Leo ni Siku ya Ukimwi Duniani

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
10,270
8,045
SALA YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Mungu Baba Yetu

Katika siku hii ya UKIMWI Duniani tunakuja kwako na kila kitu kinacho tuponda ponda na kutusukuma

Tunakuomba:
Uwe pamoja na wanao na binti wote wanaoishi na VVU na UKIMWI.
Watoto wamekuwa yatima, wanawake wamekuwa wajane.
Vizazi vinatoweka. Mungu, utupe nguvu ya kukabili wimbi la UKIMWI katika
upana na ukubwa wake.

Tuinue juu ili tuweze kwenda ulimwenguni na kupambana dhidi ya UKIMWI
na ubaguzi na unyanyapaa wenye jeuri kubwa kwa wale walioathirika.

Tusaidie kukabiliana na kujitangazia haki kwetu binafsi na mawazo yetu yasiyo sahihi kuhusu VVU na wale walioambukizwa.

Fungua mioyo yetu kwa ajili ya mabadiliko na upatanisho. Katika wema wako Mungu wape mapumziko wale waliofariki kutokana na Ukimwi, na wale wanaoishi na na VVU.

Amina.
 
Back
Top Bottom