Lema: Tutapokea kigogo wa CCM

Lema: Tutapokea kigogo wa CCM

Wakimpokea el watakuwa wameingia kwenye mtego wa ccm. ...
 
lowasa akitua ili watu wamuelewe aanze kwanza na siri ya Richmond kilichofanya hawe kimya adi leo atakua amemaliza kazi.
 
Tunapenda sana mabadiriko ila kama yataletwa na Lowassa nina wasiwasi itakuwa mabadiriko hasi. Tutakuwa tunautangazia UMMA kuwa shida yetu sio kuleta ukombozi bali nasi tunatafuta kujaza matumbo yetu tu! Hii itakuwa ni zaidi ya usaliti kwa watanzania na sijui kama haitatugeukia
 
Lema tubia kwa mungu kuwaita watu mafisadi na leo unawapigia magoti waje chadema.siasa za bongo ni maslahi binafsi
 
Kama chadema wamefika hatua ya kumwalika lowasa kwenye chama chao, basi ni hatari. Kwa lugha nyingine wanamualika chenge, rostam na wengine wa aina hiyo! Watakuwa ni wapumbavu, binafsi nakatishwa tamaa na siasa za bongo hasa ninaposikia kuwa sasa lowasa ni mbeba bendera wa chadema. Sasa baada ya uchaguzi watatuambia kuwa wanapinga ufisadi?
Kupinga ufisadi ,yeeees...why not?!?.....whatever the case hakuna mtu aliyezaliwa fisadi so if one has proof let him/her come forward,otherwise hizo zinabakia kuwa kelele tu
 
What we want is change of the system because this is what shapes the individuals....napingana na JKN hapa MABADILIKO HAYAWEZI KULETWA NA MTU ALIYE BADO NDANI YA CCM....mabadiliko hayawezi kuletwa na CCM
 
Tunapenda sana mabadiriko ila kama yataletwa na Lowassa nina wasiwasi itakuwa mabadiriko hasi. Tutakuwa tunautangazia UMMA kuwa shida yetu sio kuleta ukombozi bali nasi tunatafuta kujaza matumbo yetu tu! Hii itakuwa ni zaidi ya usaliti kwa watanzania na sijui kama haitatugeukia
Usaliti kwa watanzania?...watanzania gani hao?..wale walokuwa wakimpokea maelfu kwa maelfu kila alipokuwa akienda?
 
Lema huwa hasemi uongo!hebu tusubiri tuone.
 
Watanzania wote majizi tu, ndio maana wanamfurahia mwizi mwenzao Lowassa. Tanzania, kazi kweli kweli!!
 
Mbunge wa Arusha Mjini,Godblees Lema, amesema watapokea "kigogo mkubwa" kutoka CCM pamoja na wenyeviti wa mikoa na wilaya katika mkutano utakaofanyika Dar-es-salaam.

Mkutano huo utafanyika wiki ijayo kwa mujibu wa taarifa hiyo.


Chanzo: Mtanzania

CCM mwaka huu lazima mtafute mchawi wakati mchawi/wachawi mlicheza nao mziki pale ukumbini.

Nami nafikiri kwa kuwa habari hizi zimeletwa na Lema mwenyewe sasa yeye na uongozi wa juu wa chadema akiwemo m/kiti Freeman Mowe katibu mkuu dr. W Slaa watufahamishe yafuatayo kwanza.

(1) Wengi tunaelewa kuwa Edward Lowassa anaejulikana kwa wengi kama fisadi hana ufisadi ulio wazi kwa kiasi cha hela iwe ameisababishia serikali au yeye mwenyewe kuzichota serikalini. Kama ni hiyo richmond wanayoiimba kila leo haikuwahi kulipwa hata senti moja na serikali kwani haikuwahi kuzalisha umeme na kuiuzia serikali.Kwa maana hiyo Lowassa asingeweza kufaidika na richmond wakati haikuwahi kulipwa.

(2) Lowassa aliwajibika kisiasa kwa kuwa yeye kama mtendaji mkuu wa shughuli za serikali alizembea hivyo serikali kuingia mkataba na kampuni isiyokuwa na uwezo.Lowassa baada ya mkataba kufungwa na kupokea taarifa nyingi kuwa kampuni hiyo haikua na uwezo wa kutekeleza ule mkataba nae alifanya uchunguzi na kugundua kampuni haikuwa na mtaji,utaalamu wa kuzalisha umeme na hata ofisi inayotambulika. Alipojiridhisha ukweli wa zile taarifa alimpigia simu raisi aliekuwa nje na kumweleza nia yake ya kuvunja ule mkataba wa richmond alimwagiza kumsubiri arudi. Aliporudi na kuisoma ile ripoti alimwagiza kuuvunja mkataba. Ukumbuke Lowassa kabla ya kuwa waziri mkuu alikuwa Dawasco ambako nako aliwahi kuvunja mikataba ya kifisaidi na kuliokolea taifa mabillion ya fedha.

(3) Kamati iliyoundwa na bunge kuchunguza sakata la richmond kama kuna hela za serikali zilizopotea ikiongozwa na Harison Mwakyembe ilikuwa na wajumbe wengi wakiwepo takukuru na usalama wa taifa pia. Spika akiwa Samwel Sitta. Katika uchunguzi wao hawakuona ufisadi zaidi ya kukiukwa tu taratibu. Mwisho walimshauri waziri mkuu achague kubakia na nafasi yake au kuwajibika kisiasa. Lowassa nae ni jembe na anaona mbali akajiuliza hii kamati ni kwanini hawakwenda kumhoji wakati wote wa uchunguzi hadi kukadhi taarifa bungeni na wakati hakuwahi kusafiri wakati wote huo? Pia ujue nao takukuru walikuwa wameshaagizwa na bunge kuchunguza suala hilohilo na uhusika wa Lowassa na mkurugenzi wao kutoa taarifa kuwa hakuna hasara iliyosababishwa kwa serikali lakini bado tume ikaundwa. Sasa baada ya Lowassa kutafakari akaona pengine wapo wanaoitaka nafasi yake na ndipo alipojiuzulu kisiasa kama walivyowahi kufanya raisi mataafu Mwinyi akiwa waziri mambo ya ndani na bado akaja kuwa raisi baadae.

(4) Sasa ninachotaka kukijua kwa hao viongozi wa chadema ni hiki endapo atajiunga Lowassa chadema anaingia kama mwanachama kwanza au anaingia na kupewa nafasi ya kugombea uraisi mara moja? Sikatai huyu mheshimiwa ana nguvu kubwa ya ushawishi, uwezo mkubwa wa kuongoza na anaijua nchi hii vilivyo. Pia ana nyota ya kupendwa. Pia nakubali kabisa ataingia na idadi kubwa ya wanachama, wabunge wanaochagulika na idadi kubwa ya madiwani wengi sana.

(5) Ikiwa atapeperusha na bendera ya uraisi ina maana na uenyekiti wa chama atakuwa nao pia? Au chama kitatenganisha hizi kofia.Lowassa anao marafiki wengi wazuri na wabaya. Wengine wamehusishwa hata kwenye ukwapuaji wa hela za escrow je kwa kisingizio tu cha kumfuata Lowassa nao kutaka kujiunga chadema mtathibitije hilo kama hata uenyekiri mtamkabidhi? Hapo ndipo ninapoiona logic ya Act kumweka m/kiti mkuu kudhibiti mwenendo wa chama. Madaraka makubwa ya raisi mtakuwa mmeyapunguza? Je mikataba mikubwa ya nchi na nchi, nchi na makampuni makubwa ya nje mliyokuwa mnaipigia kelele miaka yote mtaipeleka bungeni kupitishwa kwanza? Vyama vyote ndani ya ukawa mkikubaliana wote kumpitisha Lowassa hata kama hamtashinda uchaguzi mkuu itawabidi mkae chini muunde katiba itakayowaongoza na kutamka haki za kila chama kishiriki na kusajili rasmi jina la umoja isiwe kama ilivyo sasa mnaanza kuulizana juu ya mgao wa ruzuku. Sasa kwa Lowassa ikiwa hatashinda uchaguzi atakuwa na cheo gani chadema? Ikiwa atakuwa m/kiti Mbowe atapewa cheo gani? Naomba kuelimishwa.
 
safari inaendelea tulikua tunachimba dawa kidogo sasa tupo tayari njoo dereva huondoe gari
 
geraldkowero1,

Umejaribu kujenga hoja, kwani nani alikuambia kuwa chadema kuwa mgombea urais ni kiongozi mkuu wa chama?
 
nilikuwa simpendi lawasa nikatake time zilivyokuwa richmond na misiona failed ya kutaka kusema ukweli wake wote baada ya kuwa rais
 
Lowasa ndani ya Ukawa...Nchi itatikisika ...Simba wa Yuda ataunguruma muda si mrefu
Ndoorobo!!!!!!!!!Lowassa fisadi mkubwa halafu bado anadai eti anausaka utajiri kudhihirisha jinsi alivyo fisadi asiyeridhika na utajiri aliyopata kwa kuhujumu Mali ya wananchi tangu awe waziri 1991
 
Rais Dr Slaa, waziri mkuu Lowasa.

Naunga mkonyo hoja 100%
 
Atapita tena nchi nzima akimpigia debe mgombea wa chadema. CCM mtapoteana!
 
Back
Top Bottom