Lema chupuchupu kutiwa nguvuni...

Lema chupuchupu kutiwa nguvuni...

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
3,098
Reaction score
631
Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema jana alinusurika kukamatwa na makachero wa Jeshi la Polisi ili kuhojiwa kutokana na ujumbe wake aliouposti kwenye mtandao wa kijamii akiandika: “Rais Kikwete mbona umeamua kuliangamiza taifa.”

Akizungumza na gazeti hili jana akiwa njiani kuelekea Dodoma kushiriki Kikao cha Bunge la Katiba, Lema alisema maafisa wawili wa polisi walimfuata katika hoteli aliyofikia Dar es Salaam kwa lengo la kumkamata na kumpeleka makao makuu ya polisi.

Lema alisema maafisa hao, ambao walikuwa wanatumia gari dogo, baada ya kufika hotelini hapo, waliomba aitwe na aliposhuka walimtaka kuandamana nao, hadi makao makuu ya polisi kwa mahojiano.




lema+px.jpg
 
Serikali inayonuka harufu ya damu inataka kumg'oa meno na huyo?
 
Serikali inayonuka harufu ya damu inataka kumg'oa meno na huyo?

Hapa ni ngumu saaaana, polisi mtu mbili hawawezi kumteka Lema.
Mutu ya Ar tunajielewa tuko vizuri nje ndani, wakahangaike na misukule ya kupewa Wali na kanga
 
Hivi Lema mbona huwa hasikiki akichangia hoja mbalimbali za kimaendeleo Bungeni au hata
nje ya Bunge????
 
Ukweli unauma eeh? Huyo muikulu afute kauli yake aliyowaambia wanachama wa CCM juzi pale Dodoma.

Tanzania tunahitaji kiongozi na siyo mtawala.
 
Hao jamaa itakuwa siyo POLISI, ingekuwa wenyewe wameamua kumkamata wangempata tu. Huku ni kuwatafutia biashara wachapishaji wa magazeti kwa kutengeneza HEADINGS zenye ----- wa habari ndani yake.
 
Ukweli unauma eeh? Huyo muikulu afute kauli yake aliyowaambia wanachama wa CCM juzi pale Dodoma.

Tanzania tunahitaji kiongozi na siyo mtawala.
Huyu Lema inabidi mumfundishe jinsi ya kuongea mbele ya jamii..
 
Alinusurika kukamatwa kivipi...? kwani ukinusurika unajificha ua vipi...kukamatwa si unakamatwa popote....sema alinusurika kutekwa
 
Hivi Lema mbona huwa hasikiki akichangia hoja mbalimbali za kimaendeleo Bungeni au hata
nje ya Bunge????

kwani radio ya matahira huwa inatamka jina la lema..jitahidi kufatilia bunge kupitia tv na radio za watu waliojitambua uone pinda anavyomuanya mbungeni...
 
Back
Top Bottom