Lembeli awashangaa wanaoponda maandamano na migomo

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
mbunge wa kahama james lembeli amewashangaawabunge wanao jadili na kunyoosheana vidole juu ya maandamano na migomo inayoendelea hapanchini na kusema tanzania sio kisiwa kwa kuwa maandamano na migomo vinatokea duniani kote. Lembeli amesema migomo ilikuwepo angu enzi za mwalimu na kuna watu waliochapwa viboko lakini leo hii wako bungeni na ni viongozi safi. Amesema inasikitisha kuona wanafunzi wanapanga msitari kwa zaidi ya masaa matatu halafu wakiingia benki wanaambiwa pesa hazijaingia. Katika mazingira kama hayo lembeli amesema hata kama angekuwa yeye asingekaa kimya angelalamika hivyo serrikali inapaswa kuhakikisha wanafunzi wanaostahili mkopo wanapatiwa mikopo yao kwa wakati ili kuepusha migomo na maandamano. Amewataka wabunge wache kujadili masuala hayo kwa kua sio kitu kigeni.<br><br>source: bungeni dodoma.
 
Safi sana Lembeli hamia CDM manake ndio wenye kauli nzuri kama hizo.

Naona kama wabunge toka Shinyanga wana-mix up kambi vile! Shibuda anapingana na chama chake CDM, Lembeli naye anaonekana kutofautina na chama chake CCM. Mbowe na Pinda - fanyeni barter trade!
 
Duh! Kweli watu wameamka, yaani huyu mh. alikuwa anakaa kimya mjengoni kama vile hana wajibu. Hongera sana Lembeli kwa kutambua wajibu wako endelea mkuu maana hao wenzako bila kuwachana laivu hawasikii. Usiishie kwenye maandamano tu fanya hima wananchi wako wapate barabara za ukweli sio kuwaacha na vumbi. Ishinikize serikali ijenge shule za A level watoto wasome. Bado una jukumu kubwa sana kahama haistahili kuwa hivyo hasa ukizingatia uchumi wake upo juu sana kuanzia kwenye sekta ya madini mpaka biashara.
 
Kwani madini ni mali ya watu wa Kahama au Canada? Uchumi wa Kahama si madini labda mchele! mkuu wangu. Madini Mungu aliyaweka Kahama kwa bahati mbaya. Ni milki ya wakanada na waingereza!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom