Lema: Ukimya wa Polisi kwenye mapokezi ya Lisu ni Chroloquine iliyopakwa sukari, kuna jambo linafikiriwa

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,989
2,000
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema ameonya wanachama na wapenzi wa chama hicho juu ya ukimya ulioonyeshwa na jeshi la polisi jana wakati wa mapokezi ya makamu wa mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu alipowasili nchini.

Lema ameonya hayo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, amesema wapinzani wanapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wa kawaida.

“Sina amani kwa tabia nzuri walioonyesha Jeshi la Polisi jana wakati wa mapokezi ya Mh Tundu Lissu. Ninapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wengi, ninaona ni kama chloroquine imepakwa sukari, kuna kitu kinafikiriwa na sisi tunapaswa kufikiri zaidi” ameandika Lema.

Hapo jana Julai 27, 2020 mamia ya wanachama wa chama hicho wamejitokeza kwa wingi kumlaki makamu mwenyekiti wao, Tundu Lissu aliyerejea nchini baada ya miaka mitatu ya kupatiwa matibabu nchini Ubeligiji.

Lema.jpg
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
27,003
2,000
Lema anajaribu kutengeneza taswira kwamba "kuwa mpinzani lazima utendewe mabaya sikuzote", and anasahau kufikiri kwamba yawezekana police waliamua ku withdraw baada ya kugundua kwamba nguvu ya uma/umati mkubwa ulio jitokeza kumpokea Lisu ulikua ni mkubwa hata kuzidi nguvu ilio andaliwa.
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
7,862
2,000
Chloroquine iliandaliwa kwa ajili ya kuuwa (sumu), lkn accidentally ikabainika kiwa inaponya malaria.

Kwahiyo hao ccm acha waandao maovu yatakayogeuka kuwa kete ya ushindi kwa chadema. Kilichopangwa na Mola binadamu kamwe hawezi kukipindua.
 

kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,597
2,000
Mmeanza kuweweseka!

CCM inapenda kuona Tundu Lisu anateuliwa kuwa mgombea urais!
Acha unafiki mkuu, mataga hawapendi hata kusikia lissu yupo nchini achilia mbali kugombea, we ona Leo wamekatazwa hata kwenda kuaga mwili Wa mkapa, mataga sio watu ni mashetani flani kiaina!
 

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,875
2,000
Polisi inabidi wajieleze kwa nini waliacha jukumu la kutoa ulinzi jana.

Tushukuru kwamba hakukutokea rabsha zozote ila ki ukweli Polisi hawakutekeleza wajibu wao siku ya jana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom