Lengo la kuanzishwa mabasi ya mwendokasi

lingamba lidodi

JF-Expert Member
Nov 15, 2018
964
1,137
Wana bodi saalam!
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi,juu ya mradi huu wa mabasi ya mwendokasi bila kupata majibu sahihi.
1.serikali ilikusudi kuondoa foleni jijini DSM ili kuharakisha safari kwa wananchi,au kwa viongozi na wanaomiliki usafiri binafsi?

2. Kuondoa kero ya kujazana kweli zilizokuwa daladala huko nyuma?

3,Kuondoa kero ya wasafiri kukaa muda mrefu kwenye vituko vya daladala?nk

Kwanini nimekuuliza maswali haya!
1,Nimeona siyo Mara moja watu wakihairisha safari wakiwa vituoni kwasababu ya kukaa muda mrefu kusubiri mabasi ya MWENDO kasi.

2,Ili usafiri na mabasi ya MWENDO kasi ni lazima uagane na nyonga.
Mabasi haya yanaza watu hata Nguruwe hupakiwa kwa idadi kwenye mafuso.
Ukivaa suti usiende kupanda haya mabasi utaondoa ustaarabu wote wa suti.
Karibuni tujadiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom