Lengai Ole Sabaya kuwa huru?

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,775
15,256
Mh rais Samia, sisi wana CCM tunakuomba kama ulivyoguswa na maombi ya watu mbalimbali ya kutaka umwachie mwenyekiti wa Chadema Mbowe anayetuhumiwa kwa tuhuma nzito za ugaidi na kupanga njama za kuuwa viongozi wa serikali basi tunakuomba pia uguswe na umwachie aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, kwani kusameheana kupo.

Kwenye mizani Sabaya na Mbowe wote ni wafungwa wa kisiasa na tuhuma za Mbowe ni nzito sana na ushahidi wake umetolewa na watu wakubwa ambao ni viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama lakini tuhuma za Sabaya ni nyepesi sana na ushahidi unatolewa na watu ambao tangu mwanzo wanajulikana wana chuki na Sabaya, Wengine wametamba waziwazi kwenye mabaa kuwa lazima wamkomeshe huyo kijana.

Mh rais haiwezekani ukubali kuingilia uhuru wa mahakama na kumsamehe mwana Chadema Mbowe alafu ukamuacha kijana na mtoto wako na mwana ccm mwenzako Sabaya akiteseka kwa tuhuma za uongo na uzushi alizotungiwa na wakwepa kodi na wauza madawa ya kulevya wa wilaya ya Hai.

Ni kweli Chadema na wapinzani wengi wameshangilia sana kifungo cha Lengai Ole Sabaya cha miaka 30 jela lakini ukweli ambao hausemwi ni kwamba wana ccm wengi wamehuzunishwa na kuchukizwa mno na kifungo cha Sabaya.

Kwenye macho ya wazalendo wa nchi hii, Sabaya ni mzalendo wa kweli aliyejitoa kuleta mabadiliko kwa vitendo na siyo maneno kama wanavyofanya wengi.

Bila Lengai Ole Sabaya kuwa mkuu wa wilaya ya Hai haya yangeweza kutokea kwenye wilaya hii.

1. Wilaya ya Hai kupanda kwa ukusanyaji mapato kutoka ya mwisho hadi kuwa ya nne kitaifa. Kabla ya Sabaya wilaya hii ilikuwa imekithiri kwa rushwa na ukwepaji kodi.

2. Mbunge na madiwani wa ccm kushinda na kuongoza Halmashauri
Wilaya hii ilikuwa ngome ya Chadema kwa miaka mingi na kila aliyejaribu alikiona cha mtema kuni kutoka kwa Mbowe na genge lake. Lakini kupitia Sabaya sasa jimbo la Hai ni ngome ya ccm na itawachukua miaka mingi Chadema kulirudisha tena hasa baada ya Mbowe kuwa gaidi na kupoteza imani kwa wananchi wengi.
Lakini pia Mbowe ametangaza kuachana na siasa za majukwaani.

Kwa kifupi mbunge ,madiwani na wenyeviti mbalimbali wa wilaya ya Hai wanakula kupitia jasho la Sabaya.

3. Kurejeshwa kwa ardhi ya waislamu iliyoporwa kwa miaka mingi.
Wilaya ya Hai wamepita wakuu wa wilaya wengi lakini hakuna aliyefanikiwa kumaliza mgogoro huo mpaka Lengai Ole Sabaya alipofika na kumaliza kadhia hiyo.
 
Mama unapomfanyia mtu jambo fulani fanya kwa haki kwasababu haujui kesho ya mtu..kumbuka Sabaya ni kijana mdogo tena anayependwa na CCM
 
Maadamu ni ccm haiwezi kaa jela mda mrefu atatafutiwa kifungu cha kumchomoa
 
Maadamu ni ccm haiwezi kaa jela mda mrefu atatafutiwa kifungu cha kumchomoa
sawa lakini ndoo kanyea sana na manundu atatoka nayo tayari nundu moja tushaiona
1658999278820.png
 
malipo ni hapa hapa duniani. hata wewe kwa maandishi haya ya uchochezi na chuki dhidi ya mbowe malipo yako utayapata hapa hapa duniani. jifunze kwa wapumbavu wenzio. sabaya alionywa ila hakusikia!
 
Hitler alifanya mambo makubwa na mazuri kwa wajerumani, alitoa nchi kwenye mdololo wa uchumi na akaimbwa sana sana. Akaona atumie 'mazuri' yake kufanya mabaya na kujificha kwenye kichaka cha 'mazuri'.

Huwa ni utaratibu wa viongozi kutumia mazuri machache kujificha kufanya mabaya ya kuogopesha.

Mobotu alitumia mazuri machache ya kijijini kwao kujificha kufanya mabaya.

Makonda pia yeye hadi akaanza kulia lia mitandaoni humu akituma clips za kusaidia walemavu akipinga tuhuma za mabaya yake.

Hivyo ni hulka yao, hufanya mabaya na kutumia kujifichia kwenye mazuri machache.
 
Back
Top Bottom