#COVID19 Leo ndo nimeamini COVID-19 ni hatari

Uswiss

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
842
2,160
Nilikuwa nachukulia poa hii kitu. Yaani kuvaa barakoa na kunawa sijui mikono ilikuwa ni mpaka nione kuna ulazima au kulazimishwa.

Mfano nikienda hospital ni mpaka nione watu hawaruhusiwi kuingia bila barakoa ndo na mimi nitanunua na kuvaa. Ila sasa yaliyotokea leo ndugu zangu nimenyoosha mikono juu. Yaani nimepigiwa simu jana saa nne usiku naambiwa mama yako mkubwa anaumwa kifua kimembana na vichomi tunampeleka hospitali, nikachukulia kawaida tu. Kufika saa saba na nusu usiku watu wanapiga simu wanalia amefariki.

Nimefika msibani tena naambiwa watoto wake wawili wamelazwa hospitali wapo hoi kwa tatizo hilo hilo la vifua kubana na vichomi. Aise ikabidi nitoke kimya kimya kwanza kwenda kununua barakoa za kutosha na groves kabisa maana ni hatari.

Covid ipo ndugu zangu ni hatari na inaua ghafla ghafla kabla hata hujatubu dhambi zako.

Take care chukua tahadhari.
 
Wabongo sisi nimatomaso bila kukumbwa kwanza kuamini ngumu

nilipita juzi ferry niliogopa watu wamejazana jumba la kusubiria magogoni MV ,wenyebarakoa wawili harafu kunatangazo linaendelea vaeni barakoa
Walinzi wapo

Unaishia kusema mungu ,basi
 
Back
Top Bottom