Ukoloni mambo leo unatuchelewesha Afrika

Elius W Ndabila

Senior Member
Jul 17, 2019
182
500
Na Elius Ndabila

0768239284

Tujikumbushe, niliandika September 2019

Ukoloni mambo leo ni neon lenye dhana pana na huenda likawa si geni kwenye vichwa vyetu, lakini ni vema tukawa na ufahamu wa pamoja juu ya nini maana ya ukoloni mambo leo kabla ya madhumuni ya hoja yenyewe. Pamoja na kufahamu kuwa ukoloni mambo leo ni zao la ukoloni, lakini tunayonafasi ya kuzielezea dhana hii kwa mawanda furani.

Ukoloni ni mfumo wa taifa moja kuvuka mipaka yake na kutawala maeneo ya mbali yanayokaliwa na watu wengine kwa nyanja za kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.

Maeneo haya yanaweza kuitwa koloni au eneo lindwa. Kwa mfano historia inatukumbusha kuwa bara letu kabla ya mkutano wa Berln mwaka 1984/1985 nchi nyingi za afrika zilikuwa chini ya ukoloni ijapo haukuwa rasimi. Mkutano wa Bernl ulikaliwa ilikuondoa tofauti zilizokuwepo baina ya mabeberu waliokuwa waking’ang’aniana makoloni.

Tarehe 26 Februari mwaka 1885 ilikuwa siku ya mwisho ya mkutano wa Berlin ambao ulileta mabadiliko ya kudumu barani Afrika. Wawakilishi wa nchi 13 za Ulaya na wengine kutoka Marekani walikutana kwenye ofisi ya Kansela wa Ujerumani Berlin kugawa maeneo ya bara la Afrika.

Katika chumba cha mkutano palikuwa na ramani ya Afrika yenye urefu wa mita tano. Ilionyesha milima, maziwa na mito mbali mbali iliko. Ni mkutano uliokuwa umeitishwa na Kansela Otto von Bismarck na lengo lilikuwa kuwapa wakoloni maeneo ya kutawala. Hata hivyo hakuna hata mwakilishi mmoja wa Afrka aliyealikwa kwenye mkutano huo

Ukoloni Mamboleo ni neno linalotumiwa na wakosoaji wa ukoloni kuelekezwa kwa nchi tajiri kuendelea kuingilia masuala ya nchi zinazoendelea baada ya ukoloni wenyewe kwisha kwa ukiukaji wa azimio la Umoja wa Mataifa. Neno Ukoloni Mamboleo lilianza kutumika, hasa kuhusu Afrika, baada ya mchakato wa kupata uhuru.

Kisha kupata uhuru, baadhi ya viongozi wa kitaifa na makundi ya upinzani walisema kuwa nchi zao hazitakubali aina mpya ya ukoloni kutoka mataifa yaliyoendelea. Kwame Nkrumah, ambaye mwaka 1957 akawa kiongozi wa Ghana, aliwahi kufafanua Ukoloni Mamboleo katika moja ya vitabu vyake, "Ukoloni Mamboleo, Hatua ya Mwisho wa Ubeberu" (1965), ambacho ni kama ugani wa kile cha Lenin "Ubeberu, Hatua ya Mwisho wa Ubepari" (1916), ambamo Lenin anasema kuwa ubeberu wa karne ya 19 unategemeana na mahitaji ya mfumo wa kibepari.

Ni dhahiri kuwa pamoja na madhara makubwa ambayo bara la afrika lilifikwa kwayo na kuuchukia sana ukoloni uliopelekea vijana wa zamani zile kupambana kupata uhuru wao kwa njia ya amani na bunduki lakini bado tunateswa na ukoloni mambo leo.

Ukoloni mambo leo ni mbaya kuliko ukoloni ule wa kabla na baada ya Mkutano wa Berln. Historia inatukumbusha kuwa mapambano makali yakiongozwa na akina Mkwawa huko Iringa, Kinjekitile huko kusini na akina Isike walifanya kazi kubwa ambazo zilikuja kuwapa pia ujasiri akina Hayati baba wa Taifa kuanzisha harakati upya miaka hiyo.

Dhana ya ukoloni mamboleo imetolewa fafanuzi mbalimbali na waandishi tofauti tofauti. Kwa mfano,ukoloni mamboleo unaelezwa na “The Online Thesauraskama sera ya nchi yenye nguvu ya kuendeleza utawala na udhibiti wanchi nyingine huru au eneo fulani la kijiografia bila kufanya nchi au eneo hilo koloni kirasmi.

Jambo la kimsingi linalojitokeza katika fasili hiini kuwa ukoloni mamboleo huhusisha utawala na udhibiti wanchi zilizokuwa chiniya mkoloni.Pia ni wazi kuwa ukoloni mamboleo uhusisha ukandamizwaji wa watu na nchizisizo na nguvu za kiuchumi.Ukoloni mamboleo unachukua sura mbalimbali kama vile unyamazishwaji wa lugha asili naunyakuzi wa maliasili ya nchichanga. Suala la nchi chache zenye nguvu zaidi za kiuchumi na kisiasa kuzitawala nchi zisizo na nguvu hizolimekuwepo tangu enzi za kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni.

Ni vigumu kuelewa hasa mizizi na mikito ya ukoloni mambo leo katika dunia ya leo. Mara kadhaa hayati Mwalimu Julius K Nyerere alipambana nayo lakini bado hakuweza kuing’oa. Mh Magufuli ameendeleza vita hii lakini bado kutokana na mizizi ya hawa mabwana ilivyojikita ni ngumu kuiteketeza. Kule kwetu Ileje tunaweza kusema mizizi yao ni kama mizizi ya NALUNYAMI.

Nalunyami ni mti ambao mizizi yake hutambaa umbali mrefu na vitoto vya nalunyami huota kwenye mizizi na hata mbegu za kwenye matawi. Ni ngumu sana kuteketeza msitu wa Nalunyami kwani hata ukiukata mizizi yake itachipua huko ilikoelekea. Ndivyo hata ukoloni mambo leo ulivyo kwani mizizi yao ni mingi na imeenda mbali. Ili kuitokomeza inahitaji kung’olewa na kuchomwa moto. Vinginevyo unaweza kuiteketeza kwa kuikata nab ado ndo ukaipalilia.

Tafsiri ya ukoloni huu upo katika Nyanja nyingi, matharani utoaji wa mikopo na misaada pamoja na biashara ya kimataifa.Mkakati mwingine unahusu matumizi ya sera kandamiziza mashirika ya kimataifa kama vile Benki yaDunia na Shirika la Fedha Duniani Mbinu nyingine zinazoashiria ukoloni mamboleo katika nikama vile mfumo wa kugawana gharama katika sekta za elimu na afya, mipango ya kupunguza idadi ya wafanyikazi na mipango ya maendeleo ya millenia (MDGs).

Ukoloni mamboleo ni tatizo linalo lemaza maendeleo katika nchi nyingi hasa zile zisizo na nguvu za kiuchumi.Hii ni kwa sababu nchi zilizoendelea hupania kuzitawala nchi changa kwa njia zilizofichika ili kutimiza maslahi yao. Matokeo ya kutawaliwa huku ni kuibuka kwa athari hasi za ukoloni mamboleo hasa unyonywaji wa kiuchumi.

Uhusiano unaojengeka baina ya mataifa haya unakuwa wa kinyemela na uliojaa unafiki.Mwishowe, mataifa haya machanga yanakosa kujitambua na kujinasua kutoka kwa athari hasi za ukoloni mamboleo.Ni wazi kwamba hili ni suala nyeti kwa wananchi wa mataifa machanga kote duniani kwa sababu linaathiri si tu maendeleo bali pia hali za maisha ya wanajamii wa nchi hizo.Hata hivyo,tatizo hili halij atafitiwa kwa kina kinachostahiki.

