Leo IKULU Bashe kaanza vizuri japo kakosea

Leo IKULU Bashe kaanza vizuri japo kakosea

Ni ubaguzi kumpinga Mh. Bashe kwa kuanza na asili yake eti msomali. Hivi umaskini Wa nchi hii umeltwa na minority groups, sio wabantu tunaongoza tangu Uhuru,, sasa usomali unatoka wapi. Kwa taarifa yalo Afrca south of sahara zinaelekea kuwa failed states sababu ya muono myopic kudhani uzalendo ni uzawa . Kaunda ni mzalendo Zambia, asili yake nialawi.
 
Ukiwa nje ya uwanja unaweza kucheza utakavyo kwa kukisia tu na kutikisa kichwa, huyo Msoma Ali ni lopo lopo tu na sioni kama kuna weredi wowote labda aendelee kuchukua huo unaoita ushauri.... kwa mfano wa uandishi kama huu ni mashaka makubwa kuhusu set up ya kichwa chake. [emoji1484][emoji1484][emoji1484][emoji1484]
View attachment 1161465
Mkuu naona umeamua kujikita kwenye personalities badala ya substance.
 
Ni hivi, mimi ni mkulima sina muda wa hizo porojo za ushirika, navuna mazao yangu na kumuuzia mwenye pesa, mambo ya kupeleka mazao yangu kusimamiwa na watu wasio hata na bustani ya mchicha sina. Huna pesa kaa kushoto na mazao yangu, wakajiunge na ushirika wale wenye muda wa kupigiwa siasa mfu.
He Heee, tindo Bhwanaah! Naziona hisia zile zile za kuuuleeee kwa akina Mbowe.
Tulia uwaze hayo maneno uliyoandika hapo juu.

Mkulima ni lazima awe na njia sahihi, zenye mpangilio zitakazohakikisha nguvu zake zinamletea manufaa stahiki.
Vyama vya ushirika ni vya wakulima wenyewe. Ndio wananchama na ndio wanaowachagua viongozi wao na kuwasimamia.

Hawa viongozi hawafanyi kazi nje ya matakwa ya wanachama wao, bali wapo kama watendaji kuhakikisha waliyoamua wanachama ndiyo yanayofanyika.

Unayoyasema hapa wewe ndio ule ushirika mbaya uliokosa usimamizi uweze kuwanufaisha wakulima. Na hilo la ununuzi wa holela toka kwa kila mkulima binafsi ndio janga kuu kwa mkulima. Wewe unatazama sehemu moja ya miaka ya neema, wakulima wanapopata mazao mengi huku soko likiwa hakuna kitu. Huangalii mkulima anapohangaika na mazao yake wakati soko limebuma.

Lakini pia ni lazima nifafanue kwa kifupi jinsi ushirika wa wakulima wa Kenya unavyofanya kazi.

Hawa ni wakulima, kama mia kadhaa waliojiunga pamoja na kufanya ushirika. Ushirika huu haununui mazao yao. Wanunuzi ni wafanya biashara. Sasa badala ya hawa wafanya biashara kwenda kwa mkulima mmojammoja na kupanga naye bei ya mazao yake, ushirika wao ndio unaosimamia kazi hii na mambo mengi mengine yanayowanufaisha wakulima.

Hawa wakulima kupitia kwa ushirika wao wanaingia mikataba na wanunuzi (wafanya biashara), kuhusu bei ya mazao yao na mambo mengine yanayohusu ufanisi wa kilimo wanachofanya wakulima hao.
Hii kwa kifupi ni "Contract Farming", ina mapungufu yake pia. Lakini ukilinganisha na mtindo huo wa 'holela' unaoupigia upatu hapa, mikataba hii ni bora zaidi kwa mkulima.
Wakulima wengi wadogo wadogo wananufaika na hali zao za kipato zinaimarika.
 
He Heee, tindo Bhwanaah! Naziona hisia zile zile za kuuuleeee kwa akina Mbowe.
Tulia uwaze hayo maneno uliyoandika hapo juu.

Mkulima ni lazima awe na njia sahihi, zenye mpangilio zitakazohakikisha nguvu zake zinamletea manufaa stahiki.
Vyama vya ushirika ni vya wakulima wenyewe. Ndio wananchama na ndio wanaowachagua viongozi wao na kuwasimamia.

Hawa viongozi hawafanyi kazi nje ya matakwa ya wanachama wao, bali wapo kama watendaji kuhakikisha waliyoamua wanachama ndiyo yanayofanyika.

Unayoyasema hapa wewe ndio ule ushirika mbaya uliokosa usimamizi uweze kuwanufaisha wakulima. Na hilo la ununuzi wa holela toka kwa kila mkulima binafsi ndio janga kuu kwa mkulima. Wewe unatazama sehemu moja ya miaka ya neema, wakulima wanapopata mazao mengi huku soko likiwa hakuna kitu. Huangalii mkulima anapohangaika na mazao yake wakati soko limebuma.

Lakini pia ni lazima nifafanue kwa kifupi jinsi ushirika wa wakulima wa Kenya unavyofanya kazi.

Hawa ni wakulima, kama mia kadhaa waliojiunga pamoja na kufanya ushirika. Ushirika huu haununui mazao yao. Wanunuzi ni wafanya biashara. Sasa badala ya hawa wafanya biashara kwenda kwa mkulima mmojammoja na kupanga naye bei ya mazao yake, ushirika wao ndio unaosimamia kazi hii na mambo mengi mengine yanayowanufaisha wakulima.

Hawa wakulima kupitia kwa ushirika wao wanaingia mikataba na wanunuzi (wafanya biashara), kuhusu bei ya mazao yao na mambo mengine yanayohusu ufanisi wa kilimo wanachofanya wakulima hao.
Hii kwa kifupi ni "Contract Farming", ina mapungufu yake pia. Lakini ukilinganisha na mtindo huo wa 'holela' unaoupigia upatu hapa, mikataba hii ni bora zaidi kwa mkulima.
Wakulima wengi wadogo wadogo wananufaika na hali zao za kipato zinaimarika.

Narudia tena Kalamu1, sio kwamba sioni hoja zako, lakini nakuambia jambo ninalolijua kwa vitendo sio kwa nadharia, ww uko kinadharia zaidi kuliko uhalisia. Uhuni unaofanyika kwenye vyama vya ushirika sisi wakulima tunaujua, ni vyema kila mtu auze anapojua, sio kusubiri matapeli kwa jina la vyama vya ushirika.

Nasisitiza tena, huna pesa mkononi kaa kushoto na mazao yangu, maana sina muda wa kwenda kupangiwa muda wa kupata pesa yangu. Anayetaka kujiunga na chama cha ushirika kwakuwa kina faida kama ulivyosema ni sawa na nitamuunga mkono ila sio mimi.
 
Mkuu japo naona kama unajibu jambo ambalo Bashe amelisema au kulianzisha pamoja na kwamba sijui ni nini na wewe huelezi....naunga mkono wakenya waende kwa wakulima kununua mahindi yao...hao walanguzi wa katikati ni wabaya sana na kuwagandamiza wakulima !!
Kilimo ni nini?
 
Mkuu umenena. Kama ambavyo tunaagiza ngano na kusagisha hapa nyumbani, hivyo hivyo wanunuzi wa mahindi wanataka kununua na kusagisha huko kwao watakavyo na kutokana na taste ya walaji wa kwao. Hatuwezi kuwalazimisha kununua unga wa kwetu, after all shelf life ya unga ni ndogo sana ukilinganisha na mahindi yanayoweza kuhifadhiwa kwa miaka.
saa ingine wanahitaji mahindi ya kupika makande,au kutengeza chakula cha kuku,wewe unataka kuuwauzia unga,hawakubali
Kalamu1
Nimesoma, lakini sikufika mwisho aisee, kwa sababu ninakubaliana na hoja yako moja kwa moja.
Nani yule, anauza unga wa ngano (AZAM). Kwa nini unga wa mahindi uwe shida?

Hakuna sababu hata ndogo kwa Tanzania kuuza mahindi Kenya. Kama ni mfanya biashara, weka mashine zako pale karibu na mpaka, nunua mahindi, saga kwa viwango vinavyotakiwa kwa bidhaa hiyo huko Kenya, package na nenda kasambaze kwenye supermarkets zao bidhaa zako. Shida ipo wapi

Mbali ya mahindi. Kwa nini tunaruhusu kuuza vitunguu kwa makampuni ya Kenya yanayo package na kuvisafirisha nje ya nchi hiyo kama bidhaa toka nchini humo. Hapa kwetu hatuna wafanya biashara wanaoweza kukusanya toka kwa wakulima, wakapackage' na kusafirisha nje kama bidhaa yetu, iliyotoka Tanzania?
Hawa wafanya biashara wetu wapiga kelele nyingi lakini akili ni kama zimelala.

Haya, sasa tunazungumza kuwauzia gesi, wakatengeneze umeme. Hivi hapa kwetu hatuwezi kuzalisha umeme na kuusafirisha hadi Kenya?

Tanzania tunayo matatizo makubwa!

Kalamu1 naungana na mawazo yako,mahindi yakiwa processed hapa kwetu hiyo maana yake tumebakisha ajira nyumbani.Mansander kwenye uzi huu majibu ya hoja zako nafikiri umeyaona,mtu kama kweli hii ni biashara yake yeye atajua wateja wake kule Kenya wanataka bidhaa katika hali gani mfano. mahindi yaliyokobolewa,unga wa sembe au dona ama anahitaji pumba. Uwezo wa kuwalazimisha hatuna lakini uhitaji wao ndo utawafanya waweke mezani wanahita end product ikiwa katika hali gani nasi tutatii kwakuwa tunaitaka pesa yao that is business. Shelf time ya unga kuwa ndogo ukilinganisha na ile ya mahindi ni sawa,kwa mfanya biashara makini ndo maana anakuwa na ghala la kufifadhia mahindi yake kwahiyo atakuwa akiyaprocess kulingana na mahitaji ya soko.
Elungata nawe nafikiri umeona majibu ya hoya zako. Kwahiyo kila mteja ataleta mahitaji yake na atapatiwa bidhaa yake.
Kalamu1 Tanzania tunayo matatizo makubwa! Na kinyume chake pia ni sahihi,matatizo hayo makubwa tuliyonayo ni ukubwa wa fursa tulizonazo kwahiyo tuendelee kuzichangamkia kadiri iwezekanavyo. Kila anayetatua matatizo yanayotuzunguka ndo hivyo hivyo anatengeneza fedha.
 
kitu kingine wakenya sembe wananunua kwenye packaging ya kilo moja na mbili,packaging ya paperbags,means katoni inakuwa ni box,kwa wale walioishi enzii za sokoine watakumbuka unga wa ngano wa kenya ulikuwa unakuja kwenye packaging ya kg mbili,sasa na sembe yao haipakiwi kwenye sandalusi la kg hamsini
 
Nimefuatilia toka vyanzo mbalimbali vya habari naona ngoma ya kuuza unga inogile na Mhe. N/Waziri Bashe amekuwa na vikao vya kuuza unga wa mahindi tani mil 1.
Very good initiative kwa hoja ya kusaga na kufungasha kupitia vinu vya Iringa Mwanza....

So far bado narejea, tujenge uchumi jumuishi unaogusa Watanzania kwa kuuza Kenya unga Kenya.

Watanzania wapewe fursa ya kuyafikisha mahindi kwenye vinu vya kusaga. Watanzania wapewe fursa ya kuwa sehemu ya mnyororo wa thamani wa usindikaji.
Watanzania wapewe fursa ya kusafirisha toka kwenye vinu vya usagishaji mpaka Kenya.

Singapore waliamua kutumia bahari inayowazunguka kujenga bandari na kutengeneza shughuli chungu mzima kwenye mnyororo wa thamani bandarini kama competitive advantage ya kukuza uchumi wao.

Hii dunia hata hao USAID, CIDA, SIDA, DANIDA kuna wakati wanafanya biashara na Tanzania bila kutuhurumia kwa kuuza finished products.
Ni ushauri tu maana ukifuatwa itaongeza mzunguko wa fedha katika Maisha ya watu wa Tanzania
 
Nasisitiza tena, huna pesa mkononi kaa kushoto na mazao yangu, maana sina muda wa kwenda kupangiwa muda wa kupata pesa yangu. Anayetaka kujiunga na chama cha ushirika kwakuwa kina faida kama ulivyosema ni sawa na nitamuunga mkono ila sio mimi.
Kwa hili ninakubaliana nawe moja kwa moja.
Hata ule mfano wa Kenya niliotoa hapo juu, kuna wakulima waliokataa kujiunga katika vyama vya ushirika vilivyoundwa.
 
So far bado narejea, tujenge uchumi jumuishi unaogusa Watanzania kwa kuuza Kenya unga Kenya.
Inashangaza kidogo kwa jambo kama hili nalo kuwa na mjadala kiasi hiki.

Hapa tuna soko la pamoja katika ushirika wetu huu wa EAC; kwa nini tena tuwe na mvutano wa kuuza bidhaa ya aina gani katika soko letu hili?

Inaeleweka popote duniani, kama unaongeza thamani bidhaa yako unayouza unafaidika zaidi. Sasa ni sababu zipi zinazofanya kuongeza thamani katika bidhaa yetu ya mahindi liwe ni tatizo?

Au tunataka kinyume chake? Yaani, Tanzania iuze mahindi Kenya. Wao watengeneze unga, na kwa kuwa soko ni letu sote, hawana kizuizi cha kutuuzia unga huo huo unaotokana na mahindi yetu tuliyowauzia sisi endapo kama kuna ziada baada ya kukidhi mahitaji yao?

Hali naiona kuwa ni hiyo hiyo na mazao mengine, kama pamba. Sisi tunazalisha pamba kwa wingi, tunawauzia wao hiyo pamba wanatengeneza nguo na sisi kununua nguo hizo kwa sababu hatutaki au hatuna uwezo wa kuiongezea pamba yetu thamani. Na hili naliona linakuja kwa haraka sana, kama si msimu huu wa pamba, kuanzia mwakani hali itakuwa ni hiyo hiyo.
Kwa sababu sisi tunapenda sana kusema na kuimba zaidi ya kutekeleza kwa vitendo.
Ngozi za ng'ombe na mbuzi, hali ni hiyo hiyo!
 
Mimi sikubaliani kabisa kuwepo kwa madalali/watu wa kati/walanguzi.

Ila kwenye biashara intermediaries huwa zipo. Kama ambayo una hela unamtumia mtu, kuna bank au mobile money kama mtu kati.

Shauku yangu, warasimishwe ili naoa mfumo uwatambue. Likifanyika kila mmoja ana-win.

Mbona hatuendi kununua Cement Tanga au Mbeya au kokote. Tunanunua kwa retailers ambao nao wananunua kwa wholesalers.

Tukirasimisha mfumo, tunaongeza mzunguko wa fedha katika organized systems.

Ila kama Serikali ikiamua, mimi ni nani kuzuia mambo hayo yasifanyike. Maana jana nimeona moja ya lecture the boss is always right. So far if that is true, I can just advise professionally na sio vinginevyo.
Intermediaries ndiyo madalali bosi...tofauti ni lugha tu...the roles are the same....

Hakuna biashara isiyo na udalali....hata kkoo ukipeleka fuso la nyanya....sharti upite kwa dalali....or else zitakuozea
 
Huenda baadae bashe akachukua nafasi ya mkuu wake yaani akawa ndie waziri kamili..
Ila isipokuwa hivyo ni kutumbuliwa

Uwezekano mkubwa kwa Bashe baadae ni kutumbuliwa tu kwa sababu kaambiwa aende ku "practice theory" zake alizokuwa anazitoa akiwa mjengoni huku akipewa u Naibu Waziri wa kimitego tego kama Mwigulu, Nape or Jm walivyopewa, sasa basi utaona yeye kama naibu waziri automatically haingii kwenye Baraza la Mawaziri ambako maamuzi ya sera ya wizara hufanyika hivyo basi hana uwezo wowote wa kuingiza brabra zake za Bungeni mpaka hapo atakapoambiwa na Boss/waziri wake afanye nini na akienda tofauti na Boss hapo ndipo atakapokumbana na rungu litakalomrudisha Nzega kijiweni
 
