Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Godbless J Lema

Arusha MP
Sep 28, 2013
92
2,205
Mh Rais Magufuli nakusalimu.

Nimetoka Magereza hivi karibuni ambako nilikuwa huko kwa zaidi ya miezi minne kwa kunyimwa masharti ya dhamana kwa dhamana iliyokuwa wazi.

Mh Rais, nimeona kwenye vyombo vya habari leo kuwa kwamba wale Wabunge waliokuwa wanataka kunisalimia nilipokuwa Magereza kuwa ni wasaliti wa chama cha CCM, Mh Rais wengi walinisalimia, Wachungaji, Masheikh, Wabunge na Viongozi mbali mbali, sidhani kama hatua hii ilikuwa ni usaliti isipokuwa upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yoyote haswa wakati wa matatizo.

Mh Rais, nimeogopa sana kwa kauli hii yako, je Taifa linakwenda wapi, hivi kweli sisi Wabunge ni maadui? Kama viongozi tutafikiri utengano ni moja ya njia ya kuimarisha vyama vyetu, basi bila shaka tutakuwa tunalitendea Taifa ubaya .

Dhambi hii ikikomaa basi ni hakika kwamba lugha za udini, ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa, ni muhimu sasa tukajenga utamaduni wa kuhimiza mshikamano wa Kitaifa bila kujali itikadi kama kweli tunawapenda masikini na wanyonge wa nchi hii.

Nawaomba Wabunge wenzangu walionijali wakati niko magereza wasijisikie vibaya kwani walifanya jambo jema na muhimu kwa wakati muhimu sana katika maisha yangu, ninatarajia kuwa Spika wa Bunge atatoa kauli juu ya kauli yako.

Mh Rais wakati wa Msiba wa Christina Lissu dada yake na Mh Tundu Lissu nilikuona katika msiba ule wewe na Mama yetu Mke wako, je Mh Rais na wewe ulikuwa unasaliti Chama chako?

Mh Rais neno la Mungu linasema, Wapendeni maadui zenu, waombeni wanaowauzi , wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu.

Mungu akubariki sana, natumaini Mh Rais sitakamatwa leo kwa ujumbe huu mfupi.


Godbless J Lema (MB)
 
Ujumbe Muhimu sana. Ni na uhakika watu wake wameuso na kumfikishikia. Binafsi niliogopa sana niliposikia hii kauli kutoka kwa Mh. Rais wa Jamhuri.

Kwetu sisi Roman Catholic,kuwatembelea wafungwa/mahabusu kunaongeza rehema na baraka zaidi. Hapo naona Rais anataka kuwafundisha watu matendo gani ya huruma wafaanye. Mbinguni kila mtu ataenda peke yake. Asitake kuwafanya watu watende dhambi ya chuki kwa maslahi yake binafsi.
 
Kamanda pole sana na karibu. Wapinzani kwa namna Moja ama nyingine tunawaomba mshikamane sana katika kipindi hiki. Aliyoyatabiri Tundu Lissu Leo yanatimia. Nchi IPO chini ya dictatorship. Katumieni bunge lenu tukufu kufanya yaliyo mema dhidi ya kauli chafu za Rais huyu
 
Back
Top Bottom