Leo ni Siku ya Sheria Nchini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leo ni Siku ya Sheria Nchini!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Buchanan, Feb 4, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Feb 4, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Leo tr 04/02/2010 ni siku ya Sheria nchini ambapo Mahakama zinaanza rasmi baada ya kuwa kwenye Judicial Vacation tangu tr 15/12/2009 hadi tr 31/01/2010. Mgeni rasmi atakuwa Mh JM Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ujumbe wa mwaka huu ni uboreshaji wa mahakama kama mdau wa maendeleo katika jamii (sina uhakika na exact wording ya ujumbe). Je, una maoni gani kuhusu utendaji kazi wa mahakama zetu? Zifanye nini ili kuboresha utendaji kazi wake?
   
 2. D

  Darling Member

  #2
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  VIZURI; watusaidie basi kuja sheria iko wapi katika masakata ya ufisadi. It is boring it is like we dont have sheria at all.
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Feb 4, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Darling, tatizo nafikiri sio sheria ila ni watungaji na watekelezaji wa hizo sheria ndio tatizo!
   
 4. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ni mengi mzee tu ya kurekebisha kwenye mfumo:

  Kuanzia uwezo wa Mahakimu, Majaji na watendaji wengine wa Mahakama Kama wasjili na Makarani. Hii inahitaji "system" nzima ya utoaji haki ikiwemo wateja Wapelelezi, Waendesha Mashtaka, Mawakili, na Serikali kutambua uozo uliopo na kuchuka hatua mahususi kurekebisha.

  Rushwa: Rushwa ni jambo lililoleta matabaka na tofauti kubwa sana ya kimaisha ya watumishi wa Mahakama na pengine kuwajengea viburi kwa wateja wao, hususan hawa waoitwa "Makarani" (Court clerks, or Registrar officers)!.Ukiacha athari zake xa kupoteza haki kwa mtu aliyestahili, rushwa inaharibu taaluma pia ya Mahakimu, Majaji, Wanasheria, waendesha mashtaka na wapepelezi

  Mahakama ni moja ya chombo ambacho kinaongoza kwa rushwa nchini, so to say!, kuchelewekwa kwa kesi, kesi kupangiwa kwa Mahakimu wasio makini na uwezo nazo hivyo kushindwa kuzimidu au kuzimaliza kwa muda muafaka ili jamii iweze kuwa na imani na Mahakama zetu.

  Mahakama za chini hasa za vijijini kukosa vitendea kazi, watendaji, tatizo la mfumo wa umangimeza kwa baadhi ya Mahakimu na Majaji (kujiona waumungu watu);

  Maboresho ya Sheria hayajagusa kwa kina matatizo sugu ya Mahakama , hakuna vitendea kazi, makitaba za kizamani au hazipo kwa sehemu nyingi, kompyuta pengine zipo lakini hazitumiki ipasavyo; huwezo wa kutunza kumbukumbu upo chini (hakuna kesi "updates" wala mtandao wa Mahakama unaotunza kesi zilizotolewa uamuzi katika siku za karibuni haupo).

  Huduma bado ni za kizamani sana za kutumia makaratasi, majalada na majitabu ya reja kusajili kesi (unaenda kutafuta kesi karani anachukua miezi sita kujua kinachoendelea; kumbumbu za kesi za siku (cause list) ukiacha pale Mahakama ya Biashara (Dar), ambapo mara nyingine zinakuwa "displayed" kielektoniki, Mahakama bado inajikita kwenye kumbumkubu za kumaliza makaratasi ubaoni, nk badala ya mfumo wa ki elektoniki;

  Masuala ya kijamii:- hakuna huduma ya vyoo wala vikalio (eneo la kupumzikia wateja katika Mahakama nyingi).

  Kesi kuchelewa na kuahirishwa pasipo sababu:- Kesi kuhairishwa pasipo taarifa za mapema kwa wateja, unakuta muda mabao kesi inakuja ndo karani anaibuka na ujumbe "eti, jamani Mheshimiwa leo hajisikii kuendelea na kesi yoyote mtapewa tarehe nyingine".... Hii inaleta usumbufu na gharama zizizo za msingi;

  Maslahi: - Maslahi ya utumishi ya Majaji ni Makubwa na manono ukilinganisha na Mahakimu ambao ndio wana kazin nyingi, hilo linapunguza morali....nk nk.

  Zaidi labda Jaji Mkuu (CJ) aelewa pia kumekuwa na tatizo pia kwenye mfumo wa Sheria Mpya ya Ajira na Mahusiano Kazini (Employment and Labour Relations Act) ya Mwaka 2004. Badala ya kupunguza na kuongeza kasi ya kushughulikia migogoro ya kazi kwa kuanzisha mfumo mbadala wa kusikiliza mashauri ya kazi (Alternative Dispute Resolution -ADR ) kupitia ngazi ya usuluhisi na uamuzi (Mediation & Arbitration), Mashauri yamekuwa mengi mno kwa Kamishna wa Usuluhishi na Uamuzi na Mahakama ya Kazi hata yale yasiyo na kichwa wala miguu, hii inatokana na kutokuwepo kwa utaratibu wa malipo kwa ngazi ya Usuluhishi na Uamuzi na pia hakuna vitendea kazi wala maafisa wa kutosha (Majaji na Wasuluhishi/ Waamuzi wa kumudu uwezo wa wateja...mantiki imepotea!.

  Huko kwenye kesi za jinai ndo imekuwa maumivu na majaribio kabisa baada ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuchungua Jukumu la Kuendesha Mashtaka Mahakamani ( Civilianization of prosecution service) kwa lengo la kutenganisha majukumu ya upelelezi na uendeshaji mashtaka (Separation of prosecution and investigation function) . Japo nia ni nzuri lakini kwa baadhi ya Mahakama, kesi nyingi zimekuwa zikichelewa kutokana na kukosekana kwa ushirikiano wa Karibu kati ya Mawakili wa Serikali (waendesha mashtaka) na Polisi/ Wapelelezi nk.

  Haya ndo Mawazo yangu!.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Feb 4, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180


  Hilo la kutenganisha upelelezi na prosecution nafikiri limeanza kufanyiwa kazi!
   
 6. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Long way to go!
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Feb 4, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ndio nchi yetu ambayo haina la kujivunia hata moja!
   
Loading...