Lema: Ukimya wa Polisi kwenye mapokezi ya Lisu ni Chroloquine iliyopakwa sukari, kuna jambo linafikiriwa

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema ameonya wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ukimya ulioonyeshwa na jeshi la polisi jana wakati wa mapokezi ya makamu wa mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu alipowasili nchini.

Lema ameonya hayo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, amesema wapinzani wanapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wa kawaida.

“Sina amani kwa tabia nzuri walioonyesha Jeshi la Polisi jana wakati wa mapokezi ya Mh Tundu Lissu. Ninapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wengi, ninaona ni kama chloroquine imepakwa sukari, kuna kitu kinafikiriwa na sisi tunapaswa kufikiri zaidi” ameandika Lema.

Hapo jana Julai 27, 2020 mamia ya wanachama wa chama hicho wamejitokeza kwa wingi kumlaki makamu mwenyekiti wao, Tundu Lissu aliyerejea nchini baada ya miaka mitatu ya kupatiwa matibabu nchini Ubeligiji.
Kwa mara ya kwanza nawapongeza sn jeshi la polisi
 
Mmeanza kuweweseka!

CCM inapenda kuona Tundu Lisu anateuliwa kuwa mgombea urais!

Ccm kama chama inaweza kuwa inapenda, lakini Magufuli hapendi wala hataki. Na kimsingi hakuna ccm, bali kuna Magufuli, na chama kiitwacho ccm kinachotembelea madaraka ya Magufuli kufanya siasa. Na Magufuli ndio final say. Kama alitaka atangazwe kwa kura 100% na akapitishwa kweli, atashindwa kupanga mshindani amtakaye?
 
Lema anajaribu kutengeneza taswira kwamba "kuwa mpinzani lazima utendewe mabaya sikuzote", and anasahau kufikiri kwamba yawezekana police waliamua ku withdraw baada ya kugundua kwamba nguvu ya uma/umati mkubwa ulio jitokeza kumpokea Lisu ulikua ni mkubwa hata kuzidi nguvu ilio andaliwa.

Hajaribu kujenga taswira yoyote, bali hiyo ndio hali halisi.
 
Lema, wewe furahi kuwa sasa Lisu yupo home. Mambo ya kwanini hukupigwa yasikusumbue bali mshukuru Mungu kuwa weye bado unapumua ya kesho mwachie Mungu. Panga mipango ya kesho kama kwamba upo kesho tiyari
 
Lema anajaribu kutengeneza taswira kwamba "kuwa mpinzani lazima utendewe mabaya sikuzote", and anasahau kufikiri kwamba yawezekana police waliamua ku withdraw baada ya kugundua kwamba nguvu ya uma/umati mkubwa ulio jitokeza kumpokea Lisu ulikua ni mkubwa hata kuzidi nguvu ilio andaliwa.
Hivi tokea hapo kuna mpinzani ambaye hajatendwa ndani ya miaka 5 hii?
 
Polisi na Rais waliwaacha muandamane na mjipime kama mko sahihi
 
Attachments

  • Screenshot_20200728-161228.png
    Screenshot_20200728-161228.png
    89.8 KB · Views: 1
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema ameonya wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ukimya ulioonyeshwa na jeshi la polisi jana wakati wa mapokezi ya makamu wa mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu alipowasili nchini.

Lema ameonya hayo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, amesema wapinzani wanapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wa kawaida.

“Sina amani kwa tabia nzuri walioonyesha Jeshi la Polisi jana wakati wa mapokezi ya Mh Tundu Lissu. Ninapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wengi, ninaona ni kama chloroquine imepakwa sukari, kuna kitu kinafikiriwa na sisi tunapaswa kufikiri zaidi” ameandika Lema.

Hapo jana Julai 27, 2020 mamia ya wanachama wa chama hicho wamejitokeza kwa wingi kumlaki makamu mwenyekiti wao, Tundu Lissu aliyerejea nchini baada ya miaka mitatu ya kupatiwa matibabu nchini Ubeligiji.

Kwahiyo walijiandaa kwa vurugu, ilipokosekana anaona mapokezi hayakunoga AU?

Badala ya kuwasifu Polisi wamefanya kazi yao ya kuhakikisha usalama wao na mali zao, anawatafutia mabaya.

Mabibi na Mabwana, Huyu ndo waziri kivuli wa mambo ya ndani.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema ameonya wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ukimya ulioonyeshwa na jeshi la polisi jana wakati wa mapokezi ya makamu wa mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu alipowasili nchini.

Lema ameonya hayo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, amesema wapinzani wanapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wa kawaida.

“Sina amani kwa tabia nzuri walioonyesha Jeshi la Polisi jana wakati wa mapokezi ya Mh Tundu Lissu. Ninapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wengi, ninaona ni kama chloroquine imepakwa sukari, kuna kitu kinafikiriwa na sisi tunapaswa kufikiri zaidi” ameandika Lema.

Hapo jana Julai 27, 2020 mamia ya wanachama wa chama hicho wamejitokeza kwa wingi kumlaki makamu mwenyekiti wao, Tundu Lissu aliyerejea nchini baada ya miaka mitatu ya kupatiwa matibabu nchini Ubeligiji.

Lema

Mnatakiwa mtoe press release ya kulishukuru jeshi la polisi na serikali yake kuwapa heshima kubwa ya kumpokea Tundu..
Washukuruni kwa hilo. Na muwakumbushe kwamba haku ua hata sisimizi..
 
Hatari sana upinzani wa bongo,mkipigwa mnalalamika mmeachwa mnalalamika mxhiuuu mnachekesha sana
 
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema ameonya wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ukimya ulioonyeshwa na jeshi la polisi jana wakati wa mapokezi ya makamu wa mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu alipowasili nchini.

Lema ameonya hayo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, amesema wapinzani wanapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wa kawaida.

“Sina amani kwa tabia nzuri walioonyesha Jeshi la Polisi jana wakati wa mapokezi ya Mh Tundu Lissu. Ninapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wengi, ninaona ni kama chloroquine imepakwa sukari, kuna kitu kinafikiriwa na sisi tunapaswa kufikiri zaidi” ameandika Lema.

Hapo jana Julai 27, 2020 mamia ya wanachama wa chama hicho wamejitokeza kwa wingi kumlaki makamu mwenyekiti wao, Tundu Lissu aliyerejea nchini baada ya miaka mitatu ya kupatiwa matibabu nchini Ubeligiji.

Asijekuwa anataka kutengeneza tukio maana nae na boss wake ni watuhumiwa
 
Back
Top Bottom