Lema: Narudi Tanzania

Nanyinyi mtakufa siku moja hamtaishi milele na tabiri zenu za bhangi
Kunywa maji mjane, hakuna namna.
Acha wivu, wenye maono yao wamebarikiwa. 🤸🏾‍♂️🤸🏽‍♀️🤸🏾‍♂️🤸🏽‍♀️🤸🏾‍♂️🤸🏽‍♀️
 
Ndio utakufaa siku ukumbuke siku hii nayokwambia utakufa siku moja
Ata wewe ni maiti mtarajiwa mkuu, so tenda wema ufe kifo chema usitese watu, usionee watu na tenda haki kwa kila alie mkubwa na mdogo, wewe ni sikio la kufa bt naamin leo utasikia.
 
Akaribie kulipa madeni ya watu aliyoyakimbia pia akumbuke sio mbunge tena halafu chama hakina ushawishi kina kiti kimoja
Pia ule ulevi wa wachache kudhani nchi Hii ni ya kijani pekee umeisha, hakuna ushamba huo tena! Lema aje aijenge nchi yake kwa uhuru kabisa!
 
Sawa unafurahi kwa mwenzako akati upo safarini huko huko unaelekea wala hutakiepuka kifo
Watu mnakua kama mmesahau kwamba Azori na saa8, mliona ni mbu tu,!na Lisu kuchakazwa risasi ni ‘uzalendo’?! Hamkujua kwamba trend hiyo itaendelea kwa vifo vya upande wa pili! Kuna kanuni muhimu
Sana ya maisha inaitwa “Utavuna ulichopanda”! Msiishie kulaumu tu, kumbukeni na mrekebishe ufa huu wa kitaifa mliojenga!!
 
Godbless Lema asema anafikiria kurudi nyumbani Tanzania,

Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye alikimbilia ughaibuni kwa madai ya wasiwasi wa usalama wake mara baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 anafikiria kurudi nchini Tanzania.

Baada ya kifo cha Rais Magufuli Lema anatarajia kuona uongozi wa Rais Samia ukirekebisha na kutafuta maridhiano ya taifa zima.

‘’Nataka kurudi nyumbani hata leo, nyumbani ni nyumbani tu, wakati nakimbia nyumbani nilishuhudia uzoefu mbaya mimi na familia yangu’’, alisema

Lema ameeleza kuwa mabadiliko ya mifumo ya kiutawala ikiwemo viongozi watakaojali haki ni sura itakayorejesha imani ya kwamba sasa maisha yako salama.

‘’Nitarudi nyumbani mapema sana kuendelea na mapambano. Uwepo wetu huku hauna maana ya kwamba tumekuja kula bata, hakuna maisha yoyote, mtu anaweza akakimbia nyumbani kwao ambako amejijenga vizuri.’’alisisitiza

Hata hivyo Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilitupilia mbali madai hayo ya upinzani na kusema hayo ni maigizo ya upinzani.

‘’Tanzania ni nchi inayoheshimu utawala wa sheria.’’alisema msemaji wa serikali Dokta Hassan Abbas.

Samia Suluhu Hassan ameapishwa leo jijini Dar es salaam kuongoza awamu ya sita ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kifo cha mtangulizi wake John Pombe Magufuli.
Wabongo bhana. Shida tupu
 
Lema rudi nyumbani tu. Walichokuwa wanataka ni Ubunge wako tu na sio maisha yako. Kama ni kukuua wangeweza kukuua mapema kabla
 
Ata wewe ni maiti mtarajiwa mkuu, so tenda wema ufe kifo chema usitese watu, usionee watu na tenda haki kwa kila alie mkubwa na mdogo, wewe ni sikio la kufa bt naamin leo utasikia.
Jpm alifanya mazuri ndio maana ameliliwa na wengi siku ya mazishi yake na sauti ya wengi ndio sauti ya Mungu ila wachache kama nyie waliotumbuliwa vyeti feki, wavivu, wala rushwa, wakwepa kodi, mafisadi, wenye siasa za maji taka, mliokosa sera, walizoea uwizi ndio mlimwona dikteta ndio mnashabikia vifo na magonjwa nanyi mtakufa pia siku moja
 
Mazaa sa100 hajabadili viongozi kageuzageuza kidogo so utakutananacho tuu bora uskilizie tuu chalanguu
 
Back
Top Bottom