Lema kuwataja waliomteka Dk. Ulimboka leo Ilala Bungoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema kuwataja waliomteka Dk. Ulimboka leo Ilala Bungoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mongoiwe, Jun 30, 2012.

 1. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Leo Jumamosi, Juni 30, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, atakuwa na mkutano wa hadhara Ilala Bungoni.

  Vyanzo vyangu vya habari, kutoka karibu na Lema vinasema kuwa leo atalipuka sana. Mojawapo ya masuala atakayolipua ni kuwataja vigogo/kigogo waliohusika katika suala la Dkt. Ulimboka.

  Jamani wenzetu wa habari, sijui vyombo vingapi viko maeneo hayo, mtupatie taarifa hizi mapema iwezekanavyo kama ni kweli. Hatuwezi kusubiri mpaka kesho au usiku.

  Nawasilisha.
   
 2. Kayoka

  Kayoka JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,427
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  anaingilia uhuru wa jeshi la polisi, wacha naye atulie huku tukimwomba mungu amponyeshe mapema dr. Ulli aje awataje waliomteka na kumuumiza.
   
 3. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jembe letu hilo. Eti pimbi wewe ndio msangi nini?
   
 4. M

  MMASSY JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Wewe unayemwitalema pimbi inawezekana kweli wewe ni msangi!!
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"] Madaktari 146 watimuliwa kwa mgomo [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 30 June 2012 10:04 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Mgonjwa akiwa nje ya geti la Taasisi ya Mifupa MOI jijini Dar es Salaam jana akiwa ajui chakufanya baada kukuta geti hilo limefungwa kutokana na mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.Picha na Venance Nestory

  Waandishi Wetu
  MADAKTARI 146 wamefukuzwa katika hospitali mbalimbali nchini kutokana na kushiriki mgomo unaoendelea nchi nzima kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yao.

  Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa, madaktari hao walitimuliwa katika Hospitali za Bugando na Sekou Toure mkoani Mwanza na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na ile ya Rufaa Dodoma.

  Wakati Serikali ikichukua hatua hiyo, mgomo huo jana uliendelea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Ocean Road, Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) za jijini Dar es Salaam, Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro.

  Katika kile kinachoonekana kuwaunga mkono wenzao, madaktari bingwa wa MOI, MNH na Ocean Road jijini Dar es Salaam, jana walitangaza rasmi kuingia kwenye mgomo huo hadi madai hayo yatekelezwe.

  Madai ya madaktari ni hali bora ya mazingira ya utoaji huduma nchini, ongezeko la mishahara, posho za kufanya kazi katika mazingira magumu, posho za kufanya kazi katika mazingira hatarishi na posho za kuitwa kazini.

  Tamko la madaktari hao bingwa, lilitolewa jana na msemaji wao, Dk Catherine Mng'ong'o muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

  Tamko hilo limekuja siku moja baada ya baadhi yao kuanza kushiriki mgomo huo juzi, kushinikiza pamoja na mambo mengine, Serikali itoe tamko juu ya tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk Ulimboka.

  Hata hivyo, wakati madaktari hao wakitoa tamko hilo, uongozi wa Moi jana ulitoa tangazo kuwataka madaktari wote walioshiriki mgomo huo kurejea kazini ifikapo Julai 2, mwaka huu, vinginevyo watafukuzwa kazi.

  Jana jengo la MOI lilikuwa limefungwa kwa makufuli, huku wagonjwa wakielezwa kuwa huduma zote hazitolewi zikiwamo za dharura ambazo awali ziliendelea kutolewa.
  Mmoja wa walinzi aliwambia waandishi wa habari kuwa, amefunga mageti kutokana na amri ya mkuu wake wa kazi.
  "Mimi ninatekeleza amri ya bosi wangu, amenitaka kufunga geti na hakuna mtu kuingia, awe mgonjwa au ninyi waandishi wa habari kwa kuwa hakuna huduma zinazotolewa humu," alisema.
  Mkoani Mwanza
  Madaktari 63 walio katika mafunzo ya vitendo kazini wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Hospitali ya Mkoa Sekou Toure wametimuliwa na kurejeshwa wizarani kutokana na mgomo huo.

  Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dk Charles Majinge alisema kuwa, juzi aliwataka madaktari waliokuwa katika mgomo kurejea kazini, lakini hawakufanya hivyo na jana akaamua kuwarejesha 47 wizarani.

  Katika Hospitali hiyo ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Valentino Bangi alisema, madaktari 16 wamesimamishwa kufanya kazi kutokana na agizo la wizara.

  Kilimanjaro

  Madaktari walioko kwenye mgomo katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi mkoani Kilimanjaro walisema jana kuwa, kinachofanywa na Serikali kuwafukuza kazi waliogoma, ni njia mojawapo ya vitisho, lakini wakasema kuwa kamwe hawataogopa.

  Madaktari hao ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini walisema, wao wanaendelea na mgomo mpaka pale Serikali itakapotekeleza madai yao.

  "Tumesikia wenzetu wa Dodoma na Mbeya wamefukuzwa ….Hiyo haitufanyi turudi kazini na kama Serikali inaona hiyo ndiyo njia ya kumaliza mgogoro huu waendelee sisi tutarudi kazini pale itakapotimiza tunayotaka," alisema mmoja wa madaktari hao.

  Mbeya

  Juzi Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, ilitoa tangazo la kuwataka madaktari waliopo mafunzoni waliogoma kurejea kazini jana, na endapo wangekiuka agizo hilo wangekuwa wamejifukuzisha kazi. Na hadi jana jioni hospitali hiyo ilikuwa imewafukuza madaktari 72.

  Ocean Road

  Katika Taasisi ya Taifa ya Saratani, (Ocean Road), kutokana na madaktari sita kusitisha kutoa huduma tangu Dk Ulimboka alipojeruhiwa kwa kipigo, waligoma na jana Mkurugenzi wa Tiba na Huduma Diwani Musemo alionekana akitembelea wagonjwa.

  Dodoma
  Madaktari 11 wa mafunzo kwa vitendo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma nao wamefukuzwa, tukio ambalo jana lilileta usumbufu mkubwa katika upatikanaji wa tiba hospitalini hapo.
  "Kwa hakika matibabu yanaendelea ingawa ni katika hali ya kusuasua. Hatuna uhakika kama kweli kuna mgomo wa chinichini au la, maana mimi nimefika mapema, lakini bado sijahudumiwa," alisema mmoja wa wagonjwa waliozungumza na mwandishi wa habari.
  Arusha
  Katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, huduma zimedorora lakini Mganga Mkuu, Dk Omar Chande alisema jana kuwa, imekuwa ni vigumu kuchukua hatua kuwabana madaktari ambao wanatuhumiwa kufanya mgomo baridi, kwani wote wanaripoti kazini.

  "Ni kweli kuna taarifa hizi za kuwapo mgomo baridi, lakini madaktari wote wapo kazini, ila kama kuna kufanya kazi chini ya kiwango, tumeanza uchunguzi," alisema Dk Chande.
  Amana

  Katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam utoaji wa huduma ulisuasua kutokana na mgomo huo jambo lililofanya uongozi kuweka tangazo kwenye Ofisi ya Mganga Mkuu kuwataka watumishi wote ambao hawakuwapo kazini kuanzia Juni 25, 2012 waandike barua za kurejea kazini.

  Tangazo hilo pia linawataka madaktari walioko mafunzoni kuandike barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia kwa mganga mkuu wa hospitali hiyo.

  Habari hii imeandaliwa na Frederick Katulanda, Mwanza, Rehema Matowo, Moshi, Zakhia Abdallah (SJMC), Editha Majura, Israel Mgussi, Dodoma), Victoria Mhagama na Daniel Mwingira, Sam Jacob na Issa lazaro (SJMC, Godfrey Kahango, Mbeya, na Mussa Juma, Arusha.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  "Solidarity should also mean insistence on the rule of law. To close one's eyes to trampled freedoms, to get used to violence, become inured to political murders, is to approve them and accept that there are people deserving of justice and others deserving of oppression." Utapona Kaka Ulimboka
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"] Madaktari 146 watimuliwa kwa mgomo [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Saturday, 30 June 2012 10:04 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Mgonjwa akiwa nje ya geti la Taasisi ya Mifupa MOI jijini Dar es Salaam jana akiwa ajui chakufanya baada kukuta geti hilo limefungwa kutokana na mgomo wa madaktari unaoendelea nchini.Picha na Venance Nestory

  Waandishi Wetu
  MADAKTARI 146 wamefukuzwa katika hospitali mbalimbali nchini kutokana na kushiriki mgomo unaoendelea nchi nzima kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yao.

  Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa, madaktari hao walitimuliwa katika Hospitali za Bugando na Sekou Toure mkoani Mwanza na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na ile ya Rufaa Dodoma.

  Wakati Serikali ikichukua hatua hiyo, mgomo huo jana uliendelea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Ocean Road, Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) za jijini Dar es Salaam, Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro.

  Katika kile kinachoonekana kuwaunga mkono wenzao, madaktari bingwa wa MOI, MNH na Ocean Road jijini Dar es Salaam, jana walitangaza rasmi kuingia kwenye mgomo huo hadi madai hayo yatekelezwe.

  Madai ya madaktari ni hali bora ya mazingira ya utoaji huduma nchini, ongezeko la mishahara, posho za kufanya kazi katika mazingira magumu, posho za kufanya kazi katika mazingira hatarishi na posho za kuitwa kazini.

  Tamko la madaktari hao bingwa, lilitolewa jana na msemaji wao, Dk Catherine Mng'ong'o muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

  Tamko hilo limekuja siku moja baada ya baadhi yao kuanza kushiriki mgomo huo juzi, kushinikiza pamoja na mambo mengine, Serikali itoe tamko juu ya tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dk Ulimboka.

  Hata hivyo, wakati madaktari hao wakitoa tamko hilo, uongozi wa Moi jana ulitoa tangazo kuwataka madaktari wote walioshiriki mgomo huo kurejea kazini ifikapo Julai 2, mwaka huu, vinginevyo watafukuzwa kazi.

  Jana jengo la MOI lilikuwa limefungwa kwa makufuli, huku wagonjwa wakielezwa kuwa huduma zote hazitolewi zikiwamo za dharura ambazo awali ziliendelea kutolewa.
  Mmoja wa walinzi aliwambia waandishi wa habari kuwa, amefunga mageti kutokana na amri ya mkuu wake wa kazi.
  “Mimi ninatekeleza amri ya bosi wangu, amenitaka kufunga geti na hakuna mtu kuingia, awe mgonjwa au ninyi waandishi wa habari kwa kuwa hakuna huduma zinazotolewa humu,” alisema.
  Mkoani Mwanza
  Madaktari 63 walio katika mafunzo ya vitendo kazini wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Hospitali ya Mkoa Sekou Toure wametimuliwa na kurejeshwa wizarani kutokana na mgomo huo.

  Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dk Charles Majinge alisema kuwa, juzi aliwataka madaktari waliokuwa katika mgomo kurejea kazini, lakini hawakufanya hivyo na jana akaamua kuwarejesha 47 wizarani.

  Katika Hospitali hiyo ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure, Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Valentino Bangi alisema, madaktari 16 wamesimamishwa kufanya kazi kutokana na agizo la wizara.

  Kilimanjaro

  Madaktari walioko kwenye mgomo katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi mkoani Kilimanjaro walisema jana kuwa, kinachofanywa na Serikali kuwafukuza kazi waliogoma, ni njia mojawapo ya vitisho, lakini wakasema kuwa kamwe hawataogopa.

  Madaktari hao ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini walisema, wao wanaendelea na mgomo mpaka pale Serikali itakapotekeleza madai yao.

  “Tumesikia wenzetu wa Dodoma na Mbeya wamefukuzwa ….Hiyo haitufanyi turudi kazini na kama Serikali inaona hiyo ndiyo njia ya kumaliza mgogoro huu waendelee sisi tutarudi kazini pale itakapotimiza tunayotaka,” alisema mmoja wa madaktari hao.

  Mbeya

  Juzi Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, ilitoa tangazo la kuwataka madaktari waliopo mafunzoni waliogoma kurejea kazini jana, na endapo wangekiuka agizo hilo wangekuwa wamejifukuzisha kazi. Na hadi jana jioni hospitali hiyo ilikuwa imewafukuza madaktari 72.

  Ocean Road

  Katika Taasisi ya Taifa ya Saratani, (Ocean Road), kutokana na madaktari sita kusitisha kutoa huduma tangu Dk Ulimboka alipojeruhiwa kwa kipigo, waligoma na jana Mkurugenzi wa Tiba na Huduma Diwani Musemo alionekana akitembelea wagonjwa.

  Dodoma
  Madaktari 11 wa mafunzo kwa vitendo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma nao wamefukuzwa, tukio ambalo jana lilileta usumbufu mkubwa katika upatikanaji wa tiba hospitalini hapo.
  “Kwa hakika matibabu yanaendelea ingawa ni katika hali ya kusuasua. Hatuna uhakika kama kweli kuna mgomo wa chinichini au la, maana mimi nimefika mapema, lakini bado sijahudumiwa," alisema mmoja wa wagonjwa waliozungumza na mwandishi wa habari.
  Arusha
  Katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, huduma zimedorora lakini Mganga Mkuu, Dk Omar Chande alisema jana kuwa, imekuwa ni vigumu kuchukua hatua kuwabana madaktari ambao wanatuhumiwa kufanya mgomo baridi, kwani wote wanaripoti kazini.

  "Ni kweli kuna taarifa hizi za kuwapo mgomo baridi, lakini madaktari wote wapo kazini, ila kama kuna kufanya kazi chini ya kiwango, tumeanza uchunguzi," alisema Dk Chande.
  Amana

  Katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam utoaji wa huduma ulisuasua kutokana na mgomo huo jambo lililofanya uongozi kuweka tangazo kwenye Ofisi ya Mganga Mkuu kuwataka watumishi wote ambao hawakuwapo kazini kuanzia Juni 25, 2012 waandike barua za kurejea kazini.

