Unaanza kukana maneno yako mwenyewe, hiyo ni hatua ya kwanza. Ila nenda zaidi, mkiri Yesu kwamba ni Bwana na Mwokozi wako, fanya hivyo bila aibu bali kwa furaha, sifa na shangwe. Yesu hana muda maalumu wa kumtaja. Namshukuru nikiwa nalala, na nikiwa naaamka. Namshukuru kabla na hata baada ya kula. Namshukuru hata nikiwa naoga. Namshukuru nikiwa napita mtaani. Yaani nalitaja jina lake wakati wowote, ni shetani tu na mawakala wake ndiyo hawapendi kulisikia jina lake.
Hamna aliyeongelea dhambi kwenye uzi huu mzima na hamna aliyehukumiwa, ukiacha baadhi ya walionihukumu mimi. Nimeanzisha uzi kuthibitisha uwepo wa mapepo lakini zaidi uwezo wa nguvu za Mungu kutenda kwa jinsi anavyoona yeye inafaa. Nina ushuhuda mwingi wa rehema, huruma na baraka za Mungu katika maisha yangu mwenyewe naweza kuandika vitabu.