Lengo lako la kujiunga JF limefanikiwa?

Lengo lako la kujiunga JF limefanikiwa?

Lengo langu kujiunga JF ni kuipambania dini yangu kwa hoja na kuzitupilia mbali upuuzi wa wavaa kobazi.

Kutokana na mambo ya kidini kuwa very sensitive, kuna muda nilighadhabika na kutoleana maneno ya hovyo na wachangiaji wenzangu. Tuliishia kupigwa ban nzito.

Anyway, nje ya ulingo nilijitafakari. Na kuamua kukubali kuwa imani ni jambo binafsi. Mungu wetu ni Mkuu, hapaswi kutetewa. Anajidhihirisha mwenyewe wakati sahihi.

Nikaamua kurudi sasa kwa ajili ya kujifunza mengine, na mambo si haba.

Lengo nililokuja nalo, limebadilishwa na JF.
 
Faida
Ndio nilikoijulia forex back in 2016
Nimefanya sana biashara humu kama kuuza camera na simu.

Hasara
Nikijufuza kubeti Jf na kubeti ndio kulinifelisha 2018 F6 now ningekua Daktari.

But nimejifunza vingi sana humu though
 
Nimekuelewa, lakini kukadiria kitu ambacho taarifa zake unazo au unaweza kuzipata sio jambo zuri sana, hiyo itakusaidua huko mbele ya safari.

Nikimuuliza kwanini umepata muda wa kuandika vizuri bandiko refu na ukakosa muda wa kuangalia profile Yako ulijiunga lini ukaamua kukadiria utakua nayo?

Tukirudi kwenye hoja ya msingi, nilijiunga JF niweze kupata mambo mbali mbali yanayojiri hapa kwetu na duniani Kwa ujumla. Lakini pia niweze kutoa maoni yangu na kushiriki mijadala mbali mbali. Mwisho JF ni burudani tosha kwangu na sehem ya kutoa stress kwa kusoma maoni ya wanachama.
Nilijaribu kuangalia nilijiunga lini ila sikufanikiwa kuona ndio maana nikafanya makadirio tu, uenda ni ushamba au labda hii app ninayoitumia maana kuna baadhi ya vitu nashindwa tofauti na ile ya zamani. Kuna muda picha hazifunguki, ku-quote kipande cha andiko la mtu siwezi na pia sipati notifications za reply, likes na comment ambazo wengine wamenitag hata user name ya Natafuta Ajira nimejaribu kuibadilisha lakini nashindwa
 
Umeeleweka Mkuu.
Connection hua zinaanzia mbali sana, na usiweke mbele connection au maslahi Yako Kila unapokutana na mtu, itatokea yenyewe. Kuwa binadamu kwanza, mtaendana na mtu Kisha katika kufahamiana zaidi ndio mambo mengine yatajitokeza. Kumbuka inachukua muda mtu kukyamini hadi akushirikushe mambo ya muhimu hasa Kwa enzi hizi zilizojaa ulaghai mwingi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom