Juzi nilileta thread humu JF kuhusu huo mradi nakauliza Lema, naye anahusika sikupata jibu sahihi..
Leo ndio nimepata jibu, hivi huo mradi ni wa Chadema au CCM? huo mradi ni kwa manufaa ya wana Arusha.
Nashangaa Lema kujipa majukumu ya Shekh Yahaya utabiri
Mh. Lema kubali maendeleo yaje kwa faida ya wengi; hizo guest house za Kaloleni zina tija kidogo sana kwa uchumi wa jiji letu la Arusha
amekueleza kuwa yeye hapingi maendeleo,anachopinga ni jinsi mchakato unavyokwenda,jamani muwe mnasoma na kuelewa msikurupuke tu anachodai mbunge ni jinsi swala zima linavyopelekwa bila kuwashirikisha wananchi wa eneo husika,wapi wanatakiwa kwenda,watalipwa sh ngapi na kwa mtindo upi,sasa mkuu husomi na kuelewa lakini Mkurugenzi lazima awe makini,huwezi kuanza project fulani ktk makazi ya watu bila wao kuhusishwa na hata mbunge wao hajui nini kinaendelea huo ni usaliti tena usaliti wa hali ya juu,hata sisi tusio na vyama hatuwezi kukubaliana na hili la mkurugenzi
Heshima kwenu wanajamvi,
Ni vyema kabla ya kuchangia hoja ukajiridhisha kujua unachopinga au kuunga mkono.
Ninaijua Kaloleni,nina marafiki ndugu na jamaa wanaishi kwenye hizo nyumba za Kaloleni.Mheshimiwa Mbunge Lema katoa sababu za kuupinga mradi ambazo kama ni kweli wa kwanza kulaumiwa ni yeye mwenyewe na chama chake kwa kutoweka maslahi ya wapiga kura na wananchi kwa ujumla wake.CDM ilikuwa na nguvu kubwa kwenye baraza la madiwani huu mradi usingepita kama wasingefukuza madiwani watano na kutoa nafasi kubwa madiwani wa CCM kutoa maamuzi makubwa kwakuwa idadi yao ni kubwa.Ikumbukwe pia CDM walikuwa mabingwa wa kususa vikao vya baraza hapo hapo ni mabingwa wa kuvuta posho again Mheshimiwa Lema alitakiwa ajue athari za kususia vikao.
CDM ilishinda udiwani kata ya Kaloleni suala la nyumba za Kaloleni ambazo kuna kipindi zilimilikiwa na NHC na baadaye kurejeshwa Manispaa linajulikana muda mrefu upo umoja wa wakaazi wa hizo nyumba unaowashirikisha wakaazi wa Kaloleni,Kilombero na Fire Mwenyekiti wake ni Bwana Ole Kashiro na Katibu Mzee Shemdolwa.Mheshimiwa diwani wa CDM Charles "Rasta" alishinda kwa ahadi ya kuwasaidia wakaazi wa hizo nyumba kuuziwa kama walivyouziwa wenzao wa Ngarenaro pia watumishi wa serekali nao pia waliuziwa nyumba maeneo ya Sanawari na Uzunguni.Bahati mbaya ugomvi wa CDM ukamuondoa katika nafasi yake ya udiwani.Mpaka sasa Kaloleni haina diwani kwa maneno rahisi wananchi wa Kaloleni wamenyimwa haki yao ya kuwakilishwa na CDM.Niseme kweli sijui kama huo mradi umegubikwa na ufisadi au ni mbinu za wanasiasa kuchafuana.
Mheshimiwa Lema kama anazo hoja za msingi ni vyema akaziwakilisha kunakohusika eg TAKUKURU au Mahakamani.Ningependa kusikia mbunge wangu akitumia njia sahihi kupinga huo mradi ingawa ni lazima pia ajue nyumba husika hazikidhi viwango vya kisheria kuwapo eneo la Kaloleni.Ukitaka kujenga nyumba eneo la kaloleni ni lazima ujenge ghorofa tatu na kuendelea sasa sijui kama wakaazi wa hizo nyumba wanauwezo wa kujenga ghorofa tatu ?.
Lemaaaaa!!!
Kuna waziri mmoja (jina kapuni) alipewa majisifa sana... na yeye akayafurahia sana; ila muda unavyoenda ngoma inaelekea kupasuka... Even you, kama ukiendelea kufurahia magazeti kukuandika na kusifiwa sana e.g. na wana JF, iko siku ngoma itapasuka... Haya kaka yangu, yangu macho....
Nimewahi kusema tuna tatizo Tanzania, our leaders they are not looking at big picture!!! hilo suala ya kushirikisha wananchi is not about mbunge au mkurugenzi ni jambo la kisheria.... tuache kujadili upupu humu ndani.... sheria inasema lazima tathmini ifanywe na fair compensation ifanyike so what are we discussing here!!! yasipofanyika haya sheria lazima itachukua mkondo wake... sio suala la Lema vs Mkurugenzi.. amkeni waTanzania.
Hana lolote longo longo tu Mbunge porojo
Mkuu nakuunga mkono kwa ushauri wako. Sijui kama unaishi Tanzania au uko ughaibuni. Tanzania, TAKUKURU yetu inashughulikia mahakimu wanaohongwa Tshs 50,000 kule mahakama za mwanzo. Haiwezi kushughulika na mafisadi hasa kama hiyo issue ina mahusiano na CCM. Mahakama inashughulika na wezi wa kuku na bata na kidogo wabakaji. Issues muhimu na kubwa huwa hazishughulikiwi na mahakama zetu maana zote zimechukuliwa na mafisadi. Kama huamini kawaulize wawekezaji wakubwa wote hapa Tanzania, huwa wanahakikisha dispute zote kwenye mikataba yao zipelekwe kwenye mahakama za kimataifa.
Labda Lema naye aende huko kwenye court za kimataifa ila wote tunafaham kuwa hakuna mahakama imara kama ile ya wananchi ambao ndo Lema amewafikishia habari wajiandae.
Heshima kwenu wanajamvi,
Ni vyema kabla ya kuchangia hoja ukajiridhisha kujua unachopinga au kuunga mkono.
Ninaijua Kaloleni,nina marafiki ndugu na jamaa wanaishi kwenye hizo nyumba za Kaloleni.Mheshimiwa Mbunge Lema katoa sababu za kuupinga mradi ambazo kama ni kweli wa kwanza kulaumiwa ni yeye mwenyewe na chama chake kwa kutoweka maslahi ya wapiga kura na wananchi kwa ujumla wake.CDM ilikuwa na nguvu kubwa kwenye baraza la madiwani huu mradi usingepita kama wasingefukuza madiwani watano na kutoa nafasi kubwa madiwani wa CCM kutoa maamuzi makubwa kwakuwa idadi yao ni kubwa.Ikumbukwe pia CDM walikuwa mabingwa wa kususa vikao vya baraza hapo hapo ni mabingwa wa kuvuta posho again Mheshimiwa Lema alitakiwa ajue athari za kususia vikao.
CDM ilishinda udiwani kata ya Kaloleni suala la nyumba za Kaloleni ambazo kuna kipindi zilimilikiwa na NHC na baadaye kurejeshwa Manispaa linajulikana muda mrefu upo umoja wa wakaazi wa hizo nyumba unaowashirikisha wakaazi wa Kaloleni,Kilombero na Fire Mwenyekiti wake ni Bwana Ole Kashiro na Katibu Mzee Shemdolwa.Mheshimiwa diwani wa CDM Charles "Rasta" alishinda kwa ahadi ya kuwasaidia wakaazi wa hizo nyumba kuuziwa kama walivyouziwa wenzao wa Ngarenaro pia watumishi wa serekali nao pia waliuziwa nyumba maeneo ya Sanawari na Uzunguni.Bahati mbaya ugomvi wa CDM ukamuondoa katika nafasi yake ya udiwani.Mpaka sasa Kaloleni haina diwani kwa maneno rahisi wananchi wa Kaloleni wamenyimwa haki yao ya kuwakilishwa na CDM.Niseme kweli sijui kama huo mradi umegubikwa na ufisadi au ni mbinu za wanasiasa kuchafuana.
Mheshimiwa Lema kama anazo hoja za msingi ni vyema akaziwakilisha kunakohusika eg TAKUKURU au Mahakamani.Ningependa kusikia mbunge wangu akitumia njia sahihi kupinga huo mradi ingawa ni lazima pia ajue nyumba husika hazikidhi viwango vya kisheria kuwapo eneo la Kaloleni.Ukitaka kujenga nyumba eneo la kaloleni ni lazima ujenge ghorofa tatu na kuendelea sasa sijui kama wakaazi wa hizo nyumba wanauwezo wa kujenga ghorofa tatu ?.
[/COLOR][/B]
"Kwanza huyo meya wao aseme lini tenda hii ilitangazwa na ni Watanzania wakazi wa Arusha wangapi walishirikishwa. Kama hilo halikufanyika, siwezi kukubaliana na mpango mzima na lazima tuanze upya," alisema Lema. [/FONT][/COLOR]
Ngongo,
Tatizo lako linajulikana kwamba wewe ni hater, hata Lema aseme nini chenye manufaa lazima utajitahidi kupindisha tu.
Sasa nimekurahisishia kazi, angalia alichosema mbunge wako hapo chini halafu ujipime mwenyewe.
Ni dhahiri Kama ungesoma maelezo ya Lema usingekurupuka kumwaga upupu kwa mara nyingine. Hata kama Lema na madiwani wa chadema hawkuhudhuria vikao vya baraza la madiwani, bado haiwezi kuwa sababu ya kuhalalisha ukiukwaji wa sheria ya manunuzi pamoja na kanunin nyengine zinazoongoza utendaji wa baraza la jiji.
kushabikia ufisadi kama wewe ni sawa na kula nyama ya mtu
Nimewahi kusema tuna tatizo Tanzania, our leaders they are not looking at big picture!!! hilo suala ya kushirikisha wananchi is not about mbunge au mkurugenzi ni jambo la kisheria.... tuache kujadili upupu humu ndani.... sheria inasema lazima tathmini ifanywe na fair compensation ifanyike so what are we discussing here!!! yasipofanyika haya sheria lazima itachukua mkondo wake... sio suala la Lema vs Mkurugenzi.. amkeni waTanzania.
Kwenye "Debate" lazima kuna pande mbili - kuuunga mkono hoja au kupinga hoja; tunachangia ili kukoleza mjadala na wala bandiko la mchangiaji si lazima liwe msimamo wake.
Kuna wakati mwininge nakubali watu wanafikiria kwa kutumia mioyo yao na wala sio akili zao!!! Sheria imepitishwa na bunge ya namna ya kudeal na mambo ya namna hii, Arusha sio ya Kwanza!!! Sasa siku sheria ikivunjwa wananchi wanatakiwa waende kwenye chombo cha kudai haki na hicho chombo hakiko chini ya serikali ni mhimili mwingine!!! so what are we really discussing here!!!
Ndio maana sheria ilitungwa na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, na haki zote zitapatikana kwa kutumia sheria hiyo sio kupitia kwa Lema..... let be serious guys.
Nashauri ungejaribu kurudia tena kusoma vizuri maelezo ya mbunge Lema ili umuelewe vizuri anachomaanisha, haifai kupinga kila kitu kwa kukurupuka na kusukumwa na ushabiki wa kichama.