Lembeli aishangaa serikali kuilipa Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lembeli aishangaa serikali kuilipa Dowans

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 18, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli, amesema anaishangaa serikali kuibuka na kuelezea hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Migogoro ya Biashara (ICC) kwamba, imeliamuru Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kuilipa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited mabilioni ya shilingi.
  Amesema hukumu hiyo ina utata na imezua mkanganyiko mkubwa miongoni mwa Watanzania kwani hajawahi katika maisha yake kupata kusikia serikali ikiwaeleza wananchi kwamba, Dowans Tanzania Limited imeishtaki Tanesco mahakamani. Lembeli aliyasema hayo jana alipozungumza na NIPASHE jijini hapa kuhusiana na sakata la malipo kwa Dowans Tanzania Limited.
  Alisema serikali makini lazima iwaarifu watu mapema mambo ya kitaifa yatakayowakabili ili baadaye kusiwe na maswali, kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu Julius Nyerere.
  Alisema kinachotokea sasa ni cha kusikitisha kuona viongozi wa serikali, wanatoa kauli tofauti kuhusu Dowans, hali inayomfanya mwananchi wa kawaida kuzidi kuchanganyikiwa, maana anashindwa ashike la nani na kuacha lipi.
  “Utasikia mara kampuni hii feki, mara vigogo wa serikali wanahusika na serikali imekaa kimya bila ufafanuzi. Jambo hilo ni baya na linaleta mkanganyiko kwa jamii,” alisisitiza Lembeli.
  Alisema kwa mfano kwenye suala la mgawo wa umeme, waziri husika aliutangazia umma kwamba, mgawo umekwisha, lakini baadaye lilipotokea tatizo, hakueleza kilichosababisha tatizo hilo kuendelea kinyemela na kusema jambo hilo linazidi kuchafua serikali na watu wake.
  Kuhusu bei za gesi, alisema nayo hivyo hivyo, serikali imekaa kimya, badala ya kuwaeleza wananchi sababu za kupanda kwa nishati hiyo, huku wananchi wakilalamika kwamba, hawapewi majibu sahihi.
  Alisema kitendo cha serikali kuendelea kukalia kimya masuala mazito ya taifa, ni cha hatari kwa siku za usoni, kwani kinaweza kusababissha mvurugano usio na sababu.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. WAKUNJOMBE

  WAKUNJOMBE JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Asante mzee...........

  ila mi ninahii dowans.............

  kwaupeo wangu mdogo ckampuni inapoishitaka serikali lazima wadau tutamjua mwanasheria wa hiyo kampuni............msemaji wa kampuni..........pia ukitaka kujua zaidi hata board members wa hiyo kampuni utawajua........

  kinacho nishangaza hapa muongeaji wa kampuni ni membe na serikali yake.........sasa tunamlipa nani?
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  yeah inamaana anaelipwa ni nani sasa maana wahusika wa kampuni hatuwajui na kesi imeenda kimyakimya na malipo basi wangelipa wenyewe kimyakimya!
   
Loading...