Leo: Barrack Young Controllers II Vs Azam FC

Leo: Barrack Young Controllers II Vs Azam FC

Mpira ni mapumziko,hakuna goli AZAM 0-0 BYC.
 
Mpira ni mapumziko...
Azam 0 - 0 BYC

Mpira kwa kipindi cha kwanza kilikua kizuri kwa mwanzoni timu zote mbili kusomana.
Baadaye Azam wakaamka na kutengeneza nafasi kadhaa ambazo kama wangezitumia vyema basi wangeliweza kupata bao moja hadi mawili.
Dakika za mwisho tumeshuhudia BYC nao wakizinduka na kuonesha uhai.

Utabiri wangu ni kwamba ninatumai kipindi cha pili tutashuhudia magoli walau mawili.
 
Azam wamefanya mabadiliko...Umony anatoka na Mcha Khamis anaingia nafasi yake.

Kipindi cha pili kinaanza...

Azam 0 - 0 BYC
 
Mcha anafungaga sana kwenye viwanja vya tope...
Azam wamefanya mabadiliko...Umony anatoka na Mcha Khamis anaingia nafasi yake.

Kipindi cha pili kinaanza...

Azam 0 - 0 BYC
 
Dk 55
Azam wanapata kona...wanakosa

Azam 0 - 0 BYC
 
Azam wanakosa goli hapa...kipa wa BYC anafanya kazi yake...
Kona....kipa anadaka!
 
Namna ganiiii...Balou wa Azam anapoteza nafasi ya wazi kabisaaa...lahaulaaa!!
 
Azam wanafanya shambulizi zuri...wanakosa goli
 
Dakika zilizobakia hazimruhusu hata kuku kumeza punje ya mtama...
 
Mpira umekwisha:AZAM 0-0 BYC. Mchezo ulikua mzuri timu zote zimeshambuliana kwa zamu,milango ilikuwa migumu.Hongera Azam kwa hatua inayofuata.kila la Kheri AZAM FC.
 
Mpira umekwisha.
Azam 0 - 0 BYC

Kwa matokeo haya Azam FC wanasonga mbele hatua inayofuata kwa jumla ya mabao mawili (2) dhidi ya bao moja (1) la BYC.

Kati ya tarehe 19,20 au 21 ya mwezi April Azam atarudi tena uwanjani kuikabili FAR Rabat kutoka Morocco.
 
Back
Top Bottom