Leo ngoja niongee "kwa kutumia akili nyingi" kuhusu hizi soda

Massawe909

JF-Expert Member
Jan 13, 2017
310
462
(KEY WORD:- HOFU)

FB_IMG_1506490131580.jpg

Nimesoma na kufundisha masomo ya sayansi, A-Level; ijapokuwa sasa ni mfanyabiashara. Nina weledi mkubwa katika masomo ya Physics, Chemistry na Biology. Mwaka 2007/2008 nilifundisha kama mwalimu wa muda(tempo teacher) pale Karatu Sekondari, kidato cha tano na sita masomo ya Chemistry na Biology.

Wanafunzi niliowafundisha pale Karatu Sekondari hebu nyoosheni mikono watu wawaone. Leo naweka biashara kando; nageukia sayansi ambayo kama unavyoona kwenye rekodi zangu ni kwamba nina weledi nayo wa kutosha!

Nyakati za karibuni kumekuwa na kampeni kali sana zinazopiga vita unywaji wa soda (hasa hasa Coca Cola na Pepsi) kwa madai kuwa zinasumu kali zenye hatari kubwa kwa afya. Awali ya yote nikiri wazi kwamba kwa sasa mimi sio mshabiki wa unywaji soda na ninakubaliana kuwa zina madhara kiafya kwa sehemu fulani.

Kilichonikasirisha ni ajenda ya kupinga unywaji soda ilivyobebwa na wauza madawa ya kienyeji(yaite ya asili) ambapo wanatumia muda mwingi kujaza hofu watu ili wauze hayo madawa yao. Wauzaji wa haya madawa hufanya maonesho na majaribio "mkwara" kuonesha namna soda aina hii zinavyotafuna nyama za mwili. Hawa wauzaji madawa ya kiuchwara huwa wanatoa sababu tano kusapoti ubaya wa Coca Cola lakini tatu za juu ndio hushika sana hisia za wengi. Sababu hizo ni kama zifuatazo kwamba CocaCola/Pepsi:-

1) Inayeyusha misumari
2) Inayeyusha mifupa
3) Inang'arisha marumaru
4) Ina madawa ya cocaine
5) Ina sukari nyingi mno.

Nimefanya utafiti wa kina kubaini uhalisia wa sababu hizi zinazotolewa hasa ikizingatiwa kuwa zinawatia hofu kubwa mno wale watumiaji na waliokwisha wahi kutumia soda hizi. Nilichogundua ni kuwa kampeni za kupinga matumizi ya Coca Cola (na soda nyingine zenye cocaine) zimetiwa chumvi kubwa mno na zina ajenda za kufanya watu waugue kwa hofu. Chumvi inayotiwa kwenye maelezo na hofu wanayowajaza watu ndio hugeuka kuwa mtaji wao na kuuza sana haya madawa wanayodai kuondoa sumu.

Hofu inaua na Shetani ndie muuaji. Nimetafiti sababu zote tano lakini hapa ninakuletea sababu tatu ambazo hushika zaidi hisia za watu. Ifahamike kuwa sina ugomvi na wauzaji wa madawa ya kuondoa sumu mwilini ambao huuza dawa zao kwa kutoa sababu za kisayansi zenye mashiko kuthibitisha ubaya wa soda hizi. Lakini hawa wenye mikwara ya hizi sababu tatu za juu, kwa kweli naomba tu niwateremkie kwa hoja! Maana huu mtindo wa kutumia mtindo wa kuwajaza watu hofu ili kuuza madawa ninauona ni aina mpya ya utapeli! Twende sasa:-

1) COCA COLA INAYEYUSHA HATA MISUMARI HIVYO NI HATARI MWILINI NA TUMBONI UNAPOINYWA

Wapiga vita wa Coca Cola wanasema hivi: ukifungua soda ya Coca Cola, kisha ukatumbukiza msumari; basi kesho yake unakuta msumari una kutu. Kikemia, ili kutu itokee panahitajika Iron, maji na oxygen. Msumari una madini ya Iron. Moja ya vitu vinavyotengeneza Coca Cola ni maji haya ya kawaida. Lakini unapofungua chupa ya soda unakuwa umeruhusu hewa ya oxygen kuingia. Tayari unakuwa na Iron + Maji + Oxygen = Kutu. Tunafahamu kutu hutafuna vyuma kwa hiyo sio jambo la ajabu msumari kupata kutu na kulika kwa sababu kinachofanya msumari ulike sio Coca Cola kwa ujumla wake bali ni uwepo wa maji (ya kawaida) na oxygen uliyoiruhusu kuingia baada ya kufungua chupa ya soda pamoja na msumari wako uliouweka. Kwa hiyo hiyo propaganda ya kuwa eti kunywa Coca Cola ni hatari kwa sababu inasumu inayotafuna hadi vyuma nadhani ni “umbumbumbu” wa kikemikali. Kwa wale tuliopita darasa la Chemistry tunaweza kuibaini "equation" ya kutu kama inavyoonekana hapa
Fe(Chuma) + H20 (Maji) + O2 (Oksijeni) = Fe(OH)3, (Kutu).

2) UKIWEKA MFUPA NDANI YA COCA COLA MFUPA UNAYEYUKA
Wapiga vita wanaendelea kusema kuwa: Eti ukiweka mfupa ndani ya Coca Cola, mfupa unayeyuka! Kutokana na hili wakosoaji wanasema hivi: “Ikiwa Coca Cola inayeyusha mifupa basi ndicho kinachotokea unapoinywa kwa sababu huko tumboni inaenda kuyeyusha mifupa ya mnywaji”. Kwanza si kitu cha ajabu kwa mfupa kuyeyuka unapouweka kwenye Coca Cola kwa sababu: Mifupa imeundwa kwa Calcium na ndani ya Coca Cola kuna Carbonate, unapochukua calcium na kuunganisha na carbonate unapata Calcium Carbonate (CaCO3) ambazo ni chembechembe (precipitates), ambazo ndizo zinazobaki baada ya kutumia calcium ya mfupa! La pili la kufahamu ni kuwa Coca Cola inapoingia tumboni hakuna mahali popote inapokutana na mfupa katika mmeng’enyo wa chakula, hivyo kusem eti kwa sababu Coca Cola inatafuna mifupa basi ukiinywa itaitafuna mifupa yako si kweli kibaiolojia na kikemia!

3) COCA COLA INANG'ARISHA MARUMARU HIVYO INAWEZA KUKWANGUA MWILI WAKO.
Tunatakiwa kujua kuwa moja ya viambata vya Coca Cola (ingridients) ni Carbonate (carbonated water) ambayo ni madini yanayohitajika mwilini na wala hayana shida kabisa. Marumau zinatengenezwa kwa mchanganyiko unaohusisha Calcium. Unapoimwaga Coca Cola juu ya marumaru, ile Carbonate (iliyopo ndani ya Coca Cola) inaungana na Calcium kutengeneza Calcium Carbonate ambayo tena huungana na Carbondioxide pamoja na unyevunyevu (humidity); kisha kunazalisha ayonsi (ions) zinazoivunjavunja ile calcium ya kwenye marumaru, na ndio maana unaona marumaru iking’aa. Kwa hiyo kinachoing’arisha marumaru sio Coca Cola kwa ujumla wake bali ni mchanganyiko wa kikemikali wa kawaida kabisa kutokana na madini yaliyomo kwenye marumaru zenyewe! Mtu asikutishe, wanakemia wote tunafahamu "equation" hii
CaCO3 + H2CO3 = Ca+2 + 2HCO-3 [1]. Nimemaliza!

NAWAOMBENI:-

1. Kama unamfahamu bosi yeyote wa CocaCola, tafadhali naomba umwambie waharakishe wanitumie cha juu changu, kwa sababu kwanza nimewatetea na pili nimewatangaza, haaa! Haaa!

2. Kama ukisikia serikali inatafuta walimu wa sayansi tafadhali nishtue nikapige chaki, maana ni mkali balaa. Wanafunzi wangu niliowafundisha wananifahamu vizuri, naingiaga darasani bila notisi, mafomula yote natiririsha kutoka kichwani Haaa! Haaa!

[HASHTAG]#Albertnyaluke[/HASHTAG] sanga
 
Hiyo ya kung'arisha marumaru nilsema siku moja nikapigwa nyundo, ila nilisikia na kusita kunywa Coka, sikua na utafiti (no research no right to speak) Nashukuru mwalimu kwa utafiti wako.
 
كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُور

((Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu)) [Al-'Imraan: 185]
 
Kila kitu ukizidisha huwa na madhara, hivyo nimhimu kuwa na kiasi, kuna mtu anakunywa soda hadi Tano au sita kwa siku, sasa unategemea nini kwa mtu Kama huyo.
 
Ninafahamu Coca Cola ina sukari nyingi pia carbonet acid nyingi mwilini inachochea weight issues. Sita acha kunywa Coca Cola ingawa sasa hivi ninajunywa mbili weekend tu.

Jukamiiana kunaleta UKIMWI, fizzy drinks ni hatari kwa afya sasa tukifuata yote mbona maisha yatakuwa miserable
 
Ninafahamu Coca Cola ina sukari nyingi pia carbonet acid nyingi mwilini inachochea weight issues. Sita acha kunywa Coca Cola ingawa sasa hivi ninajunywa mbili weekend tu.

Jukamiiana kunaleta UKIMWI, fizzy drinks ni hatari kwa afya sasa tukikutana vyote mbona maisha yatakuwa miserable
kipi bora, kujamiiana au kunywa pepsi mkuu?:D:D
 
Mzee wangu alikuwa ananiagiza coca wakati anasafisha caption za RUBY. Aisee ile kitu inang'arisha ruby hadi mTHAILAND anachanganyikiwa.
 
(KEY WORD:- HOFU)

View attachment 596608

Nimesoma na kufundisha masomo ya sayansi, A-Level; ijapokuwa sasa ni mfanyabiashara. Nina weledi mkubwa katika masomo ya Physics, Chemistry na Biology. Mwaka 2007/2008 nilifundisha kama mwalimu wa muda(tempo teacher) pale Karatu Sekondari, kidato cha tano na sita masomo ya Chemistry na Biology.

Wanafunzi niliowafundisha pale Karatu Sekondari hebu nyoosheni mikono watu wawaone. Leo naweka biashara kando; nageukia sayansi ambayo kama unavyoona kwenye rekodi zangu ni kwamba nina weledi nayo wa kutosha!

Nyakati za karibuni kumekuwa na kampeni kali sana zinazopiga vita unywaji wa soda (hasa hasa Coca Cola na Pepsi) kwa madai kuwa zinasumu kali zenye hatari kubwa kwa afya. Awali ya yote nikiri wazi kwamba kwa sasa mimi sio mshabiki wa unywaji soda na ninakubaliana kuwa zina madhara kiafya kwa sehemu fulani.

Kilichonikasirisha ni ajenda ya kupinga unywaji soda ilivyobebwa na wauza madawa ya kienyeji(yaite ya asili) ambapo wanatumia muda mwingi kujaza hofu watu ili wauze hayo madawa yao. Wauzaji wa haya madawa hufanya maonesho na majaribio "mkwara" kuonesha namna soda aina hii zinavyotafuna nyama za mwili. Hawa wauzaji madawa ya kiuchwara huwa wanatoa sababu tano kusapoti ubaya wa Coca Cola lakini tatu za juu ndio hushika sana hisia za wengi. Sababu hizo ni kama zifuatazo kwamba CocaCola/Pepsi:-

1) Inayeyusha misumari
2) Inayeyusha mifupa
3) Inang'arisha marumaru
4) Ina madawa ya cocaine
5) Ina sukari nyingi mno.

Nimefanya utafiti wa kina kubaini uhalisia wa sababu hizi zinazotolewa hasa ikizingatiwa kuwa zinawatia hofu kubwa mno wale watumiaji na waliokwisha wahi kutumia soda hizi. Nilichogundua ni kuwa kampeni za kupinga matumizi ya Coca Cola (na soda nyingine zenye cocaine) zimetiwa chumvi kubwa mno na zina ajenda za kufanya watu waugue kwa hofu. Chumvi inayotiwa kwenye maelezo na hofu wanayowajaza watu ndio hugeuka kuwa mtaji wao na kuuza sana haya madawa wanayodai kuondoa sumu.

Hofu inaua na Shetani ndie muuaji. Nimetafiti sababu zote tano lakini hapa ninakuletea sababu tatu ambazo hushika zaidi hisia za watu. Ifahamike kuwa sina ugomvi na wauzaji wa madawa ya kuondoa sumu mwilini ambao huuza dawa zao kwa kutoa sababu za kisayansi zenye mashiko kuthibitisha ubaya wa soda hizi. Lakini hawa wenye mikwara ya hizi sababu tatu za juu, kwa kweli naomba tu niwateremkie kwa hoja! Maana huu mtindo wa kutumia mtindo wa kuwajaza watu hofu ili kuuza madawa ninauona ni aina mpya ya utapeli! Twende sasa:-

1) COCA COLA INAYEYUSHA HATA MISUMARI HIVYO NI HATARI MWILINI NA TUMBONI UNAPOINYWA

Wapiga vita wa Coca Cola wanasema hivi: ukifungua soda ya Coca Cola, kisha ukatumbukiza msumari; basi kesho yake unakuta msumari una kutu. Kikemia, ili kutu itokee panahitajika Iron, maji na oxygen. Msumari una madini ya Iron. Moja ya vitu vinavyotengeneza Coca Cola ni maji haya ya kawaida. Lakini unapofungua chupa ya soda unakuwa umeruhusu hewa ya oxygen kuingia. Tayari unakuwa na Iron + Maji + Oxygen = Kutu. Tunafahamu kutu hutafuna vyuma kwa hiyo sio jambo la ajabu msumari kupata kutu na kulika kwa sababu kinachofanya msumari ulike sio Coca Cola kwa ujumla wake bali ni uwepo wa maji (ya kawaida) na oxygen uliyoiruhusu kuingia baada ya kufungua chupa ya soda pamoja na msumari wako uliouweka. Kwa hiyo hiyo propaganda ya kuwa eti kunywa Coca Cola ni hatari kwa sababu inasumu inayotafuna hadi vyuma nadhani ni “umbumbumbu” wa kikemikali. Kwa wale tuliopita darasa la Chemistry tunaweza kuibaini "equation" ya kutu kama inavyoonekana hapa
Fe(Chuma) + H20 (Maji) + O2 (Oksijeni) = Fe(OH)3, (Kutu).

2) UKIWEKA MFUPA NDANI YA COCA COLA MFUPA UNAYEYUKA
Wapiga vita wanaendelea kusema kuwa: Eti ukiweka mfupa ndani ya Coca Cola, mfupa unayeyuka! Kutokana na hili wakosoaji wanasema hivi: “Ikiwa Coca Cola inayeyusha mifupa basi ndicho kinachotokea unapoinywa kwa sababu huko tumboni inaenda kuyeyusha mifupa ya mnywaji”. Kwanza si kitu cha ajabu kwa mfupa kuyeyuka unapouweka kwenye Coca Cola kwa sababu: Mifupa imeundwa kwa Calcium na ndani ya Coca Cola kuna Carbonate, unapochukua calcium na kuunganisha na carbonate unapata Calcium Carbonate (CaCO3) ambazo ni chembechembe (precipitates), ambazo ndizo zinazobaki baada ya kutumia calcium ya mfupa! La pili la kufahamu ni kuwa Coca Cola inapoingia tumboni hakuna mahali popote inapokutana na mfupa katika mmeng’enyo wa chakula, hivyo kusem eti kwa sababu Coca Cola inatafuna mifupa basi ukiinywa itaitafuna mifupa yako si kweli kibaiolojia na kikemia!

3) COCA COLA INANG'ARISHA MARUMARU HIVYO INAWEZA KUKWANGUA MWILI WAKO.
Tunatakiwa kujua kuwa moja ya viambata vya Coca Cola (ingridients) ni Carbonate (carbonated water) ambayo ni madini yanayohitajika mwilini na wala hayana shida kabisa. Marumau zinatengenezwa kwa mchanganyiko unaohusisha Calcium. Unapoimwaga Coca Cola juu ya marumaru, ile Carbonate (iliyopo ndani ya Coca Cola) inaungana na Calcium kutengeneza Calcium Carbonate ambayo tena huungana na Carbondioxide pamoja na unyevunyevu (humidity); kisha kunazalisha ayonsi (ions) zinazoivunjavunja ile calcium ya kwenye marumaru, na ndio maana unaona marumaru iking’aa. Kwa hiyo kinachoing’arisha marumaru sio Coca Cola kwa ujumla wake bali ni mchanganyiko wa kikemikali wa kawaida kabisa kutokana na madini yaliyomo kwenye marumaru zenyewe! Mtu asikutishe, wanakemia wote tunafahamu "equation" hii
CaCO3 + H2CO3 = Ca+2 + 2HCO-3 [1]. Nimemaliza!

NAWAOMBENI:-

1. Kama unamfahamu bosi yeyote wa CocaCola, tafadhali naomba umwambie waharakishe wanitumie cha juu changu, kwa sababu kwanza nimewatetea na pili nimewatangaza, haaa! Haaa!

2. Kama ukisikia serikali inatafuta walimu wa sayansi tafadhali nishtue nikapige chaki, maana ni mkali balaa. Wanafunzi wangu niliowafundisha wananifahamu vizuri, naingiaga darasani bila notisi, mafomula yote natiririsha kutoka kichwani Haaa! Haaa!

[HASHTAG]#Albertnyaluke[/HASHTAG] sanga

sijui tumuamini nani sasa
 
Pole kaka. Thread umeiandika kwa staili ya kuvutia sana majivuno yako ya ufahamu mkubwa wa chemistry umeyapooza kwa mzaha/ utani wa hapa na pale. Kweli kampuni ya Bonite inatakiwa ikushike mkono!
 
Back
Top Bottom