Lema kaka yangu nikufarijije? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema kaka yangu nikufarijije?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MARCKO, Jun 5, 2012.

 1. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama Mungu yupo, kweli atakua anaona dhamira yangu dhidi yako kaka yangu. Nimekua nikifikiria sana kwamba kwa matatizo yaliyoikuta haki nchi hii katika jimbo lako yanaweza kukufanya ukajutiat kuwa mkweli na mpambanaji dhidi ya udhalimu wenye ncha kali namna hii kaka yangu!

  Kukuambia usiogope, pole, usisikitike, usihuzunike, hongera, na mengine mengi naona kama haitoshi!!. Wakikutana viongozi wawili au watatu wa serikali kwa ngazi yeyote kupitia CCM, wanasemezana namna ya kuondoa makucha ya Lema shingoni mwa ccm.

  Na kwa jinsi ulivyo chimbia makucha, kukutoa itakugarimu kama ulivyohisi tayari ili kunusuru CCM. Garama utakazoingia nipamoja na kutoa milimita nyingi za hymoglobine kuloanisha udongo au sakafu kaka yangu!

  Mimi nimeajiriwa na hii serikali ila umenijaza hasira mpaka nafikiria kuacha kazi niingie kwenye harakati za kukutetea wewe pamoja na wanasiasa wengine walio hatarini. Usirudi nyuma, maliza safari yako kishujaa, kwani hata ungaliishi miaka 100, usingaliepuka mauti ndugu yangu lema!

  Wanakuogopa kama panya wengi kwa paka mmoja kwa kapaka kadogo kamoja. Endelea kufuta tabasamu lako kwa 'injustices tanzania' maana sasa wanalaumu mama alokuzaa! ¤wana jf just say (yes or no) to this topic.
   
 2. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Its true that Lema ni mpambanaji wakweli Tanzania hii.
   
 3. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni kweli tuko nae bega kwa bega mh Lema, tunajua njama zinazofanywa na ccm ili kukukwamisha. Hakika nguvu ya MUNGU itawashinda na wataaibika. HAKI YA MTU HAIWEZI KUPOTEA ILA ITACHELEWESHWA.
   
 4. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,078
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  Lazima watu kama hawa vitabu vya kumbukumbu ya maisha yao viandikwe. Go Lema.
   
 5. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  to become a man is a reward.
   
 6. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Lema bana ana maneno maneno huyu
  "Unaweza kufanya ngono - kuzini - sirini, lakini huwezi kuugua ukimwi sirini"
  "Wao wana fedha na usalama wa taifa na polisi na jeshi, sisi tuna Mungu na watu"

  nyingine naomba mniongezee...
  hayo ni maneno au falisafa nzito sana ukiamua kuzitafakari na kuziishi

  Tanzania, na haki kwa jamii kwanza
  Mungu atakupigania tu mzee
   
 7. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Eti Lema mpambanaji, kwa lipi hasa hadi aitwe mpambanaji?.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 8. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tumuombee maisha marefu jamaa mbinu zingne zishafail.
   
 9. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Ushabiki mwingine wa KIJINGA kweli!!! Sasa unadhani nani atakusifu kwa ujinga huu? Kama unaona Lema siyo kitu kwako, ni KITU kwa wengine. Kwani lazima uchangie kila kitu? Watu wengine bana....au unatutafutia ban???? Lala kama umechoshwa na maisha magumu ya CCM na watawala wake!!!
   
 10. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Jf is the place where we dare to talk openly. We unataka nimpende ili nikuridhishe? naandika kile kilicho moyoni mwangu.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 11. t

  tara Senior Member

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naomba kuuliza kama magogoni washamjibu kamanda Lema waraka alioandika..
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,566
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Ukweli wa Lema ni upi?

  Kusema mwanamke yule kapewa mimba na fulani? acheni ujinga msifikiri hizi ni mbao za matangazo ya ushabiki

  Lema is just another disaster in this country1

  siku zote akina mama wajawazito wanaheshimiwa , unasimama jukwaani unasema alipewa mimba na yule...badala ya kuuza sera za CHADEMA? halafu ndiye hero wenu?

  kama alilipenda jimbo alitakiwa kuwa makini na domo lake, after all mahamaka imejisafisha, mbona sehemu nyingi tu CHADEMA wameshinda?

  hivi nyie wenzetu akili mmeweka wapi?? kuweni realistic ujinga wa ushabiki huu ndio umeifanya CCM iwe hivi leo...use sense lets your parents feel they have you!!

  Kumbuka hii ni JF great thinking na hoja tu!
   
 13. m

  mandemba Senior Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Basi wasira,
   
 14. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Lema anganyamaza tu ..anakuwa kama Maige bwana
   
 15. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Pamoja na hoja zako hizi zako zote hizi Wabes, sehemu moja unaposhindwa kujipambanua nikuwa ni kiasi gani gani unatarajia mambo kamilifu wengine wanaweza kuwa nayo katika harakati hizi mkuu.

  Naamini katika mapungufu yetu kama watu hapo ndio ninapomsamehe Lema ila wewe na Ngongo mna-muhukumu, kuna point nyembamba sana mnaipuuzia kuwa level ya inteligency haiwezi kuwa sawa kati ya Lema na Mnyika au na Zito ila michango yao inaweza kulingana kutokana na aina ya siasa ya nchi yetu na watu wetu ila yote katika kujenga chama cha demokrasia na maendeleo (rejea harakati za M4C toka ziasisiwe).

  Kwa point hii si sawa Wabes, ni lazima mrejee kwenye harakati za ujenzi wa Afrika huru enzi zile naomba mnitajie kiwango cha elimu cha Zuma na mchango wake kwa ANC.

  Kwanini leo hii mnataka kulazimisha Lema awe sawa na zito au mnyika wakati na nyie ni Great Thinkers pia?
  Unataka tuwe realistic? Sawa, hivi ni kweli kweli hujaona jema la Lema hata moja kweli? Naomba uniambie kuhusu msisimuko wa watu wa Atown na siasa za Atown umesababishwa na nini? Najua utataja factors zote ila ya mwisho lazima iwe Lema!

  Wakuu mnaomchukia Lema lazima tukubaliane kuwa hizi ni siasa za Africa mwisho wa siku, sio haki kumpima kwa vipimo vya siasa za ulaya au America. Hebu tumpime kwa siasa za africa na sana Tanzania kwa kuzingatia uzoba wa watu wake na wa historia yake.

  Hapa namaanisha katika kujenga siasa za harakati na kuwaamsha watu hawa kutoka kwenye huu uzoba na kulala (tunataka mtu wa namna gani?? Mi hapa naamini watz wanataka kiongozi wa mfano, sijui nyie)

  Najua siwezi kukushawishi wewe na Ngongo juu ya hili sababu watz kwenye hizi forums huwa tuna tabia za kuweka ligi ili usionekane umefunikwa ila mjue kuwa pamoja na chuki zetu juu ya CCM, ila kuna masuala tumeamua kusamehe na kuayachukulia kuwa yalikuwa ni makosa ya taifa (Tukirejea yote ya TANU).

  Namaanisha makosa ya TANU yalikuwa makubwa kuliko nyie mlivyoamua kumtundika Lema msalabani kwa makosa yake!!

  Mnasahau kuwa hamna mkamilifu kati yetu sababu tu ya ubinaadamu.

  Kwenye harakati za ukombozi wa taifa tunatafuta watu wenye manufaa kwenye eneo fulani na sio wenye mapungufu kwenye maeneo yote kama mnavyotaka kutuaminisha kuhusu Lema.

  Mapungufu ya Lema nayachukulia kama mapungufu ya kibinaadamu ambayo tukitaka kuchimba tutayapata kwa kila mtu hata hao mnaowaaminia nyie.

  Bado sijaona sababu ya kumtundika Lema msalabani kwenye harakati hizi zangu za mwisho!
   
 16. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu ambariki sana
   
 17. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mapambano bado yanaendelea, hakuna kulala
   
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  kwenye kila jambo kuna jambo jema na baya nafikiri yale mazuri huwa yanatutia moyo n yale mabaya ndizo changamoto. Mimi sishabikii chama but ukweli Lema kuna mazuri sana aliyofanya hasa uhamasishaji wa siasa miongon mwa wana ARUSHA na kwingineko Tz lakini pia yapo ambayo huwa anakosea kama binadamu. Ila yeye ni binaadamu tusitegemee yaliyo mazuri tu toka kwake hata mabaya pii manake he is not an angel.

  kwangu mimi Mungu amuongezee hekima zaid ili katika siasa hizi basi amwishie yeye na siyo binadamu mwenzie. Kwa yeye kuwa mcha Mungu lazima apate upinzani sana tena amkumbuke Daudi n wengine.
   
 19. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,775
  Trophy Points: 280
  May God bless GodBless Lema.
   
 20. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lema akinyamaza basi hayo mawe yatapaaza sauti
   
Loading...