Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,654
- 6,612
Wakuu pepo na roho chafu zipo asikudanganye mtu na Jina la Yesu lina nguvu ya ajabu.
Hapa home kuna dada wa kazi, kwa muda mrefu amekuwa na tatizo la wanaume. Ok, kila mtu ana hisia hilo linaeleweka lakini ambacho kimekuwa kinaniumiza kichwa ni usalama wa nyumba na hata waliomo ndani (ukiachilia mbali usalama wake mwenyewe kwa sababu yuko very reckless).
Kuna wakati alikuwa na mtindo hadi wa kufungua milango saa 8 za usiku na kuruka ukuta kwenda kufanya mambo yake ya ajabu. Ana matatizo mengine ya uchafu wa kutisha, hapa naongelea kusukumia vyombo vichafu chini ya makabati, hili kwa kiasi kikubwa tumelikabili ingawa na lenyewe linahitaji usimamizi wa mara kwa mara. Hata yeye personal hygiene siyo nzuri kwa kweli.
Niliwahi kumpeleka kanisani lakini kwa bahati mbaya sijaweza kumsaidia zaidi ingawa kwa niliyoyaona na kushuhudia ana mapepo huyu dada, na ni mapepo wenye nguvu hatari. Juzi nilikuwa naangalia TB Joshua, mapepo walikuwa wanaconfess jinsi wanavyoshikilia watu.
Niliwahi kumwambia jamaa yangu mmoja kuhusu huyu dada, ana potential kubwa sana kwa sababu as a person hana matatizo yoyote yaani anaongea vizuri na watu yaani kiukweli anaweza kuwa superstar, ana ucheshi ingawa mimi sijataka kumzoea kabisa.
Watoto watoto wa ndugu wakija home anasahau shughuli zake, yeye ni kucheza na watoto tu. Binafsi nadhani kuna kitu kinashikilia destiny yake.
Sasa twende kwenye story ya leo. Leo nilikuwa na mishe zangu ila roho ikaniambia nitulie nyumbani nifanye mambo mawili matatu. Jana alikuja fundi wa maji kufanya marekebisho fulani lakini leo akamleta mfanyakazi wake yeye akaondoka zake. Mara paap, mida ya mchana ikatokea tu nikachungulia dirishani, nikamuona fundi anaendelea na shughuli zake nje huku dada anajipitisha pitisha.
Hapo hapo nikagundua anamnong'oneza yule fundi vimaneno, yaani yupo hatua kama nne kutoka nilipo ila simsikii anachosema. Nikimuangalia fundi haonekani kujali na anachoambiwa, nadhani roho yake ilikuwa inakataa. Dada anaendelea kupush, mara anammwagia vimaji, kumbuka huyu fundi amekuja leo kwa mara ya kwanza na alikuwa hana hata masaa 3. Mara dada anamtupia yule fundi ndala, nikajua leo ni leo. Ila nikimcheki fundi anaonekana roho inakataa kabisaaa.
Mara namuona fundi taratibu anaacha kazi akaanza kujimwagia maji kwenye miguu, lakini kwa shingo upande. Nilijua leo ni mapambano. Nakumbuka mara moja nikaanza kukemea palepale nikisema kataa kwa Jina la Yesu!! Kichwani nilidhani jamaa ndiyo angekataa ushawishi ule.
Mara hao, wakaenda nyuma ya nyumba. Nikasubiri kama dakika mbili nikatoka nikazunguka nitokee upande wa pili. Sasa namuona jamaa ndiyo anaonekana analazimisha kama vile anataka kumbaka na dada anakataa, nikajua shetani anashindwa mbele ya macho yangu! Nikasubiri kama dakika 3 hivi situation ikazidi kuharibika.
Simu niliacha ndani lakini hata ningekuwa nayo mimi siyo mmoja wa watu wale anaona kitu badala ya kuingilia kusaidia unakimbilia kurekodi. Nikamuita oyaa! Kama mara mbili, aliposikia akageuka huyo mbio, dada amebaki tu pale.
Nikamwambia amuite jamaa hakuja. Nikamfuata namuuliza vipi nini kilikuwa kinaendelea, wote wawili wanatoa story zisizoeleweka. Dada anadai oooh aliniomba simu nilipoenda nyuma akanifuata.
Nikamwambia aache kazi. Nikamuita bosi wake akaja, baada ya wote wawili kujieleza akaamua amuondoe. Jamaa aliniambia yaani nimekuwa mstaarabu, ilitakiwa nichukue baroka nianze kumcharaza, ila binafsi nilivyoshuhudia mchezo mzima ni issue nzito zaidi. Yes, jamaa alikosa nidhamu ya kazi ila na hawa mapepo nao tusemeje?
Miezi kama 6 iliyopita aliwahi kuwa na issue kama hizi na mlinzi. Kuna siku nikamkuta ana simu ya mlinzi jikoni inacheza video za ngono. Kumuuliza mlinzi vipi haya mambo, yeye akadai alimpa amchajie atakuwa amewasha yeye mwenyewe.
Nikamuuliza na issue za dada nilizoziona kuwa naye sehemu za gizagiza, akadai mambo mengine ni yeye dada ndiyo anampressure. Sijafuatilia sana hivi karibuni kama hayo yaliisha. Nakumbuka kuna ndugu yangu alikuwa anaishi hapa na yeye aliwahi kuniambia hivyo hivyo, ni yeye dada anayeapproach wanaume.
Mtaani ni kero, si bodaboda, si dereva wa babaji, yeyote anayekatiza mbele yake ni wa kwake. Kuna siku aliwahi kutoweka mchana kwa masaa kadhaa, aliporudi story yake ni alikutana na dereva wa bajaji akataka kumpa lift. Baadae dereva akabadilisha njia, huko mbele anadai akataka kumbaka.
Naamini Mungu amenionyesha hili kitu leo kwa sababu maalumu. Kwanza naamini kemea yangu imefanya kazi, hamna kingine. Tumeshataka kumrudisha kwao mara nyingi tu lakini binafsi nimekuwa najiuliza, hivi siyo kama nakuwa nampa ushindi shetani na hila zake?
ILA AISEE HILI PEPO SITAKI KULILEA!! Naomba ushauri wa haraka, nini nifanye? Hawa pepo wana nia gani hasa? Kuleta tafrani zisizoisha hapa nyumbani au wana nia zingine?