Lembeli aunga mkono migomo/maandamano.

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Mbunge wa kahama james lembeli ameunga mkono migomo na maandamano vinavyoendelea hapa nchini kwa kudai kuwa tanzania sio kisiwa kwa kuwa migomo na maandamano vinatokea pote duniani. Lembeli pia amesema migomo ilikuwepo tangu enzi za mwalimu na kuna watu ambao walichapwa viboko ambao leo hii ni wabunge. Pia kasema inasikitisha wanafunzi wanapanga foleni kwenye benk masaa matatu halafu wakiingia ndani wanaambiwa pesa hazijaingia, katika hali kama hii ni vigumu kwa wanafunzi kukaa kimya hata angekuwa yeye angelalamika. Ameitaka serikali itoe mikopo kwa wakati ili kuepusha migomo. Lembeli pia amewataka wabunge kuacha kujadili mambo ya migomo na maandamano bungeni badala yake waielekeze nini cha kufanya kuliko kunyoosheana vidole. Source: bungeni dodoma.
 
Kaongea point!! wabunge wanatakiwa kuacha ushabiki wa kichama otherwise watakuwa wanaviua vyama vyao. Vitu viko wazi, lakini unakuta jitu from no where linapinga maandamano bila kujua source nini!!
 
Ni ajabu nchi hii. Maandamano ya amani huwatisha sana viongozi wetu. Mpaka sasa sijawahi kujua kwa nini viongozi wetu huyaogopa wakati wale wanaoandamana na kuyaongoza wameahidi kuwa yatakuwa peaceful. Badala ya kuandika au kulalama chini chini watu huweza kutoa maoni yao kwa njia hiyo. Viongozi wanaoyaogopa maandamano wana lao jambo.
 
Sasa kuweka post thread nane zenye kichwa cha habari cha aina moja ndo nini hii au unataka uongeze post zako, acheni uzembe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom