Ninaamini Ben Mzima na Mungu anamlinda huko aliko

Ninaamini Ben Mzima na Mungu anamlinda huko aliko

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
LEO NAWATUKANA!

d158a81ed39d8b474d691dcf7490a292.jpg

1
Sianzi na ashakumu, leo ninawatukana,
Mwaufanya uwazimu, na mambo yaso maana,
Huu si ubinadamu, pia siyo uungwana,
Ben wetu yuko wapi?
2
Ben hakuwa mzimu, vipi asionekane?
Kama karuka sehemu, uhamiaji wanene,
Na kama ni marehemu, mwili wake tuuone,
Ben wetu yuko wapi?
3
Bavicha machakaramu, Katambi una laana,
Siku saba zishatimu, Desemba mwaka wa jana,
Nyumbu twataka fahamu, komeni kulaliana,
Ben wetu yuko wapi?
4
UTG zenu salamu, mlipo muitikie
Sina pesa hali ngumu, fulana siniuzie,
Lengo si kuwalaumu, ila nanyi mtwambie,
Ben wetu yuko wapi?
5
Serikali naheshimu, ila kwa hili hapana,
Mloona kwenye simu, sasa yawekwe bayana,
Tunataka kufahamu, naye walopigiana,
Ben wetu yuko wapi?
6
Mbowe ni mtu muhimu, ana kubwa sana dhima,
Ela naye kala ndimu, hataki hata kusema,
Kiasi ni mtuhumu, kaushiriki unyama,
Ben wetu yuko wapi?
7
Nimtaje Jeyi Pi Emu, tuliyempa dhamana,
Mjuwe namuheshimu, ila namna hakuna,
Sikute anayo damu, ya huyu wetu kijana,
Ben wetu yuko wapi?
8
Kalamu naomba koma, miye sina roho mbili,
Siniletee nakama, nikenda fichwa mahali,
Kisha niwe madhuluma, athama hili suali,
Ben wetu yuko wapi?

31 January 2017 Jumanne 21:29
Jina la Mtunzi Dotto Rangimoto
Jina la utunzi Jini Kinyonga
Simu 0762845394 Morogoro.

9830be59ba97002d9367cce49c6722cf.jpg


MAELEZO KIDOGO

Ninamini Ben Mzima na Mungu anamlinda huko aliko, haya ni majaribu tu, midhali tu wanadamu hayana budi, ila roho inauma sana kuona kijana maridadi, nadhifu, mwenye akili kubwa na mwenye kuhitajika na kutegemewa na taifa anapotea hivihivi na kirahisi kabisa!

Unaweza kusema wengi wanapotea lakini kwanini Ben tunambebea bango. Nadhani ni sababu mbili kuu.

Mosi.
Ben ni mkosoaji mkubwa wa rais Magufuli na serikaki yake na anakumbukwa vizuri kwa hoja yake PhD ya fake ya rais Magufuli.

Kwa vyovyote vile kupotea kwa Ben kunapelekea serikali na rais Magufuli wasiaminike na hasa ukizingatia kabla ya Ben kutoweka aliripoti kwenye ukurasa wake wa fb uwepo watu kumtishia usalama wake endapo angeendelea kumkosoa rais.

Kupotea kwa Ben kumepelekea serikali kutuhumiwa kutumia mkono wa chuma kushughulikia wakosoaji wake. Kweli mtaani watu wengi hupotea tu na hawashikiwi bango zaidi ya kuona matangazo yao katika vyombo vya habari, kwa upande Ben inashikiwa bango sababu serikali yenye wajibu wa kikatiba kuwalinda raia ndiyo inayotuhumiwa kumpoteza Ben-Rabiu Wa Saanane

Kwahivyo hapa utaona kuwa serikali inatakiwa kumtafuta Ben si kwasababu ni wajibu wake tu lakini pia kama njia kuu na ya msingi ya kijisafisha dhidi ya tuhuma hizi. Najuwa ukosoaji wa Ben kwa serikali haukuwa wa kificho na kwahivyo hata maadui wa nchi yetu wanaweza kutumia mwanya huo ili kuleta uchonganishi kati ya serikali na wananchi, yaani, wampoteze Ben ili serikali ibebeshwe lawama, na kwasababu hii ndipo utaona ulazima na umuhimu wa serikali kulichunguza suala la Ben kwa kina.

Pili.
Matokeo ya Ben ya kidato cha nne, sita na elimu yake juu, na kubwa zaidi uwezo wake wa kuchambua na kuelewa mambo ni dhahiri serikali ilitakiwa kumtumia Ben kwa manufaa ya nchi hii pamoja na kwamba ni mwanachama wa chama cha upinzani. Sababu vipo vitengo serikalini ambavyo Ben angepachikwa na kuleta tija kwa taifa hata kama Ben mwenyewe hakuomba, mathalan, Prof Kitila aliomba kuwa katibu mkuu? Lakini alionekana ni mgodi unaotembea sasa kwanini usitulie ofisi umwage dhahabu?

NjanoTano au Jini Kinyonga
Morogoro
 
Kumbuka kuna serikali zenye mifumo tofauti tofauti za kiutawala, kifalme, demokrasia, kiimla.
Sasa kwa yanayoendelea hapa nchini, unaweza kupata jibu awamu hii inamrengo gani...
 
Kama ni mzima basi Mungu ampe afya nguvu kwa magumu anayopitia huko.

Kama alikwishakufa basi Mwenyezi Mungu ampunguzie adhabu ya kaburi na kilaaniwe kizazi chote kilichoshiriki dhambi hiyo.
 
Mbowe kapwaya sana, inakuwaje mambo haya yanatokea halafu yupo kimya kwa matendo!?
 
Back
Top Bottom