Wanabodi,
Naomba ku-declare interest kuwa sina ugomvi binafsi na Naibu Waziri Hussein Bashe.
Nimekuwa namkubali kwa namna ambavyo alikuwa aki-analyse dhana ya mnyororo wa thamani hususan kwenye sekta ya KILIMO kwa michango yake "mjengoni"

Nadhani, sio sawa kutoa ruhusa kwa Wakenya kuingia kwenda kununua mahidi kwa wakulima. Pengine hatuja-set regulations za namna ya kufanya biashara ya mazao mchanganyiko. Jambo hili litutake tujenge mfumo rasmi wa manunuzi ya mazao mchanganyiko. Sio waje kwenda kununua mahindi moja kwa moja kwa wakulima.

Intermediaries wana sehemu yake kwenye biashara kama watasajiliwa. Kwenye bima kuna Brokers, na agents kama intermediaries. Hata bank ni intermediary ambae tukiweka mfumo bora wa mauzo banks zitakuwa na mifumo rasmi ya kugusa wakulima na TRA ana-access ya kodi kuoitia wigo utakaopanuka.

Huwezi kwenda Marekani ukanunua maziwa kwa wakulima then ukapaleka kiwandani wakufanyie packaging halafu usafirishe. Haiko hivyo.

Mhe. Naibu Waziri you can do the best kwa kushirikiana na Mhe. Hasunga na mtengeneza mifumo rasmi ili mahindi yaunuliwe, yakobolewe/kusagwa moja kwa moja na Kenya asubiri mahindi kule kwao. Ikiwa hivyo kwa haraka haraka itaongeza mzunguko wa fedha kwa Watanzania kwa mfumo wa mauzo, ulinzi kwenye maghala, bima za hifadhi kwenye maghala na vyanzo vya ajira kwa kujenga mfumo.

Kama ambavyokwenye madini (hatuuzi raw kwa wageni ili wakachakate makinikia kwenye refineries kwa wageni) na kwenye mahindi tuwe na mfumo wa soko maalum la finished products.

Tukisaga unga kwetu na ku-package sisi ni vema pia tuka-control logistics. Walau sio mbaya Kenya apokee mzigo mpakani kwake ili Magari ya Watanzania yahusike kusafirisha unga uliosindikwa. Hii ina akisi kutoa ajira na kuongeza wigo wa mzunguko nchini hali kadhalika kodi.

Kama ambavyo niliwahi kushauri hapa JF wakati wa zoezi la kupekeka mahindi Zimbabwe na Namibia; tunaposema tunajenga Tanzania ya viwanda kwa kuongeza thamani kwenye mazao ghafi na kupata tija kwa kuuza packaged final product, sasa tufanye kwa vitendo.
Mhe. Hasunga hakuona hiyo fursa, naomba pia mhe Bashe usianze vibaya.

Natoa ushauri mapema kabla mambo hayajaharibika. Kama mtasonga mbele na maamuzi hatuna namna ya kuwazuia ila tuna jukumu la kuwashauri namna gani mfanye vyema. Mnachokifanya kiwe na taswira ya kujenga uchumi na kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.

Mungu Ibariki Tanzania
Mimi huwa nashangaa sana, mkulima alime ajuavyo akivuna sawa/I shall aspovuna atajijua, mazao yakiiva apangiwe. Kwanini hakuna Bima za kilimo ukame na dizasters kibao zinawathiri no body cares.
 
Naunga mkono Juhudi za Mheshimiwa Bashe kuruhusu Mfanyabiashara yoyote duniani kununua mazao ya wakulima wetu.
Jasho la mkulima lazima anufaike nalo.
Serikali inaweza kuingilia kwa sababu za dharura tu na kama ikifanya hivyo lazima icompensate wakulima gharama za kutouza mazao yao.

Kama mkulima atanufaika na mazao yake basi umasikini utapungua kwa kasi
sijawahi ona wazo la kipuuzi kama hili! huko brazil huwa munauziwa miwa mnapeleka viwandani kuchakata sukari?
 
Back
Top Bottom