Leo nimegoma kumpisha kwenye siti binti mjamzito

Labda anawahi kujifungua.Ila kwenye dalaldala wanawake na wasichana huwa hawawapishi viti wanawake wenzao hata awe mja nzito tumbo kubwa au ana mtoto mchanga hawapishi.Siku Moja basi la kutoka mbagala kwenda kariakoo mwanaume mmoja naona kama alitoka mikoani alimpisha kiti mja mzito baada ya kuona wanawake kwenye basi hawampishi.Akasimama mwanaume yule ameshika Bomba la Basi akiwa amebanwa hatari kwa mlundikano wa abiria kwa hasira akauliza nyie wanawake humu mbona mumegoma kumpisha mwanamke mwenzenu mja mzito roho mbaya nyie.Mwanamke mmoja akajibu kwa sauti kubwa nyie wanaume mnaotia mimba wanawake ndio mpishe mimba zenu zikae kwenye viti.Basi Zima wakaangua kicheko.Mzee wa watu akabaki kushangaa hii mibwege kwenye basi inachekelea nini Sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂
 
Ni kabinti kadogo tu lakini ndio kametundikwa mimba

Nikiwa kwenye siti ndani ya daladala, kakaanza kuniangalia kwa huruma Mara kakaropoka, kaka naomba unipishe nikae mimi mjamzito

Nikakaambia mtafute mwanamke mwenzako akupishe, kwani nyinyi wote mnajua kama kuna ugumu wa kusimama. Pindi unapokua mjamzito, mimi sikupishi

Wanawake wote wakajikausha kumpisha mwenzao ndio Safari ikaenda hivyo, alisimama mpaka mwisho wa safari

NB: Wanawake mkishindwa kusaidiana nyinyi kwa nyinyi. Mimi nitaendelea na katabia haka aka
Sent using Jamii Forums mobile app
Waanze kwanza wanawake kuonyesha mfano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna upuuzi flani hawa watu wamekua nao.

Kuna siku nipo pale kongowe gari zinapakia kwa foleni kuelekea kigamboni. Ilw gari karibia iondoke kaja dada ana mtoto. Gari ishajaa. Nikamwambia dereva subiri, nikamwambia yule mama why usishuke una mtoto gari zipo nyingi tu hapo chini, akashuka.
Mara hatujakaa sawa mwingine nae huyo ana mtoto akapanda tena... Nikaona kumbe hawa wameshakariri wanajua tu mtu atajitokeza ampishe. Aaah watu tukajikausha kau..

Sent from my Nokia 6 using Jamii Forums mobile app
 
Yanga hasira zenu mnazihamishia kwa wajawazito, subirini jumamosi
Hahahaha...hapana kaka, naona njemba ilikuwa imechoka tu kwenye mihangaiko, game ya jmosi ni kitu ingine kabisa, tutajuwa ubora wenu baada ya kaushindi kwa wala haluwa...
 
Kikubwa Ni Upendo Tu! Mimi Kuna Bibi nilipisha siti, kumbe alikuwa anashukia njiani! wakati anashuka akamwita mdada kuja kukaa pale ,iliniuma sana,,,sikubishana naye,ukiangalia waliitana kwa kilugha,,. mambo mengine jiangalie wewe kama wewe, kama unaweza fanya,
 
Ningemchomoa huyo dada sitaki upuuzi, sitoi siti yangu kwa mtu ambaye siyo mgonjwa, hata mzee simpishi
images.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom