Leo nimepokea PIN ya Google Adsense kwa ajili ya adress verification

Leo nimepokea PIN ya Google Adsense kwa ajili ya adress verification

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
21,772
Reaction score
35,770
Miezi kadhaa iliyopita nilikidhi vigezo vya 4000hrs na 1000subs baada ya kujaribu mara kadhaa ku request PIN kwa ajili ya adress verification leo naona imefika posta.

NB:

1. Adress nimetumia ya P.O. Box kawaida (kufungua posta ni kama 45000 hivi).

2. Nilituma mara ya kwanza haikufika mara ya pili imefika. Hapa nilikosea maana nilitumia address ambayo siyo.

3. Nili request PIN kwa mara ya pili tarehe 15 April..imechukua kama 3weeks barua kufika...

Tuendelee kupambana.

20220512_112756.jpg
 
Mkuu ingekuwa vyema ungetupa elimu hata kwa ufupi ili wngine tusiofahamu tupate kuelimika pia. Asante
Hii ni hatua ya muhimu katika kuidhinishwa kupokea malipo kutoka google kupitia content nnazo tengeneza online. Nikijaza hizi PIN maana yake nakua verified kupokea malipo kutoka google.
 
Hii ni hatua ya muhimu katika kuidhinishwa kupokea malipo kutoka google kupitia content nnazo tengeneza online. Nikijaza hizi PIN maana yake nakua verified kupokea malipo kutoka google.
Samahani mkuu,
1.Malipo yanakuwa kwa mwezi,wiki au?.
2.Na je,kadiri views zinavyoongezeka na malipo yanaongezeka?.
 
Samahani mkuu,
1.Malipo yanakuwa kwa mwezi,wiki au?.
2.Na je,kadiri views zinavyoongezeka na malipo yanaongezeka?.
1. Malipo ni kila mwezi na unalipwa kama tu umefikisha dola 100 (or its equivalence kulingana na currency uliyo chagua) ndani ya huo mwezi.

2. Yes views zinavyo kua nyingi ndio malipo yanakua makubwa. Pia malipo hayatokani na views tu bali yanatokana na hao viewers wanatoka wapi. Mfano ukipata views wengi kutoka 3rd word countries maana yake malipo yako yatakua madogo ila ukipata views wa kutoka developed countries maana yake malipo yako yatakua makubwa.

Baada ya kulipwa ela yako itatumwa kwenye payment method uliyo ichagua.

Karibu.
 
Samahani mkuu,
1.Malipo yanakuwa kwa mwezi,wiki au?.
2.Na je,kadiri views zinavyoongezeka na malipo yanaongezeka?.
Kama kweli unaona unahitaji kuyajua haya mambo kwa upana wake, nakushauri uingie mtandaoni na kuyatafuta. Kw hapa Jf utapewa hints chache mno, hata mtoa mada hataweza kukuelezea kila kitu ukaelewa na kuhoji tena.


😎
 
1. Malipo ni kila mwezi na unalipwa kama tu umefikisha dola 100 (or its equivalence kulingana na currency uliyo chagua) ndani ya huo mwezi.

2. Yes views zinavyo kua nyingi ndio malipo yanakua makubwa. Pia malipo hayatokani na views tu bali yanatokana na hao viewers wanatoka wapi. Mfano ukipata views wengi kutoka 3rd word countries maana yake malipo yako yatakua madogo ila ukipata views wa kutoka developed countries maana yake malipo yako yatakua makubwa.

Baada ya kulipwa ela yako itatumwa kwenye payment method uliyo ichagua.

Karibu.
Asante sana. Je, malipo yanakokotolewa kwa kila video na kisha unalipwa jumla ya pesa yote au?
 
Asante sana. Je, malipo yanakokotolewa kwa kila video na kisha unalipwa jumla ya pesa yote au?
Kama jumla una video 100 maana yake ni jumla ya fedha zilizo kusanywa kutoka kwenye video zote na sio video moja moja.

I.e. utalipwa ukifikisha 100usd kutoka kwenye video zako zote.
 
Kuna mtu anaweka effort kubwa lakini anapata sh 400 kwa siku or may be inategemea na content
Ni kweli inategemea na content. Na sio content tu bali na lugha. Content zinazo husu finance na tech na unatumia english na viwers wako wanatoka developed coubtries basi lazima ziwe na cpm kubwa (huu ni mfano).
 
Back
Top Bottom