kwa Taifa na akasema Wapinzani ni kama mkono mmoja katika mikono yake miwili, na kuwa chama chake ni kama mkono wa pili wote wanahitajika kwa ajili ya usitawi wa nchi.

Miaka 25 baade tumepata rais Mwingine, anayeonekana ana nia ya kuua upinzani, anayewaambia wananchi kuwa pindi wakichagua wasimchanganyie, anawaambia wananchi kuwa wakichagua upinzani katika maeneo yao hatopeleka maendeleo!. Hii ndo Tanzania ya leo, tofauti na miaka 25 iliyopita!. Najiuliza je Mkapa angekuwa hai leo hii akashuhudia aliyoshiriki kuyaasisi mwaka 2015 angekaa kimya ndani ya Chama? - Naamini angemwambia John bila kupepesa macho kuwa John hili unalofanya siyo sahihi badilika!

2. Mkapa atoa kitabu ajuta Mauaji ya Zanzibar
Mwaka mmoja au miwili nyuma kabla ya kifo chake rais Mkapa atoa, kitabu, ajuta kwelikweli ndani ya kitabu hicho mauaji ya watu wasio na hatia huko Zanzibar. Mauaji yale yawa mzigo kwenye mtima wake, yamkosesha raha. Miaka 19 baadae, mauaji yanatokea tena, wananchi wa Zanzibar wauawa, wateswa sababu tu ili Tanganyika iweze kuendelea kuweka mtawala inayemtaka huko Zanzibar. Je Mkapa angekuwepo hai, leo hii angemueleza John kitu gani? - Angemwambia John kuwa uko sahihi well done endelea hivyohivyo? au angemwambia John kuwa usirudie makosa niliyofanya mimi mwaka 2001 waachie Wazanzibari wamchague wanayemtaka?

3. Ni Siku chache kabla ya kifo chake, Wastaafu waitwa dodoma kujadili mtu wa kumpa kijiti cha kuongoza Zanzibar, Mkapa naye ahudhuria
Ni siku chache tu kabla ya kifo chake, Mkapa alikuwa na wenzie, Ali, Jakaya John, Shein na Mama Maria, moja ya kitu walichojadili ni mtu wa kumpa uraisi huko Zanzibar. Kitu kiichoniijia kichwani, hivi Mkapa alikubaliana kweli na wenzie wampe mtoto wa Ali uraisi? - Mkapa huyuhuyu ambaye Sumaye anasema kuwa wakati wakiwa madarakani walikubaliana wasiwape watoto wao vyeo ili kuondoa nepotism ndo eti atakuwa alikubaliana na wenzie kuleta na kulea utamaduni wa Kisultani nchini? - Akili yangu inaniambia kuwa Mkapa lazima alikataa hilo wazo, haiwezekani Mkapa huyu anayejuta kutokana na maafa ya kuwapandikizia Wazanzibar mtawala mwaka 2000 eti akubali tena kurudia dhambi ileile iliyopelekea kuuawa Wazanzibari huko Pemba mwaka 2001. Kwa hiyo akili yangu inaniambia kuwa Mkapa hakuwa onboard kwenye wazo la kumfanya Hussein kuwa Sultan huko Zanzibar.

4. Mkapa afariki, hatukutangaziwa na mkuu wa nchi ugonjwa uliomuua
Mkapa afariki, sheria inasema anapofariki kiongozi mstaafu lazima umma utangaziwe na rais aliyeko madarakani, na katika tangazo hilo mtangazaji inabidi aeleze kilichomuua mgonjwa. Sisi kwetu kweli tulitangaziwa msiba, lakini katika tangazo lile hatukuambiwa mgonjwa kafia nyumbani au kuambiwa jina la hospitali husika kama kafia hospitali. Nimetafakari sana kwa nini taarifa hizo hazikuwa kwenye tangazo? - kwa mujibu wa sheria, Umma si ulikuwa na haki ya kujua hizo info?, kwa nini zilikuwa vague sana?

5. Maombolezo yafanyika, Msiba haukuwa na kiongozi high profile kutoka nje ya nchi
Nimetafakari sana hili suala, nikasema kwa nini viongozi wa nchi jirani hawakuja? Nikasema labda ni Korona, lakini nikafikiria tena, Burundi nao sera yao ya korona si ilikuwa kama sisi na ni marafiki wetu wakubwa kwenye ukanda huu? Kwa nini rais mpya Ndaisheye hakuja? Sijapata jibu.

Kama ni Korona mbona basi raisi Museveni baadae alikuja na convoy yae wamevaa mask kwa ajili ya mradi wa Bomba la Mafuta wakati nchini kwake bado wanapambana na Korona? Kwanini baadae kabla ya uchaguzi Mkuu rais wa Burundi alikuja TZ? Mbona na rais wa Malawi alikuja baadae kipindi cha Kampeni?

6. Maombolezo yaendelea na watu waendelea na shughuli zao utadhani hakuna msiba
Nimetafakari sana hili, wakati mwili wa Marehemu umelala uwanja wa Uhuru hapo Dar, hakuna hata siku moja shule za msingi au sekondari au vyuo zilifungwa ili watoto na walimu wakatoe heshima kwa rais wao wa zamani, Lakini John alipokuwa akienda kwenye kampeni katika jimbo la uchaguzi basi shule zitafungwa, watumishi wa serikali watapewa notice ya lazima wahudhurie mikutano yake, Najiuliza serikali ya John ilishindwaje kuwapa ruhusa maalum watumishi wa serikali kwenda kuuaga mwili wa BWM kama heshima kwake? - Sitegemei jibu liwe eti Jumamosi au Jumapili watu wangeweza kwenda kutoa heshima zao za mwisho, hizo kwa wengine bado ni siku za kwenda kwenye ibada!

