Beni huyu Saa nane, kenda karibu na kumi
Bora sana tusinene, mukatuona wahuni
La moyoni tuliseme, isiwe yu aridhini
Siri wanayo wanene, yazungumzwa vikaoni
Beni siyo alibino, kama angekuwa dili
Ni mweusi kama wino, na hanao mwingi mwili
Iweje leo hayumo, humu ndani kwa ipi siri
Wametaka yake meno, tuwaulize majangiri!
Beni ni kitendawili, ajuwae ategue
Kajificha cha tumbili, ndio nionavyo mie
Hatunae tena kimwili, ajuwae atwambie
Haisemwi hii siri, hata na bosi wake Mbowe
Sitaki kusema sana, nitakwe kuomba radhi
Leo sote tumeona, nisije poteza hadhi
Ikiwa hatujamuona, kazongwa na nyingi kazi
Ni nyingi zimembana, tokea hayo majuzi
Beni urudi nyumbani, usikawie mwanetu
Watutia kisirani, sote tafrani mtu
Tusikii hatuoni, tumefika kwa Wahutu
Kama uko kwa jirani, urudi nyumbani kwetu