Wakuu hawa Majaji waliosikiliza kesi hii wana walakini. Kama huyu Mujuluzi amechambuliwa vizuri katika ripoti ya Tundundu Lissu.
JAJI ALOYSIUS MUJULIZI
Jaji Aloysius Mujulizi alikuwa miongoni mwa watu ishiriniwalioteuliwa Majaji wa Mahakama Kuu mwezi Februari, 2006. Kabla ya uteuzi wake,Jaji Mujulizi alikuwa wakili wa kujitegemea katika kampuni ya mawakili yaIshengoma, Masha, Magai & Mujulizi Advocates (IMMMA) ya Dar es Salaam.Kampuni hii ya mawakili ndiyo iliyoshiriki katika kuanzishwa kwa kampuniiitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. mnamo tarehe 18 Machi 2004. IMMMA Advocatesvile vile walikuwa mawakili wa Tangold Ltd.
Makampuni haya mawili yanatuhumiwa kutumika kupitishiamabilioni ya fedha zilizoibiwa Benki Kuu ya Tanzania kati ya mwaka 2005 na2006. Kwa mfano, katika kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 naDesemba 10, 2005 kampuni ya Deep Green Finance ilipokea jumla ya shilingi10,484,005,815.39 kutoka akaunti ya kulipia madeni ya nje (EPA) iliyokuwa BenkiKuu ya Tanzania. Katika kipindi hicho hicho, kampuni ya Tangold Ltd. ililipwadola za Marekani 13,736,628.73 kutoka kwenye akaunti hiyo ya EPA. Nyarakazilizowasilishwa BRELA na mawakili wa IMMMA Advocates na kusainiwa na Gavana waBenki Kuu wa wakati huo Daudi Ballali tarehe 20 Mei 2005 zinaonyesha kwambaTangold Limited ilikuwa kampuni ya kigeni kutoka Jamhuri ya Mauritius. Hayayote yalitokea wakati Jaji Mujulizi akiwa wakili mwenza wa IMMMA Advocates.