Lema: Nilitarajia kupokea kipigo kutoka kwa polisi Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema: Nilitarajia kupokea kipigo kutoka kwa polisi Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Dec 20, 2010.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Dec 20, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amedai kipigo alichokipata kutoka kwa Jeshi la Polisi mkoani hapa, wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mombeji, ni matokeo aliyotarajia kutoka kwa Jeshi hilo siku nyingi, lakini hatarudi nyuma kudai haki za msingi na yuko tayari kufa.

  Lema alipata ‘kibano’ kutoka kwa polisi na kusekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi kwa madai ya kufanya vurugu ndani ya Ukumbi wa Manispaa wakati madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakifanya uchaguzi wa kumchagua Meya wa Jiji la Arusha.

  Akizungumza jana mjini hapa, Lema alidai ni siku nyingi OCD Mombeji alikuwa akimtafuta na alishawahi kumtamkia kuwa iko siku ataingia katika ‘anga zake’, hivyo kipigo alichopata juzi kutoka kwa Mkuu huyo wa Polisi Wilaya pamoja na askari wake, ni matokeo ya ahadi alizokuwa ameahidi kumshughulikia.

  Alisema yuko tayari kufa kwa ajili ya kudai haki ya msingi ya wananchi wa Jimbo la Arusha kwa kuhakikisha Meya anachaguliwa kwa kufuata haki na kanuni za uchaguzi za halmashauri zilizowekwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi na sio kupindisha kama walivyofanya juzi.

  Alisema kanuni ziko wazi katika suala la akidi, Kifungu cha 8(3) kinaeleza bayana kuwa uchaguzi utafanyika kwa wajumbe (madiwani) kufika theluthi mbili na hilo ndilo tatizo kwa CCM wako 17 pamoja na diwani wa TLP, lakini sheria inakinzana na hilo na ili uchaguzi ufanyike lazima kuwe na wajumbe zaidi ya 21.

  Lema alisema hawezi kumtambua wala kumuunga mkono Meya aliyechaguliwa na CCM, Gaudence Lyimo pamoja na Naibu Meya wake wa chama cha TLP, Michael Kivuyo, kwani hawakuchaguliwa kihalali.

  “Kesho (leo) tutaonana na wanasheria wa Chadema kuangalia hatua gani za kisheria zichukuliwe juu ya kumpinga meya huyo katika vyombo vya sheria na pia tutautangazia umma kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomi Changah anapaswa kulaaniwa kwa kukiuka sheria kwa makusudi,” alisema mbunge huyo.

  Akizungumzia kitendo cha Kivuyo kuwaacha solemba dakika za mwisho, alisema kinapaswa kulaaniwa na kuwataka wakazi wa Kata ya Sokoni One kumjua kwa kina diwani wao, aliyedai ameanza kazi kwa usaliti.

  Lema alisema Kivuyo ni msaliti wa kupindukia na anapaswa kuelezwa kwa umma ni namna gani alivyoamua kufanya umafia katika dakika za mwisho na kukimbilia CCM na kuambulia kupewa Unaibu Meya.

  Alisema Chadema katika Uchaguzi Mkuu iliamua kwa makusudi kutosimamisha mgombea katika kata hiyo kwa kumheshimu kuwa ni mpinzani wa kweli na anapaswa kuungwa mkono “kumbe tulibeba chatu ndani ya gunia.”

  Kwa upande wake, Kivuyo akizungumza kwa simu, alisema Chadema wamepagawa na hawajui wanaloongea kwani kwenda kwake katika ukumbi na CCM kumchagua, sio kwamba amesaliti chama hicho.

  Kivuyo alisema kinachopaswa kufanywa na Chadema ni kufuata taratibu za kisheria na sio kuleta vurugu na kutuhumiana kwani huo sio wakati muafaka kwa sasa.

  Alisema kanuni ziko wazi na hata kipofu anajua hilo na kinachopaswa kufanywa na Chadema ni kwenda katika vyombo vya sheria na sio kuleta vurugu na kupayuka ovyo barabarani.

  ‘’Meya amechaguliwa kinyume na kanuni na hata mimi nimechaguliwa kinyume na kanuni sasa Chadema wanalia nini? Sheria si ziko wazi, mahakama zipo kwa ajili ya watu wafuate taratibu kudai haki zao za msingi na sio kulaumu watu eti nimenunuliwa?” alisema Diwani huyo wa Sokoni One.
   
