Leo bwana nilikwenda supermarket moja hivi, nilipongia nikakuta kuna kifoleni kidogo kwani mbele kulikuwa na mteja ambaye anaongea English, Kiswahili hajui ilikuwa ni wakati wakulipia na muuzaji nae Kiingereza hajui, niliumia sana kwani yule mteja mimi namjua ni dada wa Kimakonde na kaolewa na mzungu, anajua Kiswahili vizuri tu nahisi kushinda Kiingereza chenyewe.
Nilikaa nikasema why anafanya hivi lakini, huyu dada nilishawahi hata kucheza naye pool table ni Mswahili kabisa na ni Mmakonde kwa wazazi wake Mikoroshoni, kasoma Msasani Primary School.