7. Ben alitaka tume huru ya uchaguzi
Kabla ya kifo chake, ndani ya kitabu chake, Ben ni kama anaungama, kuna kitu anakisema, kinamuuma roho. Anaona wazi kuwa taratibu za chaguzi nchini haziko fair, hazina haki. Ben anataka tume huru ya uchaguzi ili wananchi wachague viongozi wao haki bin haki - Je Ben angekuwa hai leo hii akajionea hii tume ya John na Mahera wake, Ben angesemaje? - Naamini Ben angemwambia John kuwa Mwanangu sasa hii unachofanya umezidisha hatuendi hivyo!! , hebu achana na uharibifu huu haukusaidii wewe wala nchi!

8. Swali moja ambalo bado nahaingaika nalo, JE BEN ANGEUNGA MKONO MOVE YOYOTE YA KUBADILI VIPINDI VYA UTAWALA KWENYE KATIBA? - Hell no, maana huko nyuma amewahi kusimama kidete kumzuia Salmin Amour kubadili katiba kuendelea kuitawala Zanzibar!

Tangulia Ben, Kifo chako kinaniachia maswali mengi kuliko majibu!!!
 

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,023
2,000
Kitabu cha Mkapa ni maneno halisi ya kuungama kwa watanzania si tu kwake yeye binafsi, bali hata kwa system mbovu ya chama chake kwa ujumla. Alijitahidi kwa kiwango kikubwa katika kitabu hicho kutaja baadhi ya mambo ikiwa pamoja na Mauaji Zanzibar 2001, Tume huru, Katiba n.k. Chama chake hakina hata 1% ya maoni yake.

Katika kitabu hicho yaonekana wazi kuwa pamoja na mengi aliyoyafanya lakini kushindwa kumalizia mchakato wa Tume huru, suala la Zanzibar, Katiba mpya limemuumiza sana.

Na hakuwa na matumaini kuwa kuna Raisi atakayekuja kufanya hayo. Bado alikuwa anaviona vifo vya Wazanzibar mbele yake miaka kadhaa vile vile aliyaona mateso watayopata wapinzani bara na visiwani. Nguvu hakuwanayo tena, na nguvu pekee aliyobaki nayo ni kalamu- kuandika kumbukumbu ya mawazo yake.

Ni suala la muda tu kabla ya vitabu vyake kupigwa marufuku TZ.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
9,949
2,000
Kitabu chake ni Zawadi(kama jina lako) kwa Watanzania.

Wastaafu waliobaki kama Ali na Jakaya wao wanajengewa Mahekalu na Makasri makuuubwa utadhani wana mpango wa kufuga tembo, wameridhika, hawana ujasiri wa kunena au kuandika mambo ya kulitibu Taifa, hawana mpango kabisa na mustakbali wa nchi!.

Watu wana mijuumba kedekede lakini bado hawaoni aibu kwenye nchi masikini kuendelea kujengewa mihekalu na mikasri kama ile, wakati wananchi wana kila aina ya umasikini!. Shame on them!

Mimi natafsiri Mahekalu na Makasri waliyojengewa akina Ali na Jakaya ni kama rushwa tu ya kununua Ukimya wao pindi Madhalimu wakitaka kubadili katiba watawale milele au kuua upinzani nchini!, kitu ambacho naamini Kamwe Ben asingekubali

Ben hakuwa mtakatifu lakini angalau aliandika neno la kuliponya Taifa, neno la Urithi kwa Mtanzania!
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,153
2,000
Kifo cha marehemu mzee mkapa kilinifikilisha sana na hata baada ya rais mstaafu JK kuongea kuwa alipokuwa akiongea na media alistaajabu kifo kile baadaye akitabasamu!

Unaweza kusema ameshafariki tuachane nalo ila behind the curtain kuna siri inayoweza kuumiza watu.

👉Ngoja maisha yaende but the day has come.
 

Graph Theory

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,917
2,000
Nanukuu,

Ninajua mzee Mkapa hakupenda sana vitu viitwe kwa jina lake, Lakini kwa kuwa sasa ameshalala na hawezi kuniadhibu Ninaagiza uwanja huo uitwe.

Mwisho wa kunukuu.

Swali, wakati Mkapa akiwa hai alikuwa na uwezo wa kumwadhibu Rais Magufuli? Kama ndiyo alikuwa anamwadhibu vipi? Iliwezekanaje mtu asiye na amri kwenye vyombo kama Polisi, JW, TISS amwadhibu CIC? Je, mwadhibiwa alichoka kuadhibiwa?
 

Obadia Antony

Senior Member
Aug 31, 2019
121
225
Hivi huwa sielewi watu mnaomuita JPM dikteta Mara anaua upinzan huwa mna sababu zipi,,ukweli ni kwamba upinzan nchin Tanzania unauliwa na wana nchi wenyew ,,wananchi wanaona serikal iliyopo madarakani inafanya kazi nzuri ,,unategemea nin ? Zaid ,,uchaguz wa mwaka 2020 pamoj na changamoto kadhaa ,ukweli utabak kazi ya JPM ya miak 5 ilikuwa lazima CCM ishinde kwa kishindo ,,
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom