LEMA ni zaidi ya MALEMA!

LEMA ni zaidi ya MALEMA!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Godbless Lema anapendwa jamani. Kaeni msikie tu,wengine tumejionea. Jana nilishindwa kuhudhuria kwenye kesi ya mteja wangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.Nilijikuta nimefika viunga vya Mahakama Kuu(kwakuwa Mahakama ya Rufani nayo uliketi humo jana) kushuhudia na kusikiliza kusikilizwa kwa Rufaa ya Mbunge huyo wa zamani wa Arusha Mjini.

Kwakuwa katika Rufaa hiyo kumewasilishwa Pingamizi la Awali kuwa Rufaa ni batili,Mahakama ya Rufaa jana ilianza kusikiliza pingamizi hilo kama inavyopasa. Pingamizi liliwekwa na upande wa Wajibu Rufaa ukioongozwa na Mawakili Wasomi Alute Mughwai na Akida. Kwa siku itakayopangwa,kutatolewa uamuzi wa pingamizi hilo baada ya maelezo juu ya suala hilo kutolewa jana Mahakamani hapo. Uamuzi huo wa pingamizi utafanya Rufaa ya Lema iendelee au isiendelee. Ni hivi,kama pingamizi litakubaliwa rufaa itatupwa yote. Kama pingamizi likitupwa,usikilizaji wa Rufaa utaanza.

Godbless Lema,kwa hapa Arusha,hufananishwa na Malema wa Afrika Kusini. Eti kwakuwa wote ni 'vipenzi' wa vijana nchini mwao. Lakini,kadiri nimjuavyo Malema wa kwa Mandela na Lema wa Tanzania,Lema yuko juu. Arusha nzima ilisimama jana.Mimi nisiwe msemaji sana.Ujumbe wangu ni kuwa Lema ni kiboko. Wana-Arusha bado wanamhitaji sana. 'God bless our King' wameandika bangoni wana-Arusha.
 
Picha zilizorushwa na ITV zilinitisha hata mimi,Vijana wa Arusha wanamuamini Lema kupita maelezo!! Lema anabeba deni kubwa sana kwao!!!
 
Hilo hata hao CCM wanalijua na ndio maana wanachelewesha kesi yake manake
wanajua hata wakirudia uchaguzi hawatoboi.
 
Kila mtu anajua ukweli upo palepale . Vijana wa arusha hawababaishi wanajua wakifanyacho.
 
Wana Arusha wanajua nini pumba na nini mchele hivyo hata CUF wakiweka kambi mwaka mzima bado hawataweza kuitingisha CDM
 
Mleta Mungu akubariki kwa hekima yako ya kuona mambo kwa jicho la mbali.

Lema ni noumaaaaaaaa !
Lema ni jembe.....................!

Kwakweli namkubali sana huyu kamanda na hata kama ningekuwa na dada basi ningemuozesha kama zawadi.

Mtu ambaye kajishusha kwa ajili ya watu.

Hapa napata picha kuwa Lema ni mithil ya Martin luther King au Marcus garvey.

Lema we ni jembe..............!
 
wao CUF wasingeingia gharama ya kusafirisha watu.......kama ilikuwa kujaza mkutano....simple....mi mwenyewe ningeitwa ningeenda kujaza.....na ningehamasisha na wenzangu tukajaze....tujae weeeeeee......lakini rohoni tunajua tunataka nini.....
 
ameoa mkuu.....na mke wake ana mtoto mpya wa juzi juzi kati hapa......
 
Godbless Lema anapendwa jamani. Kaeni msikie tu,wengine tumejionea. Jana nilishindwa kuhudhuria kwenye kesi ya mteja wangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.Nilijikuta nimefika viunga vya Mahakama Kuu(kwakuwa Mahakama ya Rufani nayo uliketi humo jana) kushuhudia na kusikiliza kusikilizwa kwa Rufaa ya Mbunge huyo wa zamani wa Arusha Mjini.

Kwakuwa katika Rufaa hiyo kumewasilishwa Pingamizi la Awali kuwa Rufaa ni batili,Mahakama ya Rufaa jana ilianza kusikiliza pingamizi hilo kama inavyopasa. Pingamizi liliwekwa na upande wa Wajibu Rufaa ukioongozwa na Mawakili Wasomi Alute Mughwai na Akida. Kwa siku itakayopangwa,kutatolewa uamuzi wa pingamizi hilo baada ya maelezo juu ya suala hilo kutolewa jana Mahakamani hapo. Uamuzi huo wa pingamizi utafanya Rufaa ya Lema iendelee au isiendelee. Ni hivi,kama pingamizi litakubaliwa rufaa itatupwa yote. Kama pingamizi likitupwa,usikilizaji wa Rufaa utaanza.

Godbless Lema,kwa hapa Arusha,hufananishwa na Malema wa Afrika Kusini. Eti kwakuwa wote ni 'vipenzi' wa vijana nchini mwao. Lakini,kadiri nimjuavyo Malema wa kwa Mandela na Lema wa Tanzania,Lema yuko juu. Arusha nzima ilisimama jana.Mimi nisiwe msemaji sana.Ujumbe wangu ni kuwa Lema ni kiboko. Wana-Arusha bado wanamhitaji sana. 'God bless our King' wameandika bangoni wana-Arusha.

Inategemeana na aina ya viajana wanaobeba mabango hayo. JULIUS MALEMA mimi ninavyojua, huwa vijana wazee na makundi mbalimbali wanaacha kazi maofisini, biashara zao na kwenda kumsikiliza. Ni aibu kubwa sana kufananisha kazi anayoifanya JULIUS MALEMA kwa waafrika kusini na huyu jamaa wa arusha. LEMA ana mambo mengi sana anayojificha kupitia kivuli cha siasa. umaarufu wa LEMA hauna hata miaka miwili na kila mtu anajua kabla ya hapo alikuwa anafanyakazi gani tena kazi zinazohatarisha maisha ya raia wasiokuwa na hatia. Binafsi najua mji wa arusha unaweza kuwa wa kwanza kwa matukio ya uhalifu , so LEMA lazima atakuwa na marafiki wengi sana wanaotaka kujificha kupitia yeye na kwa maana hiyo wanaweza kuwa na ushawishi mkubwa sana kwa vijana katika kufanya fujo na ikaonekana kuwa anashangiliwa LEMA.
 
Siasa uchwara hizi za Mtaroni, jinsi anavyowasumbuwa haya mnayoyasema yangekuwa na ukweli si mngemfufulia kesi yoyote mumpoteze jela? Gamba wewe huna hoja bali viroja.
 
mkuu hata wewe huyajui hayo!
 
wao CUF wasingeingia gharama ya kusafirisha watu.......kama ilikuwa kujaza mkutano....simple....mi mwenyewe ningeitwa ningeenda kujaza.....na ningehamasisha na wenzangu tukajaze....tujae weeeeeee......lakini rohoni tunajua tunataka nini.....
Wanafuata taratibu za ndugu zao CCM kusafirisha watu kwenye mikutano wawaaminishe watanzania kuwa bado wanakubalika wakati si kweli.
 
nang'atuka bora usiongee kitu ambacho huna uhakika nacho
Kama huyo Lema unayesema ni mhalifu kuna vyombo vya sheria ambavyo vinafanya kazi usiku na mchana. Kuna usalama wa taifa ambao iwapo watataka record za Lema wasingeshindwa kuzipata wamfungulie mashtaka. Tume ya taifa ya uchaguzi iliyompitisha Lema kugombea ubunge ina record zake. Kama ni muhalifu wasingeshindwa kumzuia kugombea. Hata hao waliofungua kesi wangekuwa na la kusema kuwa huyu ni mhalifu sugu hapaswi kugombea.
Katika mashtaka yake hilo halijaongelewa. Kuwaambia watu wote wanaompenda Lema kuwa eti ni wahalifu na kuna watu wanajificha nyuma ya Lema ni kuwakosea adabu watu wa Arusha. Na hilo unalosema kuwa wanaomshabikia ni vijana nafikiri unakosea sana maana wapiga kura wa Arusha sio vijana peke yao wapo watu wazima wenye shughuli zao.
Ungeangalia umati wa jana wakati wanatoka mahakamani au watu walioacha shughuli zao watu wazima na vijana kabla ya kuja hapa kutoa conclusion yako kuwa wanaomshabikia ni kikundi cha wahalifu wanaojificha nyuma yake.
 
Last edited by a moderator:
Siasa uchwara hizi za Mtaroni, jinsi anavyowasumbuwa haya mnayoyasema yangekuwa na ukweli si mngemfufulia kesi yoyote mumpoteze jela? Gamba wewe huna hoja bali viroja.

Matola umeona siasa za magamba. Wakishindwa kutetea hoja wanakuja na ujinga kuwa Lema ni mhalifu na ana record ya uhalifu
Kama ana hiyo record hiyo kwa nini wanasubiri muda wote wasimpeleke ndani au wakamfungulia kesi ya aina hiyo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom