Lema kuapa mara mbili Bunge la muhula mmoja?

Makene

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
1,475
Reaction score
282
je wadau baada ya Lema kushinda kesi na kurudishwa kuwa mbunge wa Jiji la Arusha, je atahitajika kuapa tena mara ya pili, au kiapo chake cha awali kitaendelea?
 
Tusibiri wenye kujua taratibu lakini sidhani kama ataapa tena kwani mahakama imefanya kumrudishia alichoporwa tu. Nadhani ndio hivyo bali sina uhakika
 
Lazima aape, maana alivuliwa ubunge na mahakama halali, na si kuporwa kama mdau mmoja alivosema.
Hii haijalishi kama alionewa au kutoonewa.!
 
Kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa kama uchaguzi ungerudiwa na kuibuka mshindi ndo angeapishwa tena. Lakini kwa kuwa ameshinda kesi hivyo itakuwa ni kurudi mjengoni kama ilivyokuwa kwa Mnyika au Tundu Lissu.

Ila nasikitika kwani ile movement ya Live or Die ambayo ilitakiwa kuanza mwakani itapungua nguvu kwani kamanda Lema atakuwa kwenye majukumu ya kibunge.
 
Lazima aape, maana alivuliwa ubunge na mahakama halali, na si kuporwa kama mdau mmoja alivosema.
Hii haijalishi kama alionewa au kutoonewa.!

Mkuu, Lema ameshinda na ni sawa na mtu aliyefungwa kisha kupoteza haki zake za mingi kama raia wa Tanzania na akikata rufaa na kushinda hurudishiwa haki zote ikiwa ni pamoja na kuwa kiongozi serikalini.
 
Hataapa tena. Nafasi yake haikuwahi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwamba iko wazi wala Spika hakuwahi kuiarifu hivo Tume. Namshukuru MUNGU kodi zetu hazitateketea kwa uchaguzi mdogo ambao ungekuwa mama ya chaguzi ndogo zote na matokeo yangekuwa ni yaleyale.
 
Nijuavyo lema ataendelea na ubunge wake kama kawaida ikiwa ni pamoja na kupata mshahara wake wote tangu avuliwe kwa makosa.ama sivyo tutajua zaidi kitakachoendelea..
 
Lazima aape, maana alivuliwa ubunge na mahakama halali, na si kuporwa kama mdau mmoja alivosema.
Hii haijalishi kama alionewa au kutoonewa.!

Kwa maana hiyo kwa muda huu Lema ni Mbunge Mteule wa Arusha? Naomba kufahamishwa wakuu.
 
Vp kuhusu mafao yake ?

Mkuu mafao ni kitu kidogo sana kulinganisha na aliyoyafanya akiwa nje ya Bunge. Sidhani kama yeye anafikiria hicho kitu; wampe, wasimpe cha moto wamekiona.
 
Lema hawezi kuapa, uamuzi wa mahakama unatambuliwa, si na mahakama ya chini pekee bali ya rufani. Kwa kitendo cha kumtangaza kuwa ni mbunge halali, maana yake 'mahakama' imeamua. Kwa hiyo hakuna kuapa tena. Mafao yake yote atapata, na ikibidi haki nyingine zote maana alikoseshwa kwa makosa.
 
Hataapa tena. Nafasi yake haikuwahi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwamba iko wazi wala Spika hakuwahi kuiarifu hivo Tume. Namshukuru MUNGU kodi zetu hazitateketea kwa uchaguzi mdogo ambao ungekuwa mama ya chaguzi ndogo zote na matokeo yangekuwa ni yaleyale.

Kwa maana hiyo ni sahihi tukisema ubunge wake haukuwahi kukoma? Kama uliwahi kukoma, nijuavyo mimi yeyote anayeingia bungeni akitokea "uraiani" anapaswa kuapa. Kama haukuwahi kukoma, kuna tatizo kwenye sheria zetu. Naamini Magwiji wetu wa Sheria wakiongozwa na Kamanda machachari Mh. Tundu Lissu wataliweka vizuri huko mjengoni.
 
na mimi nilikua najiuliza hili swali, kidogo nimeweza kuelewa ufafanuzi wako..
 
Kama angeshindwa kesi Mahakama ya rufaa leo then akaamua kugombea tena baada ya NEC kutangaza Jimbo hilo la Arusha lipo wazi na KUSHINDA uchaguzi huo mpya LEMA ingebidi aape tena!

Lkn baada ya kuvuliwa Ubunge na Mahakama kuu kanda ya Arusha na yeye kukata rufaa Mahakama ya rufaa na kushinda LEMA HAWEZI KUAPA TENA bali ofisi ya Bunge ikitumiwa nakala ya hukumu ya leo Spika atatoa tu mwongozo wa kumrudisha kwenye kamati alizomteua za Bunge na siku ya kwanza ya Lema kuingia Bungeni spika atatoa tu mwongozo wa kumkaribisha tena bungeni!

Huwezi kuapa mara 2 kwenye bunge hilo hilo AMBALO halijavunjwa na Rais kupisha uchaguzi mpya wa ndani ya katiba!!

Kuhusu Malipo:Lema hakuwa anafanya kazi za kuwawakilisha wakazi wa Arusha hivyo HAWEZI PATA HATA SENTI kipindi kavuliwa Ubunge wake;Lema ataanza kupata malipo yake wakati kamati za Bunge zitakapo anza kukutana kabla ya kikao cha kawaida cha Bunge!
 
Lema hawezi kuapa, uamuzi wa mahakama unatambuliwa, si na mahakama ya chini pekee bali ya rufani. Kwa kitendo cha kumtangaza kuwa ni mbunge halali, maana yake 'mahakama' imeamua. Kwa hiyo hakuna kuapa tena. Mafao yake yote atapata, na ikibidi haki nyingine zote maana alikoseshwa kwa makosa.

Asante Mkuu kwa ufafanuzi. Hapo kwenye red; ni baadhi tu ya haki na sio zote kwani mambo mengine hayawezekani. Kwa mfano, haki yake aliyopotozewa ya kuwasemea wananchi wa Arusha kwa kipindi alichokosa vikao vya Bunge haiwezi kurudishwa tena na hii ndio ya msingi kuliko hata hayo mafao na mishahara.
 
Kama angeshindwa kesi Mahakama ya rufaa leo then akaamua kugombea tena baada ya NEC kutangaza Jimbo hilo la Arusha lipo wazi na KUSHINDA uchaguzi huo mpya LEMA ingebidi aape tena!

Lkn baada ya kuvuliwa Ubunge na Mahakama kuu kanda ya Arusha na yeye kukata rufaa Mahakama ya rufaa na kushinda LEMA HAWEZI KUAPA TENA bali ofisi ya Bunge ikitumiwa nakala ya hukumu ya leo Spika atatoa tu mwongozo wa kumrudisha kwenye kamati alizomteua za Bunge na siku ya kwanza ya Lema kuingia Bungeni spika atatoa tu mwongozo wa kumkaribisha tena bungeni!

Huwezi kuapa mara 2 kwenye bunge hilo hilo AMBALO halijavunjwa na Rais kupisha uchaguzi mpya wa ndani ya katiba!!

Kuhusu Malipo:Lema hakuwa anafanya kazi za kuwawakilisha wakazi wa Arusha hivyo HAWEZI PATA HATA SENTI kipindi kavuliwa Ubunge wake;Lema ataanza kupata malipo yake wakati kamati za Bunge zitakapo anza kukutana kabla ya kikao cha kawaida cha Bunge!

Well said!
 
Wakuu hizo kampeni za chadema kama hiyo ya live or die zina utata sana kwani wadau wanalalamika kua zina anzishwa juu na wakubwa halafu huku chini kwenye mashina hali ngumu hakuna pesa wajumbe na viongozi wa chini wanakata tamaa wakati chama kinapata ruzuku ya kuridhisha tu napenda kuwakumbusha chadema kua nyumba bora huanza na msingi imara endapo kama wataendelea kuyasahau mashina yao itakua sawa na kutwanga maji kwenye kinu
 
Kwa maana hiyo ni sahihi tukisema ubunge wake haukuwahi kukoma? Kama uliwahi kukoma, nijuavyo mimi yeyote anayeingia bungeni akitokea "uraiani" anapaswa kuapa. Kama haukuwahi kukoma, kuna tatizo kwenye sheria zetu. Naamini Magwiji wetu wa Sheria wakiongozwa na Kamanda machachari Mh. Tundu Lissu wataliweka vizuri huko mjengoni.
Ubunge unakoma pale Tume ya Taifa inapotangaza Jimbo liko wazi baada ya kuarifiwa hivo na Spika. Ndio maana akina Kafulia na Hamad Rashid bado ni WABUNGE pamoja na kufukuzwa kwenye vyama vyao.
 
Back
Top Bottom