Lema apinga kuvuliwa ubunge kwa hoja 42 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema apinga kuvuliwa ubunge kwa hoja 42

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpigauzi, Aug 20, 2012.

 1. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Lema apinga kuvuliwa ubunge kwa hoja 42
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Peter Saramba, Arusha
  MAJAJI watatu wa Mahakama ya Rufaa, Natalia Kimaro, Mbarouk Salim Mbarouk na Salum Masati Septemba 20,mwaka huu watapitia kurasa 990 zenye hoja 42 zilizowasilishwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema kupinga kuvuliwa ubunge.

  Awali katika rufaa yake iliyowasilishwa mahakamani kupinga hukumu ya kumvua ubunge iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila Aprili 5, mwaka huu, Lema kupitia kwa wakili wake, Method Kimomogoro aliwasilisha kitabu cha rufaa chenye kurasa 985 na hoja 18 zinazoeleza kwanini anapinga hukumu hiyo, kabla ya kuongeza kitabu kingine cha kurasa tano na hoja za ziada 24 Julai 3, mwaka huu.

  Pamoja na kubeba kumbukumbu zote za mwenendo wa shauri namba 13/2010 na vielelezo vyote vilivyowasilishwa mahakamani na pande zote mbili za wadai na wadaiwa, kitabu hicho cha kurasa 990 pia kimebeba maelezo ya kina na hoja za kuishawishi mahakama ya rufaa kumpa nafuu Lema kwa kutengua hukumu hiyo.

  Kwa mujibu wa kumbukumbu za kimahakama, tayari walalamikaji Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo wamejibu hoja zote za rufaa kupitia kwa mawakili wao Alute Mughwai na Modest Akida.

  Akizungumza kwa njia ya simu jana, Wakili Kimomogoro alithibitisha kukamilisha taratibu zote za kisheria kuhusu rufaa ya mteja wake na kilichosalia ni kusubiri tarehe ya kusikilizwa na uamuzi.

  Kwa mujibu wa hati ya rufaa hiyo, hoja ya kwanza hadi nne zinapinga uamuzi wa Jaji Aloyce Mjulizi aliyesikiliza shauri hilo katika hatua za awali kwa kutupa pingamizi za awali zilizowasilishwa na upande wa utetezi kwenye kesi ya madai namba 13 iliyofunguliwa na wapiga kura watatu waliopinga ushindi wa Lema.

  Miongoni mwahoja hizo ni kuwa wadai, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo hawakuwa na haki kisheria kufungua shauri hilo kwa sababu hakuna haki yao iliyovunjwa kisheria kama wapiga kura.

  Lema anadai aliyekuwa na haki kisheria kulalamikia kauli na maneno ya kashfa na udhalilishaji anazotuhumiwa kutoa kwenye mikutano yake ya kampeni ni aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian ambaye pamoja na kutajwa na mashahidi wote wa wadai, hakufika mahakamani kuthibitisha madai hayo licha ya umuhimu wa ushahidi wake.

  Serikali katika shauri hilo liliwakilishwa na wakili wa serikali, Timon Vitalis na Juma Masanja waliodai aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian ndiye alikuwa na haki kisheria kulalamikia ushindi na maneno ya kashfa yanayodaiwa kutolewa dhidi yake na Lema hoja ambayo Jaji Rwakibarila alitupilia mbali katika hukumu yake iliyozua mjadala baada ya kudaiwa kuvuja kabla ya kusomwa.

  Hoja ya tano hadi 18 zinapinga hukumu ya Jaji Rwakibarila ambapo katika suala la hukumu yake kukosa hadhi kisheria, wakili Kimomogoro anadai hakutolea maamuzi athari za wadai kushindwa kuwasilisha mahakamani CD zinazomwonyesha Lema akitoa maneno ya kashfa na udhalilishaji walizodai kuwa nazo katika hati yao ya madai.

  Kimomogoro anadai Jaji alikosea kwa kutotumia hata kesi moja kama rejea kati ya kesi kadhaa zilizotajwa na mawakili wa pande zote mbili za wadai na wadaiwa.

  Jaji Rwakibarila ambaye ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga pia anadaiwa kukosea kisheria kwa kukubali na kuegemea ushahidi wa mdomo pekee katika hukumu yake bila kuwepo ushahidi wa mazingira, Video wala maandishi kuunga mkono ushahidi wa mdomo.

  Mrufani pia anadai Jaji alikosea kwa kutumia viwango na vigezo tofauti kwa mashahidi wa upande wa wadai na utetezi kwa kukataa ushahidi wa Lema na mashahidi wake kwa madai kuwa walikuwa na maslahi kwa sababu ni wanachama na viongozi wa Chadema lakini akaukubali ushahidi wa wadai na mashahidiwao waliothibitika kuwa ni wanachama na viongozi wa CCM kutengua matokea.

  Lakini kwa mujibu wa wakili Kimomogoro, Lema na viongozi wa juu wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, hoja ya msingi iliyofanya wakate rufaa ni kitendo cha Jaji Rwakibarila kutumia kifungu cha 114 cha sheria za uchaguzi kwa kuagiza taarifa za hukumu hiyo kupelekwa kwa Mkurugenzi wa uchaguzi ikimaanisha Lema hataruhusiwa kupiga wala kupigiwa kura kwa kipindi kisichopungua miaka mitano kinyume na makosa aliyoshtakiwa nayo.

  SOURCE: Mwananhi 20 Aug 2012
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hawa majaji wawili siwafahamu lakni huyu Salum Masati ni jaji wa siku nyingi na majaji wa siku nyingi si ajabu akawa na kadi ya CCM mfukoni mwake. Aloyce Mujulizi amekula pesa za ccm huku akitoa hukumu iliyovunja kwama kwa kukataa ushahidi wa viongozi wa chadema kwa sababu wao ni chadema huku akikubali ushahdi wa viongozi wa ccm akiwemo musa mkangaa yaani ni kichekesho
   
 3. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu hawa Majaji waliosikiliza kesi hii wana walakini. Kama huyu Mujuluzi amechambuliwa vizuri katika ripoti ya Tundundu Lissu.

  JAJI ALOYSIUS MUJULIZI

  Jaji Aloysius Mujulizi alikuwa miongoni mwa watu ishiriniwalioteuliwa Majaji wa Mahakama Kuu mwezi Februari, 2006. Kabla ya uteuzi wake,Jaji Mujulizi alikuwa wakili wa kujitegemea katika kampuni ya mawakili yaIshengoma, Masha, Magai & Mujulizi Advocates (IMMMA) ya Dar es Salaam.Kampuni hii ya mawakili ndiyo iliyoshiriki katika kuanzishwa kwa kampuniiitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. mnamo tarehe 18 Machi 2004. IMMMA Advocatesvile vile walikuwa mawakili wa Tangold Ltd.

  Makampuni haya mawili yanatuhumiwa kutumika kupitishiamabilioni ya fedha zilizoibiwa Benki Kuu ya Tanzania kati ya mwaka 2005 na2006. Kwa mfano, katika kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 naDesemba 10, 2005 kampuni ya Deep Green Finance ilipokea jumla ya shilingi10,484,005,815.39 kutoka akaunti ya kulipia madeni ya nje (EPA) iliyokuwa BenkiKuu ya Tanzania. Katika kipindi hicho hicho, kampuni ya Tangold Ltd. ililipwadola za Marekani 13,736,628.73 kutoka kwenye akaunti hiyo ya EPA. Nyarakazilizowasilishwa BRELA na mawakili wa IMMMA Advocates na kusainiwa na Gavana waBenki Kuu wa wakati huo Daudi Ballali tarehe 20 Mei 2005 zinaonyesha kwambaTangold Limited ilikuwa kampuni ya kigeni kutoka Jamhuri ya Mauritius. Hayayote yalitokea wakati Jaji Mujulizi akiwa wakili mwenza wa IMMMA Advocates.
   
 4. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 180
  Hukumu ya lema hata kwa mimi nisiyejua sheria ni komedi mwanzo hadi mwisho,namshauri lema adili na maombi zaidi kwani Mungu ndiye mweza ya yote!
   
 5. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kila la heri kamanda Lema.
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  watapiga sana chenga ila Mwisho wa siku style zote zitaisha na watamuachia ubunge wake
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Mhimili wa mahakama umeingiliwa na wana siasa,wana kazi kubwasana kuwageuka kwanza na kuwafanya wana siasa wajue wao si ma boss zao kwa kuwaambia nini cha kufanya na wawe huru, wakishamalizana na wana siasa, itabakia kutekeleza sheria kama msumeno ila kwa sasa hakuna lolote, haki itapindishwa tu, angalia Hukumu ya Segerea na Ubungo; Segerea wamebebwa kabisa na Ubungo bado hawamaini kuwa Haki ilitendeka wamekata rufaa wakijua huko mbele watamzima bwana mdogo!
   
 8. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Ugumu wa hukumu hii kuwa ya haki upo hapa majaji wote ni wateuliwa wa rais jk ambaye Lema anamtuhumu kuwa ndio chanzo au ana mkono kwenye kuvuliwa ubunge baada ya juhudi za jk kumshawishi lema agombee Arusha kupitia CCM kushindwa (rejea kikao cha Lema na JK huko Oysterbay) Je majaji wataweka weledi mbele au maslahi binafsi mbele??? lets wait and see!!
   
 9. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Watazunguka kote kwa hila ila ukweli wa mambo utabaki palepale kuwa Lema ni mbunge halali wa Arusha mjini!Hata wangerudia uchaguzi mara mia,bado hawataweza badili upepo wa kisiasa hapa Arusha!Lema atabaki kuwa mbunge halali wa Manispaa/jiji la Arusha.
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Hilo liko wazi kwa 100%

  Mi cjui ni kwamba hawajui kusoma hata alama ya nyakati

   
 11. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Sisi tunamtakia ushindi Lema na tunamwombea Mungu aweze kumshindia
   
 12. H

  Hodarism Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa mahakama hizi na majaji wa JK hakuna jipya
   
 13. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,769
  Trophy Points: 280
  may God bless Godbless Lema.
   
 14. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Lema hakika ur alwayz on our mind.
   
 15. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kila la kheri mh. G Lema.
   
 16. RICARDO KAKA

  RICARDO KAKA JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 867
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Wataruka sana lakini watatua tu!
  "KAMA HAWATANIRUDISHIA UBUNGE WANGU, DR. SLAA ATAGOMBEA JIMBO LA ARUSHA MJINI" ---Godbless LEMA
   
 17. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,207
  Likes Received: 3,621
  Trophy Points: 280
  Politiki,ktk majaji hao 3 aliye makini zaidi ni Jaji Salum Masati!Kumbuka ndiye yeye aliyekubaliana na Mtikila kwenye kesi ya wagombea binafsi kwenye dissident yake kuwa"kwa vile katiba inasema kila mtu ana haki ya kupigiwa kura na kupiga kura kukataa wagombea binafsi ni kuwanyima haki zao za kikatiba za kupigiwa kura"

  Jaji Masati ni jaji makini sana!
   
 18. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye kumpa nafuu bado sijaelewa. Inaonekana kama anaomba hisani na sio kudai haki!

  Na hapo mwisho kwenye red ndio tatizo hasa. Na ilifanywa makusudi!
   
 19. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Lema appears to be of more help to his party now working as a non-MP partyman than when he was serving as an MP. In just a few months he's been out the Parliament, for instance, he's managed to raise funds and win new members for his party from places as far as UK and US--and that he certainly couldn't have achieved had he still been an MP. Additionally, nobody will deny the fact his current across-the-country campaign to promote his party's policies and undermine those of CCM has really proved to be so damaging to the goverment well being that JK is said to be contemplating giving him back his post. Instead of him keeping alive the unrealistic dream of winning his appeal against the verdict that blocked him from the assembly, I propose he focus on the task arguably imperative and profitable he is currently embarking on of strengthening the party health at the grassroots level and setting the public against the CCM rulers.
   
 20. m

  miti Senior Member

  #20
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Lema ni kichwa na tunamkubali sana hata ccm wanamkubali na ndio maana wameamua kumvua ubunge na kumsimamisha asigombee tena zaidi ya hiyo miaka 5. Lema komaa nao ni bora arusha kusiwe na mbunge hata kama ikifika mwaka 2015 kuliko jimbo lichukuliwe na ccm. Poa endelea kuwaburuza hadi haki ipatikane wakizingua tena kata rufaa nyingine .hadi kieleweka.
   
Loading...