Leo nimeshuhudia pepo linamuingia mtu

Leo nimeshuhudia pepo linamuingia mtu

Umeandika mengi sana aisee,
Ila nilichoshangaa kwenye title unaandika Pepo limeingia leo wakati Huyo dada Uasherati kaanza kitambo tu. Sasa sijaelewa hao waliokua wakimpitia hapo awali halikua Pepo??


Kwa mtizamo wangu pepo lilimuingia yule fundi, ndiyo maana ya title.
 
Ungeseme hivyo toka mwanzo tusingekuwa na mazungumzo.
Wewe ungezungumzia tu huo uchafu wa huyo mtu bila kumshirikisha Yesu. Tukio siyo kubwa kiasi hicbo mpaka Yesu aingilie kati. Wakati bakora mbili au tatu tu zingetatua tatizo hilo. Acha kuchezea jina la Nabii Issa kwa mambo ya ovyo ovyo.
 
Unawivu wewe unaonekana umekataliwa unakuja kumtangaza humu kama anamapepo siunamtimua tu mbona ma beki 3 wapo kibao tu
 
kaa nae zaidi ukimshauri mpeleke kwenye maombezi zaidi huku ukimwombea zaidi

Kuna mtu alinishauri nimuwekee mikono ila yasije kunitokea ya wale walikimbizwa na mapepo. Namuamini Mungu sana tu lakini mambo mengine yanahitaji kuwa na karama zake otherwise ni hatari tupu.

Jana nilikuwa naangalia video ya TB Joshua, kuna mchugaji Kenya alikuwa mahiri wa kukemea mapepo na alikuwa anatumia hata physical means. Siku moja yakamshambulia, jamaa alikuwa hata hawezi kutembea alikuwa anatambaa. TB Joshua akamwambia kila mtu ana karama zake, haya ya kuconfront mapepo one on one ni mambo hatari sana. Nitaendelea kumuweka katika maombi, definitely.
 
Unawivu wewe unaonekana umekataliwa unakuja kumtangaza humu kama anamapepo siunamtimua tu mbona ma beki 3 wapo kibao tu


Hata mtu mwenye mapepo siyo wa kumchukia, wale viumbe ni washenzi wanaweza ingia kwa watu innocent kabisa. Hilo ndiyo watu wasioelewa wanakosea. Kwa nini nimtangaze ana mapepo ili aonekane mbaya, kwa faida ya nani? Kwanza hata picha sijaweka, jina sijataja, kwa hiyo atadhurika vipi na nilichoandika? Wivu ni kitu cha mwisho unaweza kusema kuhusu uhusiano wangu na huyu dada, amini usiamini.
 
Sasa hilo pepo uliloliona lilikuwa limevaa pensi nyanya au gagulo??

Vipi sura yake iko kama ya Sizonje au Chakubanga?

Ungelipiga picha ingependeza zaidi...


Ningelipiga picha na kupost hapa ningepoteza wiki kadhaa, kuanzia kureport tukio polisi, vyombo vya habari, nk. Inawezekana hili pepo linataka kupoteza muda wangu. Kwanza inabidi nilikemee zaidi nirudi kufanya shughuli zangu, yaani nilikuwa katikati ya jambo muhimu sana.
 
1. Ni kweli mapepo yapo, ila hayamuingii mtu kadiri ya simulizi hii.
2. Mara zote watu wanaposhindwa kutafsiri vyema matatizo ya kisailolojia, wanaishia kusema ni pepo.
 
Wote mtakuwa na mapepo. Yeye la kutongoza na kujigijigi na ww la kumtamani[emoji23][emoji23][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Wewe ungezungumzia tu huo uchafu wa huyo mtu bila kumshirikisha Yesu. Tukio siyo kubwa kiasi hicbo mpaka Yesu aingilie kati. Wakati bakora mbili au tatu tu zingetatua tatizo hilo. Acha kuchezea jina la Nabii Issa kwa mambo ya ovyo ovyo.

Yesu ana nafasi katika kila ninalolifanya katika maisha yangu, kwenye hilo sioni aibu wala kujiuliza. Bakora hizo amepigwa sana na ndugu zake wa kike lakini hazijasaidia. Mimi anajua sana ukali wangu ila sijawahi kumgusa. Maandiko yanasema vita yetu siyo ya mwili na damu. Leo nimekemea na pepo ameshindwa, na anayeamini na aamini.
 
Wote mtakuwa na mapepo. Yeye la kutongoza na kujigijigi na ww la kumtamani[emoji23][emoji23][emoji125][emoji125][emoji125]


Kuna mnaotaka kulazimisha hii kitu lakini haipo, nasema kwa mara nyingine.
 
Inasikitisha sana...

Mwacheni afanye akipendacho ni ngumu kumzuia... Akichoka ataacha...


Cc: mahondaw

Asifanye nyumbani. Akafanye hayo mambo nje huko. Inamaanisha leo nisingekuwepo inawezekana wangefanya mambo yao sebuleni au jikoni. Na vipi kuhusu usalama wa mali zetu na hata usalama wetu wengine? Hii hali ya kutojali ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom