Lema kuapa mara mbili Bunge la muhula mmoja?

Lema kuapa mara mbili Bunge la muhula mmoja?

La kujiuliza hapa ni hili: Ni hatua gani UONGOZI wa juu wa MAHAKAMA unachukua kwa Majaji wanaotoa hukumu za hovyo kama hii ya Mahakama Kuu ya Arusha ambayo sio tu imewakosesha muwakilishi Bungeni wapiga kura wa Jimbo la Arusha bali pia imeligharimu TAIFA mapesa mengi.

Sio ajabu hata kidogo ukamkuta Jaji kama huyu anateuliwa kuwa Jaji Kiongozi au Jaji wa Mahakama ya Rufaa teuzi zijazo za Rais wetu! Bodi ya KITAALUMA inahitajika sana kwa WANASHERIA wetu.
 
tunashukuru mahakama ya rufaa kwa kutenda haki kwa Mh Lema na CDM na kwa wapenda demokrasi ya kweli, pili Mahakama ya rufaa , imeliepushia taifa gharama za kufanya uchanguzi mdogo mwingine ambao ungetumia pesa nyingi ambazo zingetumika kufanya mambo mengine ya maendeleo ktk jamii na taifa kwa ujumla,
 
Vp kuhusu mafao yake ?

hakuna mafao yeyeto ambayo atapata ila baada ya lema kushinda rufaa yake na hivyo basi kurudishwa bungeni , atastahili kulipwa mishahara yote aliyokosa baada ya kuvuliwa ubunge, pia atalipwa posho zote za vikao vya bunge ambazo nazo hakupata kutokana na yeye kushindwa kuhudhuria bungeni kutokana na kuvuliwa ubunge posho ambazo wabunge wenzake walikuwa wanazipata baada ya kusaini kitabu wale waliokuwa hawahudhurii bungeni walikuwa hawapewi lakini kwake itakuwa special case kutokana alikuwa haudhurii kutokana na kuvuliwa ubunge kimakosa na mahakama kuu h
 
je wadau baada ya Lema kushinda kesi na kurudishwa kuwa mbunge wa Jiji la Arusha, je atahitajika kuapa tena mara ya pili, au kiapo chake cha awali kitaendelea?
hatahitaji kuapa tena yeye alishaapishwa kama mbunge na mahakama ya rufaa imemrudishia haki yake iliyoporwa na mahakama kuu
 
Lazima aape, maana alivuliwa ubunge na mahakama halali, na si kuporwa kama mdau mmoja alivosema.
Hii haijalishi kama alionewa au kutoonewa.!
hatahitaji kuapa kwa sababua alishaapa kuwa mbunge, na kwa sababu mahakama ya rufaa imemrudishia kwenye nafasi yake ya ubunge ambayo alivuliwa kutokana na mkosa ya learned brother justice aliyeamua kumvua ubunge. Ndugu embu pitia kidogo mwenendo wa kusikiliza mashauri ya rufaa, kwa kifupi rufaa yeyote lazima isikilizwe na mahaka ya juu ya ile iliyotoa hukumu, kama ilikuwa mahakama ya mwanza lazima rufaa ipelekwe mahakam ya wilaya.
Pia uamuzi wa mahakama ya juu inayosikiliza rufaa ni wa aina 2 tuu kwanza ni kukubaliana na hukumu iliyotolewa na mahakama ya chini na pili ni kuikataa hukumu na kuitupilia mbali na yule mtuhumiwa kuachiwa huru na kuendela kama vili kulikuwa hakuna hukumu yeyote iliyotolewa hivyo basi kwenye suala hili la lema baada ya mahakama ya rufaa kuikubali rufaa ya lema na kutupilia mbali hukumu ya mahakama kuu iliyotengua ushindi wa Lema, Mhe Lema anaendelea kuwa mbunge as if kulikuwa hakuna kesi dhidi yake so hastahili kuapa tena kwa sababu amerudishiwa haki yake aliyokuwa nayo.
 
kuna lingine, wana-Arusha hawakuwa na nafasi ya mawazo yao kuwakilishwa bungeni, hivyo mchango wao ulikoseshwa kutolewa kutokana na mwakilishi wao kuondolewa hadhi ya kuingia bungeni kushiriki mijadala mbali mbali. Je wana Arusha waishitaki mahakama kuwanyima haki yao ya kikatiba ya kusikilizwa mahitaji yao? Tuendelee kuchangia..
 
Hili lako makene, la kutowawakilisha wananchi bungeni kwa muda wote, nadhani waliupata uwakilishi kupitia kwa makamanda wengine. Hoja nadhani ni ya kupeleka mapendekezo ya sheria ya kuwakamua mahakimu na majaji wanaotoa hukumu za kihuni. Wanaleta mtafaruku, hasara na kuwakosesha wananchi haki yao ya kuwakilishwa.
 
Hawezi kuapa tena maana hukumu ya mahakama ya rufaa inatengua hukumu ya mahakama kuu. Kitakachotokea ni Lema kurudi bungeni bila kuapa tena na kulipwa mishahara yake yote. Ni sawa na mtu aliyesimamishwa kazi halafu baadaye akaja kugundulika kwamba hakuwa na hatia. haajiriwi upya bali hurudi kazini na kulipwa mishahara yake yote. Kuhusu la pili ni kwamba kama kuna watu wa kuwashtaki ni wale waliomfungulia kesi Lema na si Mahakama.
 
Kwa kuwa mheshimiwa Lema alifutiwa ubunge wake na kwa kuwa mamlaka iliyomvua ubunge ni mamlaka halali, na kwa kuwa hakusimamishwa ubunge bali alivuliwa na hiyo kumwondolea haki ya kuhudhuria vikao halali vya bunge, basi hii ina maana kuwa leo mahakam ya juu ambayo ina mamlaka kisheri imemrudishia ubunge wake na hivyo itampasa kuapa kama spika ataona kwa kufanya hivyo havunji kanuni za bunge. Endapo angekuwa amesimamishwa ubunge wake na akashinda ina maana atakuwa na haki ya kudai hata mishahara yake yote lakini alivuliwa kwa hiyo hana haki hiyo. Leo alikwenda mahakamani kama Ndg. G. Lema akarudi nyumbani kama Mh. G. Lema. Nimeeleweka mkuu?
 
Kuhusu Malipo:Lema hakuwa anafanya kazi za kuwawakilisha wakazi wa Arusha hivyo HAWEZI PATA HATA SENTI kipindi kavuliwa Ubunge wake;Lema ataanza kupata malipo yake wakati kamati za Bunge zitakapo anza kukutana kabla ya kikao cha kawaida cha Bunge![/QUOTE]

Mkuu Kwani alishindwa au alikataa kuwawakilisha watu wake au ni majaji walimkatalia? Maana hapakuwa na sheria sahihi iliyotumika kutengua ubunge wake inapaswa alipwe maana badala ya kuwakilisha watu wake jimboni ilibidi aanze kushughulikia maswala ya sheria kudhibitisha usahihi wa kuchaguliwa kwake kuwawakilisha wananchi wake. Sasa iweje leo kwamba eti asilipwe? Na kama ni hivyo basi CCM watakuwa wanawafanyia hivyo wapinzani kila baada ya uchaguzi. Kama kweli ndivyo ilivyo Mkuu basi sheria zetu ni dhaifu!
 
La kujiuliza hapa ni hili: Ni hatua gani UONGOZI wa juu wa MAHAKAMA unachukua kwa Majaji wanaotoa hukumu za hovyo kama hii ya Mahakama Kuu ya Arusha ambayo sio tu imewakosesha muwakilishi Bungeni wapiga kura wa Jimbo la Arusha bali pia imeligharimu TAIFA mapesa mengi.

Sio ajabu hata kidogo ukamkuta Jaji kama huyu anateuliwa kuwa Jaji Kiongozi au Jaji wa Mahakama ya Rufaa teuzi zijazo za Rais wetu! Bodi ya KITAALUMA inahitajika sana kwa WANASHERIA wetu.

Nilkuwa nawaza sana kuhusu hoja ya Mh. Tundu Lisu kuhusu uteuzi wa majaji. Sasa je? Serikali imekiri kuwa kweli wana majaji vihiyo? Maana kesi ya Lema ameisimamia yeye mwenyewe! Tusemeje sasa?
 
Back
Top Bottom