 2. c

  collezione JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  i hate CCM,
  hawa watu ni mataira
   
 3. D

  DENYO JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  MIMI NINAAMINI WEWE MUYA NDIO NEGATIVE MINDED PERSON WITH VERY LITTLE THINKING -TRY TO OPEN UP YOUR THINKING CAPACITY -AND THINK OUTSIDE THE BOX, TALK THE FACTS
  1. ccm walizimisha mbunge wa viti maalum kupitia tanga apigie kura ccm eti kisa mwenyekiti mkoa arusha -hii ni kuvunja sheria au? jibu unalo
  2. Mkurugenzi anatakiwa kuendesha kikao cha madiwani cha kuchagua meya na naibu wake baada ya idadi ya wajumbe kufika ukiondoa wajumbe yaani madiwani wa chadema 2/3 haipo nani kavunja sheria wewe muya????? jibu unalo
  3. Hon. Lema aliwambia waliitisha kikao hicho wakati wametoa barua ya semina bila kuwajulisha chadema wapi kuna haki???
  4. Police kazi yao ni kulinda amani raia na mali zake kwakuwa mheshimiwa Lema alikuwa anahoji utaratibu na ccm kwenda kumwita OCD amutoe Lema kwenye kikao na hivyo OCD kutumia Polisi hiyo ni haki? Tuambie wewe muya unajua sheria
  5. Tangu uzaliwe ni lini ulisikia mbunge wa ccm kapigwa hata kofi na polisi zaidi ya mgombea mbunge wa shinyanga kumpiga mtama OCD kule Maswa je angekuwa Shibuda ndio kampiga OCD ingekuwaje?? hiii inasikitisha saana.
  6. Kwa ujumla CCM sasa inaonesha waziwazi sura yake halisi ya sasa na kwa vyovyote vile inachochea hasira na vurugu ipo siku tutasema vinginevyo harafu wewe muya sijui utatwambia lini -kipofu mkubwa au fisadi mkubwa wewe.
  7. Mapolisi wa namna hii ipo siku nguvu ya umma itawaangukia ndio watapata adabu na fundisho
  8. Ninaamini IGP hana uwezo wa kufanya lolote kwa ccm kupigwa kwa lema ni agizo la serikali kupitia mkurugenzi arusha mjini aliyekuwa akitekeleza amri ya aliyemtea kuhakikisha kwa kumwaga damu au vingenevyo chadema haiongozi jiji -yana mwisho haya
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi nchi hii inawezaje kuwa na mtu anayeitwa Mkurugenzi wa Jiji hasiyejua sheria ya serikali za mitaa kiasi cha kusimamia uchaguzi batili! Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipuuzia kumchukulia hatua Afisa huyo utakuwa ni ushahidi tosha ya kuwa hata Pinda yote ayasemayo kuhusu kupambana na uozo katika halmashauri hapa nchini, ni danganya toto.
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KAMA HATA MHE MBUNGE HAYUKO SALAMA WANANCHI TUKIMBILIE WAPI???

  Kwa kitendo hiki cha ajabu (Askari Polisi Kumpiga Mh Mbunge) sana kuwahi kufanywa nchini mwetu, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI PAMOJA NA SAID MWEMA WOTE WAJIUZULU mara moja kwa kuzingatia MSINGI WA UWAJIBIKAJI katika dhana zima ya Utawala bora na huyo askari awajibishwe kwa Maslahi ya Umma!!

  Hili la askari kumpiga mbele ya hadhara Mhe Mbunge mbele ya wananchi anaowaongoza kamwe HAIKUBALIKI na wala HAIVUMILIKI hata kidogo. Katika hili hakuna kiwango chochote cha MAELEZO WALA VISINGIZIO vitakavyoweza kutolewa kuhalalisha CHOMBO CHOCOTE KUMDHALILISHA KIONGOZI kiasi hicho.

  Chombo chetu cha jeshi la polisi KIKATIBA ni chombo USALAMA NA UTULIVU kumshambuliwa kiongozi yeyote bila kujali itikadi yake ya kisiasa nchini. Kitendo hiki hakina tofauti sana na kitendo cha KUMPIGA BABA AU MAMA MZAZI mbele ya watoto wake.

  Msononeko kwa watoto hautokaa ufutike kiurahisi kwenye kumbukumbu zao na hata kusadikiwa jambo kama hili kusababisha madhara makubwa kisaikolojia katika jamii. Ni kutokana na ukweli huu ndio MAANA SHERIA KOKOTE DUNIANI HUTOA ADHABU KALI MNO kwa wadhalilishaji wa aina ya askari polisi huyu wa Arusha.

  Siku zote watoto pale nyumbani huamini kwama ama BABA AU MAMA NDIO WATU WENYE NGUVU KULIKO WOTE DUNIANI kiasi kwamba wanapoona mashujaa wao hawa wakipigwa hadharani basi ujue moja kwa moja kwamba mpaka hapo Ulimwengu wao unakua umefunikwa juu kutazama chini.

  Kitendo cha KUSHAMBULIWA KWA MANENO NA KIWILI NA KUJERUHIWA kwa mwakilishi halali wa raia bungeni akiwa katika eneo lake ya kazi jimboni kwake Arusha ni kitendo UDHALILISHAJI MKUBWA mbele ya macho ya umma wa Tanzania.

  Kama hilo halitoshi na tunaiomba Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kamati zake za (i) Kamati ya Maadili na (ii) Kamati ya Ulinzi na Usalama kukutana mara moja na KUSHUGHULIKIA KWA NAMNA ITAKAVYOTURIDHISHA WANANCHI JUU YA HUU UTOVU MKUBWA WA NIDHAMU uliofanywa na askari wetu kwa kiongozi wa ngazi ya juu wa ngazi ya ubunge kama alivyofanyiwa Mhe Lema.

  Hili ni jambo zito lisilohitaji hiyana hata kidogo. Nani analo jibu atakayepigwa kesho au kesho kutwa kati ya viongozi wetu. Huwezi kujua kesho huenda akapigwa Waziri, Waziri Mkuu au hata Raisi wetu. Japo Rais katukashirisha sana alilolifanyia taifa kwenye uchaguzi mkuu lisilokubalika lakini mtu kumpiga hatuwezi kukubali hata kidogo.
   
 6. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Daima Tanzania Polisi hufikiri wao wapo juu ya sheria angalia njia watumiazo katika hata kutawanya watu wanapoandamana au kutaka kuandamana mabavu huwa ni mengi sana huku wakijua wazi kuwa Watanzania ni watu wa kufyata mkia kama Jibwa lionapochatu! Kwa kitendo hicho ni wazi kuwa Polisi kama wataendelea na Ubabe wa kijinga ipo siku wataleta maafa makubwa sana.
  Leo Mbuge anapigwa na Polisi kwa kisa gani na chanzo nini hasa? Je Polisi katumwa au ni Kichaa? haiingii hakilini hata kidogo.Hakuna jambo la mzaha kama kuendelea kulea watu wachache kwa kutumiwa au kujua kuwa watabebwa na mtu furani basi kujichukulia maamuzi mikononi.

  Hichi kitendo ni cha kulaaniwa kwa namna yeyote ile!
   
 7. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,073
  Likes Received: 4,648
  Trophy Points: 280
  Just imagine, yule mgombea ubunge wa Shinyanga alimvamia mkuu wa kituo cha polisi na kumpiga hadi chini ni kwa sbb alikuwa wa CCM
  wala hakuna hatua za kisheria zilichukuliwa dhidi yake, ila huyu kwa sbb ni wa CDM wanaonea, ndio maana tunasema 2015, already tutakuwa na katiba mpya, NEC mpya na huru, lazima CHANGE ije, we are tired of oppression & poor governance
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  brutality and subjugation of strong african v. fellow weak african! wziri huyo juzi kaanza makeke utasikia tu sijiuzulu ngó!
   
 9. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ulikubaliaje kuchaguliwa kinyume na kanuni? Hufai kuwa mwakilishi wa wananchi. Ndumilakuwili we.
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WHAT MAKES THE GOVERNMENT THINK BEING IN OPPOSITION MAKES OTHERS LESSER CITIZENS??

  No more Police Brutality!! No more selective treatment of citizens alongside their political beliefs, race raligion or any other. We want to see immediate, most deserving and substantial action NOW.

  If a member of parliament can not be any safer simply because he is coming from an opposition party the what about the actual state of affairs of treatment that are being meted out by various state organs to the people being represented by MPs in the opposition camp.

  Does being in the opposition make someone a lesser citizen of this country by any standards??? Minister for Home Affairs MUST RESIGN now!! The IGP Saed Mwema MUST give way on this Most embarassing 'politically instigated' police brutality.

  What conclusions would one make on a CCM parliamentary aspirant (No near Member of Parliament) arrogantly walk into a police station in Shinyanga, unleashes several thrushes to a senior police officer and bangs the door of his VX car before speeding away scot-free to-date.

  But to another extreme, we meet a somber scenario of a duly elected CHADEMA Member of Parliament being subjected to such major BODILY ASSAULT and untold PUBLIC EMBARRASMENT by being roughed up to literaly unconciousness in front of the eyes of his electorates!! Is someone inclined to spark-off chaos in the country through suchlike reckless and most irresponsible acts?

  It is very hard to understand whether police officers expect to direct an MP on when and how to executi his lawful duties in the constituency. This is a case whereby the a area MP, Hon Lema, going about his normal duties in his Arusha Constituency, the roles for which the people enlisted his services just the other day in Arusha only for yet another senior police officer to start raining verbal insults and full-blust bodily assault to no avail!!!

  Resign from our honoured offices now!!!

   
 11. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Hamna haja ya waziri wa mambo ya ndani au IGP Kujiuzuru. Nasema hivyo kwani hao askali wametekeleza maagizo ambayo moja kwa moja yana baraka za ikulu na mkwele na hao watendaji wa wizara na polisi wapo hapo kama vivuli tu mkwele hii inchi yeye ni kila kitu na hizo wizara na watendaji wengine wapo tu ila hawana kazi, maamuzi yote ni ya mkwele,Ndio maana hata wakitaka kutoa maamuzi lazima wapige simu kwa mkwele hata kama wakijua haki ipo huku ili mkulu aamue haki ataihamishia upande gani.SASA HAPA INATAKIWA MKWELE AJIUZURU na wengine wafuatie kwani yeye ni chanzo cha matatizo haya yote.CCM is very foolish.
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180


  Soma taratibu uelewe badala ya kukurupuka kama panya.
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Dec 21, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Wajiuzuru!! Labda kama wamebadilika.
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180


  Hana ujasiri wa kufanya hivyo, Si Mwema wala Nahodha.
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180


  Tena siku mbunge anapewa Kibano Mkwere alikuwepo A-town.
   
 16. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tupo pamoja Denyo maana huu ni unyanyasaji wa hali ya juu mno na sisi wananchi tumechoka kuvumilia, Kama hii ndio amani wanayoihubiri TZ sasa tunaona wazi haipo na kilichobaki ni kuondoa madarakani Hawa mafisadi.

  Mimi naiunga mkono CDM na viongozi wake katika kulaani matukio kama haya na itafika mahali wananchi watashindwa kuwa wavumilivu kwani wananchi kifanya CCM siyo halali kabisa.

  Kwanini siku zote wavunje sheri tena kwa nguvu, ingekuwa ni CDM wanafanya hivyo ingekuwaje?

  Naomba majibu kutoka kwa makada wa CCM waliopo humu. Maana mimi siwaelewi kabisa inakuwaje mtu anavuja sheria polisi wapo wasiwakamate na babala ya wanamkamata Mbunge mtetezi wa wananachi na haitoshi tu kumkamata na kumpiga hadi kuzimia kis kasema madiwani wanCCM na Mkurugenzi wanavunja Sheria.

  Nawahakikishia hao dawa yao iko jikoni.

  Peoples power
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wa kuwalaumu zaidi ni polisi wenyewe kwa kushindwa kuelewa wanamtumikia nani... wao wanajiegemeza kwa CCM wakidhani ndio baba na mama lakini wanasahau wanaishi mitaani ambapo CCM ni bendera na kofia tu

  labda tuwapime akili polisi wote kujua wanawaza nini kwani kupiga sio suluhu ya jambo lolote lile....
   
 18. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Naungana na wewe hapo, kuna habari JK alikuwa Arusha siku ya ijuamaa akifungua hotel ya Mount Meru kwa kutumia hele za watanzania, na akaangiza meya wa Arusha lazima atoke CCM. Sasa aligungua hotel binafsi, akatoka tamko kama M/Kiti wa CCM na piak kama rais wa TZ.
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Dec 21, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ushauri kwa lema na baadhi ya wabunge wa chadema... si lazima kuwa vuvuzela ndio upate sifa

  fanya mambo kwa ustadi uwazidi akili, kesho ukiwa kilema au taahira haitakusaidia sana, kuna njia mbadala

  siungi mkono polisi lakini na wewe jiulize why you all the time? umekua drama queen to say the least
   
 20. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #20
  Dec 21, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yaani nimefurahi sanaaaaaaa. acha kwanza wapate kichapo sasa zamu yao. walipigwa CUF wote wakawa wanasherekea, kushangilia na kuwaona wapinzani wenzao ni watu wa fujo sasa zamu yenu. Hapo ndo mtakapojua kuwa CCM hawana parmanet rafiki ila wana parmanent interest. cheki mnavyolalamika. hapa lazima mshike adabu na ndo hapo mtakapoona umhimu wa kuungana na wenzenu kuwaondoa hawa waheshimiwa CCM. Wakati akina Lipumba wanavunjwa mikono na akina seif wakisota jela kudai katiba mpya hivi nyinyi milisemaje vile? Sikumbuki! Nyinyi mliona mwenzenu ananyolewa ila nyinyi mlipuuzia na hamkutia maji, sasa ni kunyolewa kavukavu (aka dry). mkimaliza kunyolewa mtakuwa mmejifunza kwani zitaota tena. Hata hivyo muombe huyu mkulu wa wa sasa (JK) andalao hakuwapiga virungu hata kipindi cha kampeni angekuwa mtangulizi wake (BM) mbona cha moto mngekiona. Natamani BM angerudi hata mwaka mmoja tu kwanza mjifunze nini maana ya utengano na ni maana ya umoja (msamiate primary school) mimi ngoja kwanza nikapate kinywaji baridiiii. see you then.
   
Loading...