Ni wazi pia Mh Rais anatamani huku kwenye ukoloni totoke, lakini kazi kubwa aliyonayo ni kuondoa hii mizizi mawe. Hawa watu wanaakili nyingi kwani mizizi yao walishapandiiza hata kwenye mioyo ya Raia ndiyo maana sasa ni jambo la kawaida kwa waafrika kuamini shida zao zitamalizwa na wazungu. Taasisi na sasasi nyingi za kiserikali na kiraia zinategemea sana wazungu ndiyo maana wakati mwingine akisimama mhubiri mwafrika na mzungu, basi watu watamwamii mzungu.

Tunapaswa kama Afrika sasa kuamua kuwa moto na si vuguvugu. Kazi ya kwanza ya kuwaondoa mabwana hawa ilifanywa na wazee wetu, kazi hii ya pili ya kuondoa ukoloni mambo leo ni yetu. Ninaamini wakitokea viongozi wakubwa Afrika 20 tu kama Mh Magufuli afrika miaka 20 mbele tutajitegemea na tutatoa misaada kwa hawa wanyonyaji. Hii ni kwa kuwa misaada tunayopata inatokana na mali ghafi za Afrika ambazo tumeshindwa kuzichakata kwetu.

Rodney (1973) anasema kuwa njia moja kuu iliyotumiwa na mataifa ya Magharibi katika kujenga Ulaya ni aina mbili za biashara. Biashara ya utumwa ya kabla ya ukoloni na biashara ya kisasa ya kimataifa ambayo sheria zake zinatungwa bila kulihusisha bara la Afrika. Rodney anasema kuwa Ulaya ndilo bara lililohodhi vyombo vya kusafiria majini na usafiri huu ulisaidia ukuaji wa haraka wa Ulaya kwani meli zao zilihakikisha utoshelevu wa malighafi ya viwanda.

Anasema kuwa biashara hii inaendeleza unyanyasaji kwa nchi changa. Kando na biashara kama njia ya kuendeleza ukoloni-mamboleo, Rodney pia anachukulia kuwa makampuni ya kimataifa yameendeleza ukoloni mamboleo katika bara la Afrika na kwingineko. Kwa mfano, analaumu taasisi kama vile benki za Ulaya,Mashirika yanayomiliki meli, makampuni kama vile yale ya uchimbaji madini na mengineyo. Anazishutumu kampuni za kimataifa (Sunlight,Unilever, Lifebuoy, Lux na Vim) kwa kutegemea maliasili ya Afrika Magharibi ili kujiendeleza huku yakiwadhulumu wakulima.


Kuondoa ukoloni mambo leo kunahitaii uzalendo wa hali ya juu na umoja. Kunahitaji akili kubwa, kunahitaji maarifa mengi, kunahitaji ujasiri, kunahitaji uhodari na zaidi kunahitajika ushujaa wa hali ya juu. Muungeni mh Rais kwa kuchapa kazi kwa bidii ambako ndiko matokeo ya kujitegemea yanapatikana.
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,968
2,000
Elius W Ndabila,
We nawe ni mwathirika wa siasa za ujamaa zilizofail duniani kote kwa ugonjwa uleule wa Watawala wa kiafrica kushindwa kuwaletea waafrika maendeleo wakaja na msemo wa ukoloni mambo Leo ili kuzifukarisha fikra za waafrika waaendelee kuamini umasikini wao chanzo ni external factor na sio internal factors kama mfumo mbovu wa hovyo usio na tija kwa wafrika zaidi ya kujali maslai ya viongozi,ukosefu wa utawala bora,ubinafsi,uvivu,ufisadi,wizi,kutowajibika ndio chanzo cha umasikini wa Africa na sio external factor kama sijui ukoloni mambo Leo

Mara sijui mashirika ya kimataifa utadhani nchi tulizokuwa nazo sawa baada ya Uhuru huo ukoloni mambo Leo na hayo mashirika ayapo.Brazil,falme za kiarabu,south Korea, India, Singapore, Indonesia,Malaysia,na tiger country zote hivi nao wangekaa wanalaumu sijui ukoloni mambo Leo Mara sijui mabeberu mara sijui mashirika ya kimataifa wangefikia walipo.Mchawi wa maendeleo yetu ni sisi wenyewe kusingizia wengine ni sawa na kisa cha mbaazi.Hata ukisoma history maisha ya waafrika yamekuwa ya hovyo yaanni umasikini, Vita, njaa, nk baada ya Uhuru na sio kabla Uhuru.

Jaribu kuwa na global vision na sio kujifungia kwenye box la fikra za kijima za enzi za mwalimu. Watawala wa kiafrica wanakopa wanapokea misaada halafu wanaiweka kwenye miradi ya kisiasa white elephant project isiyo na tija kwa waafrika bali sifa kwa Watawala ikiwemo kuuwa demokrasia eti unakuta mtawala anapambana kuuwa upinzani wakati wenzetu wako bize kupambana kuuwa umasikini halafu tunashindwa tunabaki kulaumu sijui WB,IFM nk utadhani ndo wametushauri tutupe pesa kwenye White elephant project. Adui wa mwafrika ni mwafrika mwenzake.Tulipigania Uhuru ili tutawaliwe na waafrika wenzetu.Africa ina watawala haina Viongozi.
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,968
2,000
Eti unatuchelewesha utadhani ukoloni mambo Leo umetuzuia kuzalisha chakula tukauza nje ya nchi,au kutumia raslimali zetu kujikwamua,au kuwapa elimu ya ujuzi watu wetu wawezezalisha tuuze nje.Vyote hivo ni kusingizia mbaazi.
Waafrika tuache sababu za kuwalaumu watu sijui wakoloni mabeberu tujilaumu wenyewe kwa kushindwa kuwatumia mabeberu kuicheza ngoma tunayoita ukoloni mambo Leo tujinasue na umasikini wetu.Hakuna jamii yeyeto iliyoshirikiana positive na mabeberu ikawa fukara chek falme za kiarabu, Korea kusini,Brazil, India, tiger countries. Huwezi ukataka kuendelea kwa kuwa kisiwa ili uendelee ni lazima uliwe.Kila nchi duniani kuanzia USA China zimeliwa ndo maana zikawa na maendeleo. Maendeleo ni sawa na mchezo wa bao au draft huwezi shinda au kufunga bila kuliwa
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,968
2,000
Walter Rodney,Prof Lumumba hawa wana mawazo ya kijamaa ( mawazo ya akili kufungwa kwenye box ) falsafa zao ni outdated kwa kizazi cha sasa cha dotcom chenye awareness kubwa yaani global vision sababu ya maendeleo ya technology ya mawasiliano,tofauti na zamani pale ilipokuwa ni ngumu sana kupata maarifa huru kwa maana maarifa yote yalifungwa na watawala waliofaidika na mfumo mbovu wa ujamaa uliokumbatiwa na watawala wa kiafrica ili kuwapumbaza waafrika wasione mwanga ili watawaliwe kirahisi.
 

dindilichuma

JF-Expert Member
Dec 19, 2015
1,261
2,000
Eti unatuchelewesha utadhani ukoloni mambo Leo umetuzuia kuzalisha chakula tukauza nje ya nchi,au kutumia raslimali zetu kujikwamua,au kuwapa elimu ya ujuzi watu wetu wawezezalisha tuuze nje.Vyote hivo ni kusingizia mbaazi.
Waafrika tuache sababu za kuwalaumu watu sijui wakoloni mabeberu tujilaumu wenyewe kwa kushindwa kuwatumia mabeberu kuicheza ngoma tunayoita ukoloni mambo Leo tujinasue na umasikini wetu.Hakuna jamii yeyeto iliyoshirikiana positive na mabeberu ikawa fukara chek falme za kiarabu, Korea kusini,Brazil, India, tiger countries. Huwezi ukataka kuendelea kwa kuwa kisiwa ili uendelee ni lazima uliwe.Kila nchi duniani kuanzia USA China zimeliwa ndo maana zikawa na maendeleo. Maendeleo ni sawa na mchezo wa bao au draft huwezi shinda au kufunga bila kuliwa
Unaelewa ukoloni mambo Leo kwa ufasaha?
Au unahisi ukoloni mambo Leo unakuruhusu ufanye chochote unachotaka na uzalishe chochote unachotaka?
Kweli elimu tuliyopata ni ya kufanya siasa tu za kitoto za CCM na CDM

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom