Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 734
TAIFA Stars ilithubutu kuifunga Chad kwao, leo iifunge timu hiyo Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ili isonge mbele.
Hivyo ndivyo unavyoweza kuzungumza mtihani muhimu kwa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars wakati itakaporudiana na Chad mchezo wa mchujo kuwania kuingia hatua ya makundi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Ndjamena, Chad Ijumaa iliyopita Taifa Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Mrisho Ngassa na Nurdin Bakari.
Kama ikifanikiwa kushinda mchezo wa leo, Taifa Stars itakuwa kundi moja na nchi za Morocco, Ivory Coast na Gambia katika kampeni za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza mwakani, ambapo fainali zake zitafanyika Brazil mwaka 2014.