Leo nahisi mke wangu anachepuka huko alipoenda

Hujasababisha chochote acha ufala wewe,mwanaume kuwa na mwanwmke zaidi ya moja ilikuwepo toka kipindi cha yesu.

Fukuza huyo Mwanamke,huna Mkwe hapo.
Mkuu hata ukahaba ulianza toka kipindi cha Yesu na aliwasamehe unataka kusemaje labda? Kwamba kama dhambi ilianza toka kipindi cha Yesu ndiyo inakuwa siyo dhambi au?
 
Hii nakiri kosa mkuu naeza kuwa nimesababisha

Kosa lako, fix your mess. Hii ndoa hata ikivunjika mhusika mkuu wa uvunjaji wa hii ndoa ni wewe! Wewe umeanza, wife kamaliza. Unachepuka halafu ukichepukiwa unaumia . Unakiri kuchepuka halafu unasema hiyo haimpi uhalali wife kuchepuka .

Ulikua ukiwasiliana na mchepuko wako, wife nae alikua akichati na mchepuko wake . Ulipanga kulala na mchepuko wako sema ikashindikana, wife na yeye sijui ndo walikutana na mchepuko wake .

Anyway thamani ya ndoa imeshuka mno siku hizi, mtu haoni shida kukiri hadharani kuwa anachepuka na akamlalamikia mkewe kwa nini anachepuka
 
Yaaa akili nyingine inasema hivo kwakujiangalia mimi ni mara nyingi nimechepuka lkn sijawahi kumwonyesha

Yeye sasa ameamua kukuonyesha next time ukichepuka hakikisha na yeye anajua ili mwende sawa, haiwezekani we uchepuke kwa kujificha ficha halafu yeye afanye wazi wazi tu
 
Mkuu usishangae mpka mida hii sioni dalili za yy kurud home acha tu mi nimeamua nitulie zangu tu hapa kumsubir asipo rud bas ntafanyaje sasa
Hongera kwa kuvumilia, maana ungemwambia umerudi upo home ungeboronga upelelezi wako!
 
Duuuuuh, mwamba kashampasua huyo, ila hongera sana kwa uvumilivu, mi nlivyokua nasoma huu uzi nilijua mwisho itakua mwanamke hana jicho na meno manne ya mbele hivyo kalazwa MOI
 
Wakuu ipo hivi nilisafir toka jtano mkoa flan plan ya kurudi ilikuwa jmos kesho jion lakin nikaamua tu nirudi leo kwa sababu kazi nilionda kufanya imeisha toka jana jion.

Sasa nikampigia mchepuko wangu leo narudi aje anipokee leo narud zangu Dar , na nikamwambia ntafika saa kumi na moja so awe hapo,

Huku wife anajua kesho jmos ndio nakuja tena jion sana ndio ratiba nilivyompa ila plan yangu ni nikalale sehem na mchepuko wangu na kushinda nae mpka jion.

Nimefika stand sijamkuta na piga simu hapokei nikasema poa acha tu niende zangu home kwanza nimechoka sana ntamchek next time huu ni mchepuko haunaga shida niko nae kitambo na anamjua wife vizur sana ,pia anasubir nimwoe mke wa pili nimemwambia awe na subira,

Hata hivo nimefika home ndio mchepuko anajibu Sorry nilipitiwa nilikuwa nimelala so nakusubir tunafanyaje nikamjibu Poa subir ntakwambia,

Tatizo nimerud home wife hayupo na sasa inaenda saa tatu usiku nimefika toka saa moja usiku na nimempigia simu just kumwambia vipi huko unaendeleaje kasema yupo home anaangalia tamthilia zake yaan hapa nilipo uongo sijui kaanza lin huyu wife

Tena kwa saut kavu kabisa anasema nipo nyumbani anaangalia tu tamthilia na anaanza kunihoji unarudi saa ngapi kesho mi nikamjibu tu kesho usiku saa mbili hivi kasema sawa nimletee zawadi.

nafkiri tabia hii imeanza muda kidogo japo huwez kujua kirahis ila mtu unaye kaa nae mabadiliko kidogo tu utajua kuna shida maana alikuwa hayupo huru sana na simu yake na hata akiiweka anaigeuza sehem ya mbele inakua chin na passward kabadilisha na simwoni tena kufatilia nyendo zangu kama zaman.

itakuwa kuna msela ameshakula mzigo tayar naleo mida hii itakuwa anakula,,

Nimefika tu kuingia ndani bafun mtu ameoga,mswaki amepiga,na ni kama tumepishana tu mi nafika saa moja kamil yy itakuwa ametoka saa kumi na mbili jioni.,

Hapa nawaza sijui nimpigie tu mchepuko wangu nikalala huko au nimpigie wife arud home .

Inauma lakn hebu wakuu nipeni msaada tumezaa nae watoto wa wili wote madume sema walienda kwa bibi yao mwezi sasa ndio maana amekuwa huru kutoka.,

Pia huwa inaeza kuwa hata mimi nimechangia maana huwa nachepuka marakwamara lkn hajawahi kunikamata ila hiyo haihalalishi yeye pia achepuke.

Nawasilisha...

Mrejesho wa kisa hiki soma hapa:Mrejesho: Kilichotokea baada ya wife kurudi saa sita usiku
Na wewe chepuka my friend ereeeeee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom