Leo nimekumbuka zamani

Nahman

JF-Expert Member
Oct 4, 2023
522
1,521
Leo nahmn nmeikumbuka zamani,

Nimeyakumbuka maisha ya zamani,

Japo naonekana mshamba mbele ya kadamnasi ila nmeitamani zamani.

Nimetamani kuyaishi maisha yale

Zamani akina mama walivaa nguo ya ndani-suruali-gagulo-kisha sketi au gauni

Zamani wanawake walisimama kisha kupiga magoti wakiongea na wanaume!

Zamani bikira zilikua ni lazima kwa mwanamke (leo ukiongelea bikira unaonekana unawaonea)

Zamani vijana walisikiliza sana wazee wao pindi waongeapo!

Zamani kutembeleana lilikua ni swala la muhimu kwa wote

Zamani mboga majani na nyama zilikua tamu kuzidi kawaida

Zamani akina dada walisafisha nyumba na kulima vinyungu kuliko kawaida!

Zamani tulivuna mahindi kisha kuyaweka kwenye kihenge..,hatukuhitaji madawa kuyafanya yaishi

Zamani grocery na vilabuni waliuza akina mama

Zamani bar walikuepo wazee na wababa watu wazima

Zamani sigara zilitumiwa na wazee

Zamani bangi ilivutwa kwa kificho

Zamani ukahaba ulifanywa kwa siri sana

Zamani tuliandikiana barua na kuviziana chini ya mto au kando ya kisima cha maji.

Zamani ukipanda gari hutamani kushuka hata

Zamani taraka zilitolewa kwa aibu
Zamani wanaume walieapenda wake zao
Na wanawake walitii!

Zamani

Zamani zamani……….

Leta yako moja ulioikumbuka toka zamani..
 
SITAKI ZAMANI.
1. Hakukuwa na usafiri wa kutosha. Sehemu ya kwenda fasta kwa daladala au bodaboda inakubidi utembee kwa mguu.
2. Ukeketaji wanawake ulikuwa umekithiri kila kabila
3. Uvutaji sigara ulikuwa unafanyika hadi kwenye mabasi ya abiria.
4. Huduma nyingi za kijamii zilikuwa duni sana. Watoto wengi walishindwa kuendelea kidato cha kwanza kwa sababu ya uhaba wa shule. Hata mahospitali na vituo vya afya vilikuwa vichache.
5. Viongozi wa serikali na chama walikuwa kama miungu watu. Nakumbuka tulimsubiri katibu mkuu Horace Kolimba toka asubuhi akaja kupita mchana huku akiwa na haraka.
6. Kodi ya kichwa ilikuwa kero.
 
Back
Top Bottom