Leo: Barrack Young Controllers II Vs Azam FC

Leo: Barrack Young Controllers II Vs Azam FC

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
===
Barrack Young Controllers II, Vs Azam FC

Leo ni leo asiye na mwana aleke jiwe' na mtoto atumwi dukani - ni pale marudiano ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam FC ya Tanzania na Barrack Young Controllers II ya Laberia zitakapo shuka uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mechi hii itaanza muda wa saa 10:30 jioni.
Waamuzi wa mechi hii wanatoka Comoro, na
mwamuzi wa mezani (fourth Official) ni Ansudane Soulaimane, kamishna wa mechi ni Abdelhamid Radwan kutoka Misri.

Tukumbuke kuwa katika mechi ya awali iliyofanyika nchini Liberia, Azam FC ilifanikiwa kushinda mchezo huo kwa mbao 2-1, matokeo ambayo yameiweka timu hiyo katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye kombe hilo la Shirikisho.
Watanzania tujumuike pamoja kuwashangilia vijana wetu.
===
Matokeo Ya awali:

17/03 Barrack Young Controllers 2 1 - 2 Azam FC - - - W
03/03 Al Nasir 0 - 5 Azam FC - - - W
16/02 Azam FC 3 - 1 Al Nasir - - - W
 
...sasa ni swala la kufikilia ni timu gani Azam atakumbana nayo kwenye mzunguko unaofuata(iwe ligi style au mtoano) kwa hawa watoto-B.Y.Controllers tayari imeishawavuka
 
kikosi cha Azam
1. Mwadini
2. Himid mao
3. Waziri
4. Atudo
5. Mwantika
6. Baluo
7.kipre
8. Sure boy
9. Bocco
10. Mieno
11. Omony
 
Mpira Taifa umeshaanza....
Azam 0 - 0 Barrack
 
Young wanapata kona...wanaanza kona fupi Azam wanautoa.
 
Azam wamefanya shambulizi hapa...alikua ni Kipre Tchetche, mpira unakuwa goalkick...
 
Rekebisha heading
sio Barrack Vs Azam...

Ni

Azam Vs Barrack
 
Azam wanapata freekick...ni nje kidogo ya 18

Mpira unatoka nje...
 
Azam wanafanya shambulio la nguvu...lahaulaaah Kipre anaotea
 
Azam wanakosa goli la wazi...mpira unaokolewa...lahaulaaa!!!
 
Back
Top Bottom