  Tangazo hilo pia linawataka madaktari walioko mafunzoni kuandike barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia kwa mganga mkuu wa hospitali hiyo.

  Habari hii imeandaliwa na Frederick Katulanda, Mwanza, Rehema Matowo, Moshi, Zakhia Abdallah (SJMC), Editha Majura, Israel Mgussi, Dodoma), Victoria Mhagama na Daniel Mwingira, Sam Jacob na Issa lazaro (SJMC, Godfrey Kahango, Mbeya, na Mussa Juma, Arusha.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 8. m

  mpepalilambo Senior Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  jambawazi na siasa wapi nawapi? Ubabaishaji mtupu
   
 9. n

  nndondo JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Na ataje tu hatuna sababu ya kusubiri lolote, na pili naomba tafadhali nirudie madaktari wateua wajumbe wa tume yao iunganike na waandishi mahiri wa investigative reporting wafanye utafiti na kutoa matokea, mimi najitolea kuwemo kwenye tume hiyo na haraka sana matokeo yatolewe kwa kupitia press conference. Tunaomba hamasisheni marafiki zetu wote wa ndani na nje kwa kazi hii
   
 10. a

  adolay JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Subira yavuta kheli, kama lema anao ushahidi pasipo kuacha masha basi na awataje, kama hana bora kunyamaza, wapuuzi huko serikalin wanatafuta pa kuficha aibu. wanasubili mtu ajichanganye waendeleze ufashit na udikiteta wao. Hawanason kwao wauwaji na mafisadi huitwa makada.
   
 11. m

  mpepalilambo Senior Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  toka lini jambazi akaweza siasa? Kama ni jembe lenu kweli basi hamna watu.
   
 12. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  bora nngezaliwa afghanstan kwenye vita kuliko huku kwenye uuaji wa wazi unaofanywa na serikali
   
 13. d

  dguyana JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa ni Mafia haogopi ndio maana JK anamgwaya pia. Big up Lema go go go Lema
   
 14. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu ni bonge la jambazi hata zile pesa kule bank za uswisi ni zake alituibia hata ujambazi wa EPA na Rada alishiriki kweli lema ni jambazi la kimataifa
   
 15. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Kamanda anajua siri zote za ccm hata swala la kuwekwa kura kwenye chupa za chai arumeru yeye alitoa ile siri ndo nasema serikal inahusika kwa 99.9%
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kamanda rejea walaka wa lema kwenda kwa dr dr dr Kikwete

  [​IMG]

  "
  Ndugu Wananchi;

  Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo
  . ( J.K . KIKWETE.)

  "Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge".

  Mh Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha .

  Mh Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa dhidi ya haki , utu na ukweli.

  Mh Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni
  "Afadhali Vita Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu " umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama chako , hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi ya kebehi na hadaa , Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea Zanzibar , mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .

  Mh Rais , Mama Theresa , Nelson Mandela , Martin Luther Jr na Malcom X hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao , sihitaji Ubunge kupigania ukweli, haki na utu , nahitaji dhamira safi , nia njema na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini , nitakapomaliza mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini nilifanya , ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta , magorofa , magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki ,Usawa na utu vikiwa kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo, pengine sitaishi miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi , Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe , hata hivyo siogopi kufa kwani nisipokufa kesho , nitakufa siku moja ambayo siijui , napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama itawezekana , lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora ishindakane kwa kuthamini haki , kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana , unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako , niko tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu watu wa Arusha Mbunge wao.

  Mh Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli katika Jimbo langu na Nchi yangu.

  Mh Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na haki na ukweli .

  Mh Rais
  "Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri" Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .

  "
  ONLY TIME WILL TELL".

  Tafakari chukua hatua
   
 17. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 842
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
   
 18. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  mimi toka Mwakyembe ataje maofisa wa serikali waliokuwa wamepangwa kumuua na kutoa ushahidi wa aina ya magari na namba waliyotumia na ni nani kawapokea na ni wapi walishukia na akaweka wazi kuwa yupo tayari kuisaidia polisi zaidi kama atahitajika, sina tena imani na hii serikali anymore. Nikikumbuka pia issue ya Bilali, Zombe na kesi ya Mahanga, ni dhahiri na haki kabisa kwa serikali ya ccm kusulubiwa.
  .
   
 19. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Suala la Dr Ulimboka unamsubiri Lema akuambie wakati inajulika wazi ACP Hemed Msangi ndiye mhusika mkuu.
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa nini nynyiemu mnam-hara huyu Lema. Akitamka kitu tu matumbo yenu yatonanayo na mapesa ya ufisadi yanaendesha na mnakimbilia chooni.

  Walafi wakubwa. Jambawazi Na 1 ni Mkuu wa Kaya, ndiye alipotufikisha hapa tulipo.
   